Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Aprili 2027 › 3 Aprili

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 3 Aprili 2027

Jumamosi · Oktava ya Pasaka

Sikukuu na watakatifu

Jumamosi katika Oktava ya Pasaka

Sherehe · Rangi ya liturujia: nyeupe

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Mdo 4:13–21

13Sasa walipoona ujasiri wa Petro na Yohana, na wakagundua kwamba walikuwa ni watu wakawaida wasio na elimu, walishangaa, wakafahamu kwamba Petro na Yohana wamekuwa pamoja na Yesu. 14Kwa sababu walimwona yule mtu aliyeponywa amesimama pamoja nao, hawakuwa na kitu cha kusema dhidi ya hili. 15Lakini walipokuwa wamekwisha kuwaamuru mitume waondoke mbele ya mkutano wa baraza, walizungumza wao kwa wao. 16Walisema, tutawafanyaje watu hawa? Ni kweli kwamba muujiza wa ajabu umefanyika kupitia wao unajulikana na kila mmoja anayeishi Yerusalemu; hatuwezi kulikataa hilo. 17Lakini, ili kwamba jambo hili lisienee miongoni mwa watu, hebu tuwaonye wasinene tena kwa mtu yeyote kwa jina hili. 18Waliwaita Petro na Yohana ndani na kuwaamuru kamwe wasinene wala kufundisha kwa jina la Yesu. 19Lakini Petro na Yohana walijibu na kuwaambia, “Kama ni sahihi machoni pa Mungu kuwatii ninyi kuliko Mungu, hukumuni wenyewe. 20Maana sisi hatuwezi kuacha kuyanena mambo ambayo tumeyaona na kuyasikia.” 21Baada ya kuwaonya sana Petro na Yohana, waliwaacha waende. Hawakuweza kupata sababu yoyote ya kuwaadhibu, kwa sababu watu wote walikuwa wakimsifu Mungu kwa kile kilichokuwa kimetendeka.

Wimbo wa katikati

Zab 118:1, 14–16, 18–21

1Mshukuruni Yahwe, kwa kuwa ni mwema, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele. 14Yahwe ni nguvu yangu na furaha yangu, na ndiye anaye niokoa. 15Kelele za ushindi zimesikika katika maskani ya wenye haki; mkono wa kuume wa Mungu umeshinda. 16Mkono wa kuume wa Mungu umetukuka; mkono wa kuume wa Yahwe umeshinda. 18Yahwe ameniadhibu vikali; lakini hajaruhusu nife. 19Unifungulie milango ya haki; nitaingia na nitamshukuru Yahwe. 20Hili ni lango la Yahwe; wenye haki hupitia kwalo. 21Nitakushukuru wewe, kwa kuwa ulinijibu, na umekuwa wokovu wangu.

Injili

Mk 16:9–15

9Mapema katika siku ya kwanza ya juma, baada ya kufufuka, alimtokea kwanza Mariamu Magdalena, ambaye kutoka kwake alimtoa mapepo saba. 10Aliondoka na kuwaambia wale ambao walikuwa pamoja naye, wakati walipokuwa wakihuzunika na kutoa machozi. 11Walisikia kwamba ni mzima na ameonekana naye, lakini hawakumwamini. 12Baada ya hayo, akajitokeza katika namna tofauti kwa watu wengine wawili, wakati walipokuwa wakitembea kutoka katika nchi. 13Walienda na kuwaambia wanafunzi wengine waliobaki, lakini hawakuwaamini. 14Yesu baadaye akajitokeza kwa wale kumi na mmoja walipokuwa wameegama katika meza, na akawakemea kwa kutokuamini kwao na ugumu wa mioyo, kwa sababu hawakuwaamini wale waliomwona baada ya kufufuka kutoka kwa wafu. 15Akawaambia, “ Enendeni ulimwenguni mwote, na kuhubiri injili kwa viumbe vyote.

Watakatifu wa 3 Aprili

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki