Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Februari 2027 › 17 Februari
Kalenda ya Kiorthodoksi · 4 Februari (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 17 Februari 2027
Jumatano · Wiki ya 38 baada ya Pentekoste · Sauti ya 4
Sikukuu na watakatifu
Baada ya Sikukuu ya Kuingia kwa Bwana Hekaluni
Siku ya mfungo
Samaki wanaruhusiwa
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Waraka
1Kwa hiyo, kwa kuwa Kristo aliteseka katika mwili, jivikeni silaha za nia ile ile. Yeye aliyeteseka katika mwili ameondokana na dhambi. 2Mtu huyu haendelei tena kuishi katika tamaa za mwili, bali kwa mapenzi ya Mungu, kwa maisha yake yaliyosalia. 3Kwa kuwa muda uliopita umetosha kutenda mambo ambayo wamataifa wanataka kufanya- ufisadi, nia mbaya, ulevi, ulafi, sherehe za kipagani na ibada za sanamu zenye machukizo. 4Wanafikiri ni ajabu mnapojiepusha kutenda mambo hayo pamoja nao, hivyo wananena maovu juu yenu. 5Watatoa hesabu kwake aliye tayari kuhukumu walio hai na wafu. 6Kwa kusudi hili injili ilihubiriwa kwao waliokwisha kufa, kwamba ijapokuwa walikwisha hukumiwa katika miili yao kama wanadamu, ili waweze kuishi kulingana na Mungu katika roho. 7Mwisho wa mambo yote unakuja. Kwa hiyo, mwe na ufahamu ulio sahihi, na iweni na nia njema kwa ajili ya maombi yenu. 8Kabla ya mambo yote, eweni na bidii katika upendo kwa kila mmoja, kwa kuwa upendo hautafuti kufunua dhambi za wengine. 9Onyesheni ukarimu kwa kila mmoja bila kunung'unika. 10Kama ambavyo kila mmoja wenu alivyopokea karama, itumieni katika kuhudumiana, kama wasimamizi wema wa karama nyingi zilizotolewa bure na Mungu. 11Kama mtu akiongea, na iwe kama mausia ya Mungu, na kama mtu akihudumu, na iwe kama uwezo aliopewa na Mungu, ili kwamba kwa kila jambo Mungu apate kutukuzwa kupitia Yesu Kristo. Utukufu na uweza vina Yeye milele na milele. Amina.
Injili
28Mmoja wa waandishi alikuja na kuyasikia mazungumzo yao; aliona kwamba Yesu aliwajibu vema. Alimwuliza, “Je! ni amri ipi iliyo ya muhimu zaidi katika zote?” 29Yesu alimjibu, “Iliyo ya muhimu ni hii, “Sikia, Israeli, Bwana Mungu wetu, Bwana ni mmoja. 30Lazima umpende Bwana Mungu wako, kwa moyo wako yote, kwa roho yako yote, kwa akili yako yote, na kwa nguvu zako zote.' 31Amri ya pili ni hii, 'Lazima umpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe.' Hakuna amri nyingine kuu zaidi ya hizi.” 32Mwandishi akasema, “Vema Mwalimu! Umesema kweli kwamba Mungu ni mmoja, na kwamba hakuna mwingine zaidi yake. 33Kumpenda yeye kwa moyo wote, na kwa ufahamu wote na kwa nguvu zote, na kumpenda jirani kama mwenyewe, ni muhimu mno kuliko matoleo na dhabihu za kuteketeza.” 34Wakati Yesu alipoona ametoa jibu la busara, alimwambia, “Wewe hauko mbali na ufalme wa Mungu.” Baada ya hapo hakuna hata mmoja aliye thubutu kumwuliza Yesu maswali yoyote. 35Na Yesu alijibu, wakati alipokuwa akifundisha katika hekalu, akasema, “Je! waandishi husemaje kuwa Kristo ni mwana wa Daudi? 36Daudi mwenyewe katika Roho Mtakatifu, alisema, 'Bwana alisema kwa Bwana wangu, keti katika mkono wangu wa kuume, mpaka niwafanye maadui wako kuwa chini ya miguu yako.' 37Daudi mwenyewe humwita Kristo, 'Bwana' Je! ni mwana wa Daudi kwa jinsi gani?” Na kusanyiko kuu lilimsikiliza kwa furaha.
Watakatifu wa siku
- Mtakatifu Mtawa Isidori wa Pelusio (karibu 436-440)
- Mwana Mkuu wa Mfalme Mwaminifu Georgi (Yuri) Vsevolodovich wa Vladimir (1238)
- Mtakatifu Mtawa Kirilo wa Novoyezero (1532)
- Mfiadini wa Kikasisi Methodio, Askofu wa Petropavlovsk (1921)
- Wafiadini wa Kikasisi Eustathio, Yohana, Aleksanda, Sergio, Yohana, Theodoro, Aleksanda, Nikolao, Aleksi, Nikolao, Aleksi, Aleksanda, Arkadio, Boris, Mikaeli, Nikolao, Aleksi, Andrea, Demetrio, Yohana, Petro, mapadri, Mtawa Mfiadini Serafim, Watawa Wafiadini Rafaela, Ekaterina na Ana, Wafiadini Yohana, Basili, Demetrio, Demetrio na Theodoro (1938)
- Mfiadini Yadoro (karne ya 3)
- Mfiadini wa Kikasisi Ibrahimu, Askofu wa Arbela (karibu 344-347)
- Mtakatifu Mtawa Nikolao Mwungamaji, abati wa Studion (868)
- Watakatifu Watawa Ibrahimu na Koprio wa Pechenga, wa Vologda (karne ya 15)
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 4 Februari katika kalenda ya kanisa ni 17 Februari katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki