Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Februari 2027 › 18 Februari
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 18 Februari 2027
Alhamisi · Juma la 1 la Kwaresima
Sikukuu na watakatifu
Alhamisi ya Juma la 1 la Kwaresima
Siku ya kawaida · Rangi ya liturujia: zambarau
Masomo ya siku
Somo la kwanza
Haimo katika tafsiri hii
Wimbo wa katikati
1Zaburi ya Daudi. Nitakushukuru kwa moyo wangu wote; mbele ya miungu nitakuimbia sifa. 2Nitasujundu mbele ya hekalu lako takatifu na kulishukuru jina lako kwa ajili ya uaminifu wa agano lako na kwa uaminifu wako. Umelifanya muhimu zaidi neno lako na jina lako kuliko kitu chochote. 3Siku ile niliyo kuita, ulinijibu; ulinitia moyo na kuitia nguvu nafsi yangu. 7Nijapopita katikati ya hatari, wewe utauhifadhi uhai wangu; utanyoosha mkono wako dhidi ya hasira ya adui zangu, na mkono wako wa kuume utaniokoa. 8Yahwe yuko pamoja nami hadi mwisho; uaminifu wa agano lako, Yahwe, wadumu milele. Usiwaache wale ambao mikono yako imewaumba.
Injili
7Omba, nawe utapewa. Tafuta, nawe utapata. Bisha hodi, na wewe utafunguliwa. 8Kwa yeyote anayeomba, hupokea. Na kwa yeyote anayetafuta, hupata. Na kwa mtu ambaye anayebisha hodi, atafunguliwa. 9Au kuna mtu miongoni mwenu ambaye, ikiwa mtoto wake amemwomba kipande cha mkate atampa jiwe? 10Au ikiwa atamwomba samaki, na yeye atampa nyoka? 11Kwa hiyo, ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu zawadi nzuri, Je! Ni kiasi gani zaidi Baba aliye mbinguni atawapa vitu vizuri wale wanao muomba yeye? 12Kwa sababu hiyo, unapotaka kufanyiwa kitu chochote na watu wengine, nawe pia itakupasa kuwafanyia hivyo hivyo wao. Kwa kuwa hiyo ni sheria na manabii.
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki