Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Machi 2027 › 26 Machi

Kalenda ya Kiorthodoksi · 13 Machi (kalenda ya Juliani)

Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 26 Machi 2027

Ijumaa · Wiki ya 2 ya Kwaresima Kuu · Sauti ya 1

Sikukuu na watakatifu

Kuhamishwa kwa masalia ya Askofu Mtakatifu Nikeforo, Patriarki wa Konstantinopoli (846)

Kwaresima Kuu

Mfungo mkali (chakula kikavu: mkate, mboga, matunda)

Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.

Masomo ya siku

Saa ya 6

Isa 7:1–14

1Siku zile wakati Ahazi mtoto wa Yothani mtoto wa Uzia, mfalme wa Yuda, Rezeni mfalme wa Amramu, na Peka mtoto wa Remaelia, mfalme wa Israeli, walienda Yerusalemu kupigana vita nao, lakini hawakuweza kushinda vita. 2Ilitaarifiwa kwa nyumba ya Daudi kwamba Amramu amejiunga na Efraimu. Moyo wake na moyo watu wake ukatetemeka, kama vile miti ya misitu inavyopepea kwa upepo. 3Ndipo Yahwe akamwambia Isaya, ''Nenda nje na kijana wako, Sheari Jashubu ukaonane na Ahazi mwisho wa mfereji wa birika la juu, katika njia kuu ya uwanja Dobi. 4Mwambie, 'awe makini, awe mtulivu, asiogope au vitisho kwa sababu ya mikia hii miwili ya vingi hivi vitokavyo moshi, kwa sababu ya hasira kubwa ya Resini na Amramu, na mtoto wa Remalia. 5Amramu, Ephraimu, na mtoto wa Remaeli wamepanga mabaya juu yako; wamesema, '' njooni tuwavamie Yuda na kuwaogopesha, 6njooni tujipange na tumueweke mfalme wetu ndani ya Yuda, mtoto wa Tabaeli.'' 7Bwana Yahwe asema, ''haitatokea; haitaonekana, 8maana kichwa cha Amramu ni Damaskasi, na kishwa cha Damaskasi ni Rezini. Ndani ya miaka sitini na tano, ndoto za Ephraimu zitasambaratishwa na hapatakuwa na watu. 9Efraimu ni kichwa Samaria, na kishwa cha Samaria ni mtoto wa Remaria. Na kama hamtasimama imara katika imani yenu, hakika hamtakuwa salama''. 10Bwana akaongea tena na Ahazi, 11''Omba ishara ya Yahwe Mungu wako; omba juu ya hilo kwa kina au kwa kiwango cha juu.'' 12Lakini Ahazi anasema, sintomba wala kumjaribu Yahwe.'' 13Hivyo Isaya akajibu, ''sikilizen, nyumba ya Daudi. Je haijatosha kwa watu kuujaribu uvumilivu wa watu? Je ni lazima kuujaribu uvumilivu wa Mungu? 14Hivyo basi Mungu mwenyewe atawapa yeye mwenywe ishara: ona, mwanamke bikira atapata mimba na kumzaa mtoto, na atamwita Emanueli.

Sala ya Jioni: somo

Mwa 5:32–6:8

32Baada ya Nuhu kuishi miaka miatano, akamzaa Shemu, Hamu, na Yafethi. 6:1Ikawa wakati watu walipoanza kuongezeka juu ya uso wa nchi na wana wa kike wakazaliwa kwao, 2wana wa Mungu walipoona kuwa mabinti wa wanadamu ni wenye kuvutia. waliwachukua kuwa wake zao, kila waliye mchagua. 3Yahwe akaema, “ roho yangu haitasalia kwa mwanadamu milele, kwa kuwa wao ni nyama. Wataishi miaka 120.” 4Majitu makubwa yalikuwa juu ya uso wa nchi nyakati hizo, na hata baada ya hapo. Hii ilitokea wakati wana wa Mungu walipowaoa binti za wanadamu, na kupata watoto pamoja nao. Hawa walikuwa watu hodari zamani, watu wenye sifa. 5Yahwe akaona kwamba uovu wa watu umezidi katika nchi, na kwamba mawazo ya mioyo yao daima inaelekea tu katika uovu. 6Yahwe akajuta kuwa amemuumba mwanadamu juu ya nchi, na ikamuhuzunisha moyo wake. 7Kwa hiyo Yahwe akasema, “Nitamfutilia mbali mwanadamu ambaye nimemuumba katika uso wa nchi; mwanadamu na wanyama wakubwa, na vitambaavyo na ndege wa angani, kwa kuwa nimehuzunika kuwa nimeviumba.” 8Lakini Nuhu akapata neema ya upendeleo machoni pa Yahwe.

Sala ya Jioni: somo

Mit 6:20–7:1

20Mwanangu, itii amri ya baba yako na wala usiyaache mafundisho ya mama yako. 21Uyafunge katika moyo wako siku zote; yafunge kwenye shingo yako. 22utembeapo, yatakuongoza; ulalapo yatakulinda, na uamkapo yatakufundisha. 23Maana amri ni taa, na mafundisho ni nuru; kinga za kuadilisha za njia ya uzima. 24Yanakulinda dhidi ya mwanamke malaya, dhidi ya maneno laini ya uzinzi. 25Moyoni mwako usiutamani uzuri wake wala usitekwe katika kope zake. 26Kulala na malaya inaweza kugharimu bei ya kipande cha mkate, lakini mke wa mtu mwingine inagharimu uzima wako wote. 27Je mtu anaweza kubeba moto katika kifua chake bila kuuguza mavazi yake? 28Je mtu anaweza kutembea juu ya makaa bila kuchomwa miguu yake? 29Ndivyo alivyo mtu alalaye na mke wa jirani yake; yule alalaye na huyo mke hatakosa adhabu. 30Watu hawawezi kumdharau mwizi kama anaiba ili kukidhi hitaji lake la njaa. 31Walakini akimatwa, atalipa mara saba ya kile alichoiba; lazima atoe kila kitu cha thamani katika nyumba yake. 32Mtu anayefanya uzinzi hana akili; hufanya hiyo kwa uharibifu wake mwenyewe. 33Anasitahili aibu na majeraha na fedheha yake haiwezi kuondolewa. 34Maana vivu humghadhibisha mtu; hatakuwa na huruma wakati wa kulipa kisasi chake. 35Ujapompa zawadi nyingi, hatakubali mbadala wa kusuruhishwa wala kulipwa. 7:1Mwanangu, yatunze maneno yangu na ndani yako udhihifadhi amri zangu.

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 26 Machi

Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 13 Machi katika kalenda ya kanisa ni 26 Machi katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki