Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Februari 2027 › 17 Februari

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 17 Februari 2027

Jumatano · Juma la 1 la Kwaresima

Sikukuu na watakatifu

Jumatano ya Juma la 1 la Kwaresima

Kumbukumbu ya hiari · Rangi ya liturujia: zambarau

Waanzilishi Saba Watakatifu wa Shirika la Watumishi wa Maria · Ukumbusho

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Yon 3:1–10

1Neno la Bwana likamjia Yona mara ya pili, akisema, 2“Ondoka, uende Ninawi, mji ule mkubwa, na uhubiri ujumbe ule ambao nitakuagiza.” 3Basi Yona akaondoka akaenda Niniawi kwa kutii neno la Bwana. Sasa Ninawi ilikuwa mji mkubwa sana, ilikuwa safari ya siku tatu. 4Yona akaanza kuingia ndani ya mji, na baada ya safari ya siku, akapaza sauti, akasema, “Katika siku arobaini Ninawi itaangamizwa.” 5Watu wa Ninawi walimwamini Mungu na wakatangaza kufunga. Wote hwakavaa nguo za magunia, kutoka aliyemkubwa hata mdogo. 6Mapema habari zilimfikia mfalme wa Ninawi. Akasimama kutoka kiti chake cha enzi, akavua vazi lake, akajivika magunia, akaketi katika majivu. 7Alitoa tangazo ambalo lilsemalo, “katika mji wa Ninawi, kwa mamlaka ya mfalme na wakuu wake, msiruhusu mtu wala mnyama, ng'ombe wala kundi, asionje kitu chochote. Wao wasile wala kunywe maji. 8Lakini watu na wanyama wawe wamefunikwa kwa magunia na walie kwa sauti kubwa kwa Mungu. Kila mtu ageuke na kuacha njia yake mbaya na kutoka katika udhalimu uliyopo mikononi mwake. 9Nani anajua? Mungu anaweza kurejea na kubadili mawazo yake na kuacha ghadhabu yake kali ili tusiangamie.” 10Mungu akaona yale waliyoyafanya, wakaziacha njia zao mbaya. Kwa hiyo Mungu alibadili mawazo yake juu ya adhabu aliyowaambia angewafanyia, nae hakufanya hivyo.

Wimbo wa katikati

Zab 51:1–2, 10–11, 16–17

1Kwa kiongozi wa muziki. Zaburi ya Daudi; wakati nabii Nathani amekuja kwake baada ya kusikia kuwa alilala na Bathsheba. Unirehemu, Mungu, kwa sababu ya uaminifu wa agano lako; kwa ajili ya wingi wa matendo yako ya rehema, uyafute makosa yangu. 2Unioshe kabisa uovu wangu na unisafishe dhambi zangu. 10Uniumbie moyo safi, Mungu, na uifanye upya roho ya haki ndani yangu. 11Usiniondoe uweponi mwako, na usimuondoe roho Mtakatifu ndani yangu. 16Kwa maana wewe haufurahishwi katika sadaka, vinginevyo ningekutolea sadaka; wewe hauwi radhi katika sadaka ya kuteketezwa. 17Sadaka ya Mungu ni roho iliyovunjika. Wewe, Mungu hautadharau moyo uliopondeka na kujutia.

Injili

Lk 11:29–32

29Wakati umati wa watu wanakusanyika na kuongezeka, Yesu akaanza kusema “ Kizazi hiki ni kizazi cha uovu. Hutafuta ishara, na hakuna ishara watayopewa zaidi ya ile ishara ya Yona. 30Maana kama Yona alivyokuwa ishara kwa watu wa Ninawi, ndivyo na Mwana wa Adamu atakavyokuwa ishara kwa kizazi hiki 31Malkia wa Kusini atasimama siku ya hukumu na watu wa kizazi hiki na kuwahukumu wao, kwani yeye alitoka katika mwisho wa nchi ili aje asikilize hekima za Solomoni, na hapa yuko aliye mkuu kuliko Solomoni. 32Watu wa Ninawi watasimama katika hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki siku ya hukumu watakihukumu, kwani wao walitubu kwa mahubiri ya Yona, na tazama, hapa yuko aliye mkuu kuliko Yona.

Watakatifu wa 17 Februari

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki