Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Machi 2027 › 25 Machi
Kalenda ya Kiorthodoksi · 12 Machi (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 25 Machi 2027
Alhamisi · Wiki ya 2 ya Kwaresima Kuu · Sauti ya 1
Sikukuu na watakatifu
Mtakatifu Mtawa Theofani Mwungamaji, wa Sigriani (818)
Kwaresima Kuu
Mfungo mkali (chakula kikavu: mkate, mboga, matunda)
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Saa ya 6
1Nyakati zile za kifo cha mfalme Uzzia, nilimuona Bwana akiketi katika kiti cha cha enzi; alikuw juu na mahali palipo inuka, na pindo la vazi lake limejaa hekaluni. 2Juu yake kuna maserafi; kila moja lina mabwa sita; mawili yamefunika uso wake, na mawili yamefunika miguu yake, na mawili ya kurukia. 3Kila mmoja anaitana na mwenzake nakusema, ''Mtakakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu. ni Yahwe wa majeshi! Dunia yote imejaa utukufu wake.'' 4Misingi ya vizingiti imeshtuka kwa sauti ya mtu aliye nje, na njumba imejaa moshi. 5Ndipo nikasema,'' Ole wangu'' ninastahili adhabu maan mimi ni mtu mwenye midomo michafu, na ninaishi na watu wenye midomo michafu, maana macho yangu yamemuona Mfalme, Yahwe, Yahwe wa majeshi.'' 6Ndipo mmoja wa maserafi akaruka juu yangu; mkononi mwake akiwa amebeba makaa ya mawe yanayong'aa, ameyachukuwa kwa koleo mathebauni. 7Akaugusa mdomo wangu kwa makaa ya mawe na akasema, ''Ona, makaa ya mawe yameshika midomo yako; maovu yako yameondolewa, na dhambi zako zimelipiwa kwa hili.'' 8Nilisikia sauti ya Bwana ikisema, Nimtume nani; nani ataenda kwa niaba yetu?'' Ndipo nikasema, Niko hapa; nitume mimi.'' 9Akasema nenda na uwambie watu, ' mnasikiliza lakini hamelewi; anaona lakini hamuangalii. ' 10Nenda ufanye mioyo ya watu hawa kuwa migumu, na masikio yao kuwa mazito, na macho yao kuwa vipofu. Hivyo basi wanaweza kuona kwa macho yao, kusikia kwa masikioa yao, na kuelewa kwa mioyo yao wakajeuka na kuponjwa. 11Ndipo nikasema, ''Bwana, mda gani?'' Akanijibu, mpaka mji itakapopata ajali na kuharibiwa na pasipo wakazi, na nyumba hazina watu, na nchi imeanguka katika ukiwa mtupu, 12na mpaka pale Yahwe atakapo wapeleka watu mbali, na upweke wa nchi ni mkubwa.
Sala ya Jioni: somo
1Hii ni orodha ya vizazi vya Adamu. Katika siku ambayo Mungu alimuumba mtu, aliwaumba katika mfano wake mwenyewe. 2Mwanaume na mwanamke aliwaumba. Akawabariki na akawaita Adam wakati walipoumbwa. 3Wakati Adamu alipokuwa ameishi miaka 130, akamzaa mwana katika sura yake mwenyewe, kwa mfano wake, na akamuita jina lake Sethi. 4Baada ya Adamu kumzaa Sethi, aliishi miaka mia nane. Akawazaa wana wengi waume na wake. 5Adamu akaishi miaka 930 kisha akafariki. 6Wakati Sethi alipokuwa ameishi miaka 105, akamzaa Enoshi. 7Baada ya kumzaa Enoshi, akaishi miaka 807 na akawazaa wana wengi waume na wake. 8Sethi akaishi miaka 912 kisha akafariki. 9Wakati Enoshi alipokuwa ameishi miaka tisini, akamzaa Kenani. 10Baada ya kumzaa Kenani, Enoshi aliishi miaka 815. Akazaa wana wengi wa ume na wake. 11Enoshi aliishi miaka 905 na kisha akafariki. 12Wakati Kanani alipokuwa ameishi miaka sabini, akamzaa Mahalaleli. 13Baada ya kumzaa Mahalaleli, Kenani aliishi miaka 840. Akawazaa wana wengi wa ume na wake. 14Kenani aliishi miaka 910, na kisha akafariki. 15Mahalaleli alipokuwa ameishi miaka sitini na tano, alimzaa Yaredi. 16Baada ya kumzaa Yaredi, Mahalaleli aliishi miaka 830. Akazaa wana wengi wa ume na wake. 17Mahalaleli aliishi miaka 895 na kisha akafariki. 18Yaredi alipokuwa ameishi miaka 162, alimzaa Henoko. 19Baada ya kumzaa Henoko, Yaredi aliishi miaka mianane. Akazaa wana wengi waume na wake. 20Yaredi aliishi miaka 962 na kisha akafariki. 21Henoko alipokuwa ameishi miaka sitini na tano, akamzaa Methusela. 22Henoko akaenenda na Mungu miaka miatatu baada ya kumzaa Methusela. Aliwazaa wana wengi wa ume na wake. 23Henoko aliishi miaka 365. 24Henoko alienenda na Mungu, na kisha alitoweka, kwa kuwa Mungu alimtwaa.
Sala ya Jioni: somo
3Mwanagu, ukinaswa kwa maneno yako mwenyewe, fanya haya ili kujiokoa, kwa kuwa umeangukia kwenye mikono ya jirani yako; nenda unyenyekee na ufanye shauri mbele ya jirani yako. 4Usiruhusu usingizi katika macho yako wala kope za macho yako kusinzia. 5Jiokoe mwenyewe kama swala kutoka katika mkono wa mwindaji, kama ndege kutoka katika mkono wa mwinda ndege. 6Wewe mtu mvivu, mwangalie mchwa, zitafakari njia zake ili kupata busara. 7Hana akida, afisa au mtawala, 8lakini huandaa chakula chake wakati wa joto na wakati wa mavuno huweka hazina ili kula baadaye. 9Ewe mtu mvivu, utalala hata lini? Wakati gani utainuka usingizini?” 10Lala kidogo, sizia kidogo, kunja mikono kupumzika kidogo” - 11ndipo umasikini wako utakapokujia kama mporaji na uhitaji wako kama askari wa vita. 12Mtu asiyefaa-mtu mwovu- huishi kwa kauli za udanganyifu wake, 13akipepesa macho yake, akiashilia kwa miguu yake na kusonta kwa videle vyake. 14Hufanya njama za uovu kwa hila ya moyo wake; daima huchochea faraka. 15Kwa hiyo msiba wake utamkumba kwa ghafula, punde atavunjika vibaya wala hatapona. 16Kuna vitu sita ambavyo Yehova huvichukia, saba ambavyo ni chukizo kwake. 17Macho ya mtu mwenye kiburi, ulimi wa uongo, mikono inayomwaga damu ya watu maasumu, 18moyo unaobuni njama mbaya, miguu inayokimbilia maovu upesi, 19shahidi asemaye uongo na apandaye faraka kati ya ndugu. 20Mwanangu, itii amri ya baba yako na wala usiyaache mafundisho ya mama yako.
Watakatifu wa siku
- Mtakatifu Aleksanda Mwungamaji, padri (1933)
- Wafiadini wa Kikasisi Yohana na Konstantino, mapadri, Mtawa Mfiadini Vladimir (1938)
- Mfiadini wa Kikasisi Sergio, padri (1943)
- Mwenye Haki Finehasi (karibu 1500 K.K.)
- Askofu Mtakatifu Gregori Dialogo, Papa wa Roma (604)
- Mtakatifu Mtawa Simeoni Mwanatheolojia Mpya (1021)
- Ikoni ya Mama wa Mungu ya Lida, isiyofanywa kwa mikono (juu ya nguzo) (karne ya 1)
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 12 Machi katika kalenda ya kanisa ni 25 Machi katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki