Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Februari 2027 › 16 Februari
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 16 Februari 2027
Jumanne · Juma la 1 la Kwaresima
Sikukuu na watakatifu
Jumanne ya Juma la 1 la Kwaresima
Siku ya kawaida · Rangi ya liturujia: zambarau
Masomo ya siku
Somo la kwanza
10Maana kama mvua na theluji zishukavyo chini kutoka mbinguni na hazirudi tena pale isipokuwa kueneza nchi na kufanya uzalishaji na chipukizi na kutoa mbegu kwa wakulima waliopanda na mkate kwa walaji, 11hivyo neno langu litakuwa linalotoka kwenye mdomo wangu: halitanirudia tena mimi bure, Lakini itatimiza lilie nililokusudia, na litatimiza lile nililolituma.
Wimbo wa katikati
3Msifuni Yahwe pamoja nami, kwa pamoja tuliinue jina lake. 4Nilimuomba Yahwe msaada naye akanijibu, akanipa ushindi juu ya hofu yangu yote. 5Wale wanao mtazama yeye wana furaha, na nyuso zao hazina aibu. 6Huyu mtu aliye onewa alilia na Yahwe akamsikia na kumuokoa kwenye matatizo yake yote. 15Macho ya Yahwe yako kwenye haki na masikio yake huelekea kulia kwao. 16Uso wa Yahwe uko kinyume na wale watendao uovu, kuikatilia mbali kumbukumbu yao duniani. 17Wenye haki hulia na Yahwe husikia na kuwaokoa kwenye matatizo yao yote. 18Yahwe yu karibu nao waliovunjika moyo, naye huwaokoa waliogandamizwa rohoni.
Injili
7Na unapokuwa ukiomba, usirudie rudie maneno yasiyo na maana kama mataifa wanavyofanya, kwa kuwa wanafikiri kwamba watasikiwa kwa sababu ya maneno mengi wanayosema. 8Kwa hiyo, usiwe kama wao, kwa kuwa Baba yako anatambua mahitaji yako hata kabla hujaomba kwake. 9Hivyo basi omba hivi: Baba yetu uliye mbinguni, ulitukuze jina lako. 10Ufalme wako uje, mapenzi yako yafanyike hapa duniani kama huko mbinguni. 11Utupatiye leo mkate wetu wa kila siku. 12utusamehe deni zetu, kama nasi tunavyowasamehe wadeni wetu. 13Na usitulete katika majaribu, lakini utuepushe kutoka kwa yule mwovu.' 14Ikiwa mtawasemehe watu makosa yao, Baba yako aliye mbinguni pia atawasamehe ninyi. 15Lakini ikiwa hamtawasamehe makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe makosa yenu.
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki