Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Mei 2027 › 1 Mei

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 1 Mei 2027

Jumamosi · Juma la 5 la Pasaka

Sikukuu na watakatifu

Jumamosi ya Juma la 5 la Pasaka

Kumbukumbu ya hiari · Rangi ya liturujia: nyeupe

Mt. Yosefu Mfanyakazi · Kumbukumbu ya hiari

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Mdo 16:1–10

1Paulo pia alipokuja Derbe na Lystra; na tazama, pale palikuwepo na mwanafunzi aitwaye Timotheo, ni Kijana aliyezaliwa na mama wa Kiyahudi ambaye ni muumini na baba yake ni Mgiriki. 2Watu wa Listra na Ikonia walimshudia vizuri. 3Paulo alimtaka ili asafiri naye, hivyo akamchukua na kumtahiri kwa sababu ya Wayahudi waliokuwako huko kwani wote walimjua kuwa baba yake ni Mgiriki. 4Walipokuwa wakienda walipita kwenye miji na kutoa maagizo kwa makanisa ili kuyatii maagizo hayo yaliandikwa na mitume na wazee huko Yerusalemu. 5Hivyo makanisa yakaimarishwa katika imani na walioamini wakaongezeka kwa idadi kila siku. 6Paulo na mwenzake wakaenda Firigia na Galatia, kwani Roho wa Mungu aliwakataza kuhubiri neno huko kwenye jimbo la Asia. 7Walipokaribia Misia, walijaribu kwenda Bithinia, lakini Roho wa Yesu akawakataza. 8Kwa hiyo wakapita Misia wakaja mpaka Mji wa Troa. 9Maono yalimtokea Paulo usiku, kulikuwa na mtu wa Makedonia amesimama, akimwita na kusema “Njoni mtusaidie huku Makedonia”. 10Paulo alipoona maono, mara tukajiandaa kwenda Makedonia, akijua kwamba Mungu alituita kwenda kuwahubiria injili.

Wimbo wa katikati

Zab 100:1–3, 5

1Zaburi ya shukrani. Mpigieni Yahwe kelele za furaha, enyi nchi yote. 2Mtumikieni Yahwe kwa furaha; njoni mbele zake mkiimba kwa furaha. 3Mjue kuwa Yahwe ni Mungu; alituumba, na sisi tu wake. Tu watu wake na kondoo wa malisho yake. 5Maana Yahwe ni mwema; uaminifu wa agano lake wadumu milele na uaminifu wake vizazi na vizazi vyote.

Injili

Yn 15:18–21

18Kama ulimwengu utawachukia, mjuwe kwamba ulinichukia mimi kabla haujawachukia ninyi. 19Kama mngekuwa wa ulimwengu, ulimwengu ungewapenda kama wa kwao; Lakini kwa sababau ninyi sio wa ulimwengu na kwa sababu niliwachagua kutoka katika ulimwengu, ni kwa ajili hii ulimwengu huwachukia. 20Kumbukeni neno ambalo niliwaambia, 'Mtumwa si mkuu kuliko bwana wake.' Ikiwa walinitesa mimi, watawateseni ninyi pia; Kama walishika neno langu, wangelishika la kwenu pia. 21Watawatendeeni mambo haya yote kwa ajili ya jina langu kwa sababu hawamjui yule aliyenituma.

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 1 Mei

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki