Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Aprili 2027 › 4 Aprili

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 4 Aprili 2027

Jumapili · Juma la 2 la Pasaka

Sikukuu na watakatifu

Dominika ya 2 ya Pasaka (Dominika ya Huruma ya Mungu)

Dominika · Rangi ya liturujia: nyeupe

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Mdo 4:32–35

32Idadi kubwa ya wale walioamini walikuwa na moyo mmoja na roho moja: na hakuna hata mmoja wao aliyesema kwamba chochote alichomiliki kilikuwa cha kwake mwenyewe; badala yake walikuwa na vitu vyote shirika. 33Kwa nguvu kubwa mitume walikuwa wakiutangaza ushuhuda wao kuhusu ufufuo wa Bwana Yesu, na neema kubwa ilikuwa juu yao wote. 34Hapakuwa na mtu yeyote miongoni mwao aliyepungukiwa na mahitaji, kwa sababu watu wote waliokuwa na hati za viwanja au nyumba, waliviuza na kuleta pesa ya vitu waliyokuwa wameuza 35na kuviweka chini ya miguu ya mitume. Na mgawanyo ulifanywa kwa kila muumini, kulingana na kila mmoja alivyokuwa na hitaji.

Wimbo wa katikati

Zab 118:2–4, 16–18, 22–24

2Israeli na aseme, “Uaminifu wa agano lake wadumu milele.” 3Nyumba ya Haruni na iseme, “Uaminifu wa agano lake wadumu milele.” 4Wafuasi waaminifu wa Yahwe na waseme, “Uaminifu wa agano lake wadumu milele.” 16Mkono wa kuume wa Mungu umetukuka; mkono wa kuume wa Yahwe umeshinda. 17Sitakufa, bali nitaishi na kuyatangaza matendo ya Yahwe. 18Yahwe ameniadhibu vikali; lakini hajaruhusu nife. 22Jiwe ambalo wajenzi walilikataa wajenzi limekuwa msingi. 23Yahwe ndiye afanyaye hili; ni la ajabu machoni petu. 24Hii ni siku ambayo Yahwe ametenda; tutaifurahia na kuishangilia.

Somo la pili

1 Yoh 5:1–6

1Yeyote anayeamini kuwa Yesu ni Kristo amezaliwa na Mungu. Na yeyote ampendaye yeye ambaye ametoka kwa Baba pia huwapenda watoto wake. 2Kwa hili twajua kwamba twawapenda watoto wa Mungu — tunapompenda Mungu na kutekeleza amri zake. 3Hivi ndivyo tunavyompenda Mungu kwamba twazishika amri zake. Na amri zake ni nyepesi. 4Kwa kuwa kila aliyezaliwa na Mungu huushinda ulimwengu. Na huu ndio ushindi wa kuushinda ulimwengu, imani yetu. 5Ni nani aliyeushinda ulimwengu? Ni yule aaminiye kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu. 6Huyu ndiye aliyekuja kwa maji na damu- Yesu Kristo. Hakuja tu kwa maji bali kwa maji na damu.

Injili

Yn 20:19–31

19Na ilipokuwa jioni, siku hiyo, siku ya kwanza ya juma, na milango ikiwa imefungwa mahali wanafunzi walipokuwapo kwa kuwahofia Wayahudi, Yesu alikuja na kusimama katikati yao na kuwaambia, “Amani iwe kwenu.” 20Alipokwisha sema haya akawaonesha mikono yake na ubavu wake. Nao wanafunzi walipomwona Bwana walifurahi. 21Kisha Yesu akawaambia tena, “Amani iwe nanyi. Kama vile Baba alivyonituma mimi, vivyo hivyo nami nawatuma ninyi.” 22Yesu alipokwisha sema hayo, akawavuvia akawaambia, Pokeeni Roho Mtakatifu. 23Yeyote mmsameheye dhambi, wamesamehewa; na wale mtakaowafungia watafungiwa.” 24Thomaso, mmoja wa wale kumi na wawili, aliyeitwa Didimas, hakuwa na wanafunzi wenzake Yesu alipokuja. 25Wale wanafunzi wengine waka mwambia baadaye, “Tumemwona Bwana.” Naye akawambia, “Kama sitaona alama za misumari katika mikono yake, na kuweka vidole vyangu kwenye hizo alama, na pia kuweka mkono wangu kwenye ubavu wake sitaamini.” 26Baada ya siku nane wanafunzi walikuwa chumbani tena, naye Thomaso alikuwa pamoja nao. Wakati milango ilipokuwa imefungwa Yesu alisimama katikati yao. na akasema, “Amani na iwe nanyi.” 27Kisha akamwambia Thomaso, leta kidole chako na uone mikono yangu; leta hapa mikono yako na uweke kwenye ubavu wangu; wala usiwe asiyeamini bali aaminiye.” 28Naye Thomaso akajibu na kumwambia, “Bwana wangu na Mungu wangu.” 29Yesu akamwambia, Kwa kuwa umeniona, umeamini. Wamebarikiwa wao wanaoamini, pasipokuona.” 30Kisha Yesu alifanya ishara nyingi mbele ya wanafunzi, ambazo hazijawahi kuandikwa katika kitabu hiki; 31bali hizi zimeandikwa ili kwamba muweze kuamini kwamba Yesu ndiye Kristo, mwana wa Mungu, na kwamba muaminipo muwe na uzima katika jina lake.

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 4 Aprili

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki