Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Machi 2027 › 8 Machi
Kalenda ya Kiorthodoksi · 23 Februari (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 8 Machi 2027
Jumatatu · Wiki ya Kuacha Jibini · Sauti ya 7
Sikukuu na watakatifu
Jumatatu ya Wiki ya Kuacha Jibini
Wiki ya Kuacha Jibini
Bila nyama; maziwa, mayai na samaki vinaruhusiwa
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Waraka
1Mzee, kwa Gayo mpenzi, ninayempenda katika kweli. 2Mpendwa, nakuombea ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya njema, kama vile roho yako inavyofanikiwa. 3Maana nilifurahi sana wakati nilipoambiwa na ndugu waliokuja na kutoa ushuhuda juu ya kweli yako, kama vile unavyoenenda katika kweli. 4Sina furaha kubwa zaidi ya hii, kusikia kwamba watoto wangu wanatembea katika kweli. 5Mpendwa, unaenenda kwa uaminifu unapowahudumia ndugu na wageni, 6ambao wametoa ushuhuda wa upendo wako mbele ya kanisa. Unafanya vizuri kuwasafirisha katika safari zao kwa namna ambayo inampendeza Mungu. 7Kwa sababu kwa ajili ya Jina, walienda bila kuchukua kitu chochote kutoka kwa watu wa Mataifa. 8Hivyo, tunatakiwa kuwakaribisha watu kama hawa, ili tuwe watenda kazi wenza kwa ajili ya kweli. 9Nililiandikia kusanyiko jambo fulani, lakini Diotrofe, anayependa kuwa wa kwanza miongoni mwao, hakubaliani na sisi. 10Hivyo, kama nikija nitayakumbuka matendo yake anayoyafanya, jinsi anavyosema maneno mabaya kinyume nasi. Hajaridhika na matendo haya, yeye mwenyewe hawapokei ndugu. Hata huwakataza wengine ambao wanatamani kuwakaribisha hao ndugu na kuwafukuza watoke kwenye kusanyiko. 11Mpenzi, usiige kilicho kibaya, bali iga kilicho chema. Yeye atendaye mema ni wa Mungu; na yeye atendaye mabaya hajamwona Mungu. 12Demetrio ameshuhudiwa na wote na kweli yenyewe. sisi pia ni mashahidi, na unajua kuwa ushahuhuda wetu ni wa kweli. 13Ninayo mambo mengi ya kukuandikia, lakini sipendi kukuandikia kwa kalamu na wino. 14Bali ninatarajia kukuona hivi karibuni, na tutaongea nawe ana kwa ana. 15Amani iwe pamoja nawe. Marafiki wanakusalimu. Wasalimu marafiki kila mmoja kwa jina lake.
Injili
29Ikawa alipokaribia Bethfage na Bethania, karibu na mlima wa Mizeituni, aliwatuma wanafunzi wake wawili, 30akisema: 'Nendeni katika kijiji cha jirani. Mkiingia, mtakuta mwana-punda hajapandwa bado. Mfungueni, mkamlete kwangu. 31Kama mtu akiwauliza, 'Mbona mnamfungua? ' Semeni, “Bwana anamhitaji. '' 32Wale waliotumwa wakaenda wakamwona mwana-punda kama Yesu alivyokuwa amewaambia. 33Walipokuwa wanamfungua mwana punda wamiliki wakawaambia, 'Kwa nini mnamfungua mwana punda huyu?' 34Wakasema, 'Bwana anamhitaji. ' 35Basi, wakampelekea Yesu, wakatandika nguo zao juu ya mwana punda na wakampandisha Yesu juu yake. 36Alipokuwa akienda watu wakatandaza mavazi yao barabarani. 37Alipokuwa anateremka mlima wa Mizeituni, jumuiya yote ya wanafunzi wakaanza kushangilia na kumtukuza Mungu kwa sauti kubwa, kwa sababu ya mambo makuu waliyoyaona, 38wakisema, 'Ndiye mbarikiwa Mfalme ajaye kwa jina la Bwana! Amani mbinguni, na utukufu juu!' 39Baadhi ya Mafarisayo katika mkutano wakamwambia, Mwalimu, wanyamazishe wanafunzi wako. ' 40Yesu akajibu, akasema, 'Nawaambieni, kama hawa wakinyamaza, mawe yatapaza sauti. ' 22:7Siku ya mikate isiyotiwa chachu ikafika, ambapo kondoo wa Pasaka lazima atolewe. 8Yesu akawatuma Petro na Yohana, akasema, “Nendeni mkatuandalie chakula cha Pasaka ili tuje tukile.” 9Wakamuuliza, “Wapi unataka tuyafanyie hayo maandalizi?” 10Akawajibu, “Sikilizeni, mtakapokuwa mmeingia mjini, mwanamume ambaye amebeba mtungi wa maji atakutana na ninyi. Mfuateni kwenye nyumba ambayo ataingia. 11Kisha mwambieni bwana wa nyumba, “Mwalimu anakwambia, “Kiko wapi chumba cha wageni, mahali ambapo nitakula Pasaka na wanafunzi wangu?” 12Atawaonyesha chumba cha ghorofani ambacho kiko tayari. Fanyeni maandalizi humo.” 13Hivyo wakaenda, na wakakuta kila kitu kama alivyowaambia. Kisha wakaandaa chakula cha Pasaka. 14Muda ulipofika alikaa na wale mitume. 15Kisha akawaambia, “Nina shauku kubwa ya kula sikukuu hii ya Pasaka na ninyi kabla ya kuteswa kwangu. 16Kwa maana nawaambieni, sitakula tena mpaka itakapotimizwa katika ufalme wa Mungu.” 17Kisha Yesu akachukua kikombe, na alipokwisha kushukuru, akasema, “Chukueni hiki, na mgawane ninyi kwa ninyi. 18Kwa maana nawaambia, sitakunywa tena mzao wa mzabibu, mpaka ufalme wa Mungu utakapokuja.” 19Kisha akachukua mkate, na alipokwisha kushukuru, akaumega, na kuwapa, akisema, “Huu ni mwili wangu ambao umetolewa kwa ajili yenu. Fanyeni hivi kwa kunikumbuka mimi.” 20Akachukua kikombe vivyo hivyo baada ya chakula cha usiku akisema, “Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu, ambayo imemwagika kwa ajili yenu. 21Lakini angalieni. Yule anisalitie yuko pamoja nami mezani. 22Kwa maana Mwana wa Adamu kwa kweli aenda zake kama ilivyokwisha amuliwa. Lakini ole kwa mtu yule ambaye kupitia yeye Mwana wa Adamu asalitiwa!” 23Wakaanza kuulizana wao kwa wao, nani miongoni mwao ambaye angefanya jambo hili. 24Kisha yakatokea mabishano katikati yao kwamba ni nani anaye dhaniwa kuwa mkuu kuliko wote. 25Akawaambia, “Wafalme wa watu wa mataifa wana ubwana juu yao, na wale mwenye mamlaka juu yao wanaitwa waheshimiwa watawala. 26Lakini haitakiwi kabisa kuwa hivi kwenu ninyi. Badala yake, acha yule ambaye ni mkubwa kati yenu awe kama mdogo. Na yule ambaye ni wa muhimu sana awe kama atumikaye. 27Kwa sababu yupi mkubwa, yule akaaye mezani au yule anayetumika? Je si yule aketie mezani? Na mimi bado ni kati yenu kama atumikaye. 28Lakini ninyi ndio ambao mmeendelea kuwa nami katika majaribu yangu. 29Nawapa ninyi ufalme, kama vile Baba alivyonipa mimi ufalme, 30kwamba mpate kula na kunywa mezani kwangu kwenye ufalme wangu. Na mtakaa kwenye viti vya enzi mkizihukumu kabila kumi na mbili za Israel. 31Simoni, Simoni, fahamu kwamba, Shetani ameomba awapate ili awapepete kama ngano. 32Lakini nimekuombea, kwamba imani yako isishindwe. Baada ya kuwa umerudi tena, waimarishe ndugu zako.” 33Petro akamwambia, “Bwana, niko tayari kwenda na wewe gerezani na hata katika mauti.” 34Yesu akajibu, “Nakwambia, Petro, Jogoo hatawika leo, kabla hujanikana mara tatu kwamba unanijua.” 35Kisha Yesu akawaambia, “Nilipowapeleka ninyi bila mfuko, kikapu cha vyakula, ua viatu, je mlipungukiwa na kitu?” Wakajibu “Hakuna.” 36Kisha akawaambia, “Lakini sasa, kila mwenye mfuko, na auchukue pamoja na kikapu cha vyakula. Yule ambaye hana upanga imempasa auze joho lake anunue mmoja. 37Kwa sababu nawaambia, yote ambayo yameandikwa kwa ajili yangu lazima yatimilike, 'Na alichukuliwa kama mtu ambaye anavunja torati.' Kwa sababu kile kilichotabiriwa kwa ajili yangu kinatimizwa.” 38Kisha wakasema, “Bwana, tazama! Hizi hapa panga mbili.” Na akawaambia”yatosha.” 39Baada ya chakula cha usiku, Yesu aliondoka, kama ambavyo amekuwa akifanya mara kwa mara, akaenda mlima wa Mzeituni, na wanafunzi wakamfuata.
Watakatifu wa siku
- Mfiadini wa Kikasisi Polikarpo, Askofu wa Smirna (167)
- Wafiadini wa Kikasisi Aleksi, Nikolao, Mikaeli, mapadri, na Mfiadini Sergio (1938)
- Mtakatifu Mtawa Aleksanda, mtawa, mkuu wa monasteri ya “Wasiolala” († karibu 430)
- Watakatifu Watawa Yohana, Antioko, Antonino, Musa, Zebina, Polikronio, Musa mwingine na Damiani, wakaa jangwani wa Shamu (karne ya 5)
- Mtakatifu Mtawa Polikarpo wa Bryansk (1620-1621)
- Ikoni ya Mama wa Mungu ya Kipro katika kijiji cha Stromyn, mkoa wa Moscow
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 23 Februari katika kalenda ya kanisa ni 8 Machi katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki