Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Aprili 2027 › 5 Aprili
Kalenda ya Kiorthodoksi · 23 Machi (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 5 Aprili 2027
Jumatatu · Wiki ya 4 ya Kwaresima Kuu · Sauti ya 3
Sikukuu na watakatifu
Mtawa Mfiadini Nikoni, askofu, na wanafunzi wake 199 (251)
Kwaresima Kuu
Mfungo mkali (chakula kikavu: mkate, mboga, matunda)
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Saa ya 6
24Yahwe wa majeshi ameapa, ''Hakika, kama nilivyodhamiria, itakuwa kama ilivyo; na kama nilivyo kusudia itakuwa: 25Nitawavunja Waasiria kwa mikono yangu, na kukanyaga milima kwa miguu yangu mwenyewe. Hivyo nira yake itanyanyuliwa juu yao na mzigo juu ya mabega yao.'' 26Huu ni mpango uliokusudiwa katika nchi yote, na huu ndio mkono ulionyanyuliwa juu ya mataifa. 27Kwa maana Yahwe wa majeshi amepanga hivi; ni nani atakayemzia yeye? Mkono wake umenyanyuliwa juu, ni nani atakajemrudisha nyuma? 28Katika miaka ambayo mfalme Ahazi alipokufa, hili ndio tamko lilokuja: 29Msishangilie, enyi wafilisti wote, kwamba fimbo ya kukupigia wewe imevunjika. Maana katika njia ya nyoka atatoka fira, na watoto wake watakuwa moto nyoka wanaopaa. 30Na mtoto wa kwanza wa maskini watachunga kondoo wao kwenye malisho yangu, na wahitaji watalala chini salama. Nitaiuwa mizizi yenu kwa njaa ambayo atawauwa wakazi wenu wote. 31Omboleza, ewe lang, lia, ewe mji; ninyi nyote mtayeyukia mbali, Ufilisti. Maana kutoka kaskazini limetoka wingu la moshi, na hakuna hata mmoja atakaye odoka kwenye nafasi yake. 32Ni kivipi mtu mmoja atamjibu mjumbe wa taifa? Kwamba Yahwe ameipata Sayuni, na ndani yake walionewa watatafuta kimbilio.
Sala ya Jioni: somo
21Yahwe akanusa harufu nzuri ya kuridhisha na akasema moyoni mwake, “ Sita laani tena ardhi kwa sababu ya mwanadamu, ingawa nia za mioyo yao ni mbaya tokea utoto. Wala sita haribu kilakitu chenye uhai, kama nilivyo fanya. 22Wakati nchi isaliapo, majira ya kupanda mbegu na mavuno, baridi na joto, kiangazi na majira ya baridi, mchana na usiku havitakoma.” 9:1Kisha Mungu akambariki Nuhu na wanawe, na kuwaambia, “Zaeni, mkaongezeke, na muijaze nchi. 2Hofu na utisho wenu vitakuwa juu ya kila mnyama aliye hai juu ya nchi, juu ya kila ndege wa angani, juu ya kila kitu kiendacho chini juu ya ardhi, na juu ya samaki wote wa baharini. Vimetolewa katika mikono yenu. 3Kila kitu kiendacho kilicho hai kitakuwa chakula kwa ajili yenu. Kama nilivyo wapa mimea, sasa nawapa kila kitu. 4Lakini msile nyama pamoja na uhai wake - yaani damu yake - ndani yake. 5Lakini kwa ajili ya damu yenu, uhai uliomo katika damu yenu nitataka malipo. Kutoka katika mkono wa kila mnyama nitaitaka. Kutoka katika mkono wa kila mtu, yaani, kutoka katika mkono wa yule ambaye amemuua ndugu yake, nitataka fidia kwa ajili ya uhai wa mtu huyo. 6Yeyote amwagaye damu ya mtu, kwa njia ya mtu damu yake itamwagwa, kwa sababu ilikuwa ni katika mfano wa Mungu kwamba Mungu alimuumba mtu. 7Na hivyo nanyi zaeni na kuongezeka, sambaeni katika inchi yote na muongezeke juu yake.”
Sala ya Jioni: somo
19Mtu mwaminifu atendaye haki ataishi, bali yeye atendaye uovu atakufa. 20Yehova anawachukia wenye ukaidi mioyoni, bali anawapenda wale ambao njia zao hazina makosa. 21Uwe na uhakika juu ya hili- watu waovu hawatakosa adhabu, bali uzao wa wale watendao haki watawekwa salama. 22Kama pete ya dhahabu kwenye pua ya nguruwe ndiyo alivyo mwanamke mzuri asiye na busara. 23Shauku ya wale watendao haki ni matokeo mema, bali watu waovu wanaweza kutumainia ghadhabu tu. 24Kuna yule ambaye hupanda mbegu- atakusanya zaidi; mwingine hapandi- huyo anakuwa masikini. 25Mtu mkarimu atafanikiwa na yule awapaye maji wengine atapata maji yake mwenyewe. 26Watu wanamlaani mtu ambaye hukataa kuuza nafaka, bali zawadi njema hufunika kichwa chake ambaye huuza nafaka. 27Yule ambaye hutafuta mema kwa bidii pia anatafuta kibali, bali yule atafutaye ubaya atapata ubaya. 28Wale wanaotumaini utajiri wataanguka, bali kama jani, wale watendao haki watasitawi. 29Yule ambaye analeta taabu kwenye kaya yake ataurithi upepo na mpumbavu atakuwa mtumishi wa wenye moyo wa hekima. 30Wale watendao haki watakuwa kama mti wa uzima, lakini vurugu huondoa uzima. 31Tazama! Ikiwa wale watendao haki hupokea wanachositahili, je si zaidi kwa waovu na wenye dhambi! 12:1Anayependa mafundisho hupenda maarifa, bali yule anayechukia maonyo ni mpumbavu. 2Yehova humpa fadhila mtu mwema, bali mtu ambaye hufanya mipango ya ufisada atahukumiwa. 3Mtu hawezi kuimarishwa kwa uovu, bali wale watendao haki hawawezi kung'olewa. 4Mke mwema ni taji ya mume wake, bali yule aletaye aibu ni kama ugonjwa unaoozesha mifupa yake. 5Mipango ya wale watendao haki ni adili, bali shauri la mwovu ni udanganyifu. 6Maneno ya watu waovu ni uviziaji unaosubiri nafasi ya kuua, bali maneno ya mwenye haki yatawatunza salama.
Watakatifu wa siku
- Mfiadini wa Kikasisi Makario, padri (1931)
- Wafiadini wa Kikasisi Basili na Stefano, mapadri, Mtawa Mfiadini Eliya, Watawa Wafiadini Anastasia na Barbara, Mfiadini Aleksi (1938)
- Mtakatifu Mtawa Sergio Mwungamaji (1948)
- Wafiadini Fileto, Lidia, mke wake, Makedono, Theoprepio, Kronido na Amfilokio, watoto wao (117-138)
- Mtakatifu Mtawa Nikoni, abati wa Mapango ya Kyiv (1088)
- Mfiadini Basili wa Mangazeya (1600)
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 23 Machi katika kalenda ya kanisa ni 5 Aprili katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki