Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Aprili 2027 › 4 Aprili

Kalenda ya Kiorthodoksi · 22 Machi (kalenda ya Juliani)

Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 4 Aprili 2027

Jumapili · Sauti ya 3

Sikukuu na watakatifu

Jumapili ya 3 ya Kwaresima Kuu

Jumapili ya Kuuheshimu Msalaba Mtukufu

Kwaresima Kuu

Mfungo: pamoja na mafuta

Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.

Masomo ya siku

Injili ya 11 ya Sala ya Alfajiri

Yn 21:15–25

15Baada ya kuwa wamefungua kinywa, Yesu akamwambia Simon Petro, “Simon mwana wa Yohana je, wanipenda mimi kuliko hawa?” Petro akajibu, “Ndiyo, Bwana; “Wewe wajua kuwa mimi nakupenda.” Yesu akamwambia, “Lisha wanakondoo wangu.” 16Akamwambia mara ya pili, “Simon mwana wa Yona, je, wanipenda?” Petro akamwambia, “Ndiyo, Bwana; wewe wajua kuwa nakupenda. “Yesu akamwambia, “Chunga kondoo wangu.” 17Akamwambia tena mara ya tatu, “Simon, mwana wa Yohana, Je wanipenda?” Naye Petro alihuzunika kwa vile alivyomwambia mara ya tatu, “Je Wewe wanipenda?” Naye akamwambia, “Bwana, unajua yote; unajua kuwa nakupenda.” Yesu akamwambia, Lisha kondoo wangu. 18Amini, amini, nakuambia, ulipokuwa kijana ulizoea kuvaa nguo mwenyewe na kwenda kokote ulikotaka; lakini utakapokuwa mzee, utanyosha mikono yako, na mwingine atakuvalisha nguo na kukupeleka usikotaka kwenda.” 19Yesu alisema haya ili kuonesha ni aina gani ya kifo ambacho Petro angemtukuza Mungu. Baada ya kuwa amesema haya, akamwambia Petro, “Nifuate.” 20Petro aligeuka na kumwona yule mwanafunzi ambaye Yesu alimpenda akawafuata- Huyu ndiye aliyekuwa amajiegemeza kwenye kifua cha Yesu wakati wa chakula cha jioni na kumwuliza, “Bwana, ni nani atakayekusaliti?” 21Petro alimwona na kisha akamwuliza Yesu, “Bwana, Huyu mtu atafanya nini?” 22Yesu akamjibu, “Kama nataka abaki mpaka nitakapokuja, hilo linakuhusu nini?” Nifuate.” 23Kwa hiyo habari hii ikaenea miongoni mwa wale ndugu, kwamba mwanafunzi huyo hatakufa. Lakini Yesu hakumwambia Petro kuwa, mwanafunzi huyo hafi, “Kama nataka yeye abaki mpaka nitakapokuja yakuhusu nini?” 24Huyu ndiye mwanafunzi atoaye ushuhuda wa mambo haya, na ndiye aliye andika mambo haya, na tunajua ya kuwa ushuhuda wake ni kweli. 25Kuna mambo mengine mengi ambayo Yesu aliyafanya. Kama kila moja lingeandikwa, nadhani kwamba ulimwengu wenyewe usingetosha kuviweka vitabu ambavyo vingeandikwa.

Waraka

Ebr 4:14–5:6

14Baadaye kuwa na kuhani mkuu aliyeingia katika mbingu, Yesu Mwana wa Mungu, kwa uimara tushikilie imani zetu. 15Kwa kuwa hatuna kuhani mkuu ambaye hawezi kuhisi huruma kwa ajili udhaifu wetu, lakini yeye ambaye kwa njia zote amekuwa akijaribiwa kama sisi, isipokuwa yeye ambaye hana dhambi. 16Na tuje kwa ujasiri katika kiti cha enzi cha neema, ili kwamba tupokee rehema na kupata neema ya kutusaidia wakati wa hitaji. 5:1Kwani kila kuhani mkuu, aliyechaguliwa kutoka miongoni mwa watu, amechaguliwa kusimama badala yao katika vitu vinavyohusiana na Mungu, ili aweze kutoa kwa pamoja zawadi na dhabihu kwa ajili ya dhambi. 2Anaweza kujishughulisha kwa upole na wajinga na wabishi kwa kuwa yeye mwenyewe pia amezungukwa na udhaifu. 3Kwa sababu ya hili, ana wajibu wa kutoa sadaka kwa ajili ya dhambi zake kama afanyavyo kwa dhambi za watu. 4Na hakuna mtu achukuaye heshima hii kwa ajili yake mwenyewe, lakini badala yake, lazima aitwe na Mungu, kama alivyokuwa Haruni. 5Hata Kristo hakujipa heshimu mwenyewe kwa kujifanya mwenyewe kuwa kuhani mkuu. Badala yake, Mungu alisema kwake, “ Wewe ni mwanangu, leo nimekuwa Baba yako.” 6Ni kama asemavyo pia sehemu nyingine, “ Wewe ni kuhani milele baada ya mfumo wa Melkizedeki.”

Injili

Mk 8:34–9:1

34Kisha akauita umati na wanafunzi wake pamoja, na kuwaambia, “Kama kuna mtu anataka kunifuata, ajikane mwenyewe, achukue msalaba wake, na anifuate. 35Kwa kuwa yeyote anayetaka kuyaokoa maisha yake atayapoteza, na yeyote atakayepoteza maisha yake kwa ajili yangu na kwa ajili ya injili, atayaokoa. 36Inamfaidia nini mtu, kupata ulimwengu wote, na kisha kupata hasara ya maisha yake? 37Mtu anaweza kutoa nini badala ya maisha yake? 38Yeyote anioneaye aibu na maneno yangu katika kizazi hiki cha wazinzi na kizazi cha wenye dhambi, Mwana wa Adamu atamwonea aibu atakapokuja katika ufalme wa Baba yake pamoja na malaika watakatifu. 9:1Na alisema kwao, “Hakika nasema kwenu, baadhi yenu kuna watu waliosimama hapa hawataonja mauti kabla ya kuuona ufalme wa Mungu ukija kwa nguvu.”

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 4 Aprili

Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 22 Machi katika kalenda ya kanisa ni 4 Aprili katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki