Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Januari 2027 › 27 Januari

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 27 Januari 2027

Jumatano · Juma la 3 la Mwaka

Sikukuu na watakatifu

Jumatano ya Juma la 3 la Mwaka

Kumbukumbu ya hiari · Rangi ya liturujia: kijani

Mt. Angela Merici, bikira · Kumbukumbu ya hiari

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Ebr 10:11–18

11Ni kweli, kila kuhani husimama kwa huduma siku kwa siku, akitoa dhabihu ile ile, ambayo, kwa vyovyote, kamwe isingeweza kuziondoa dhambi. 12Lakini baada ya Kristo kutoa dhabihu mara moja kwa dhambi milele yote, aliketi mkono wa kuume wa Mungu, 13akisubiri mpaka maadui zake watiwe chini na kufanywa kiti kwa ajili ya miguu yake. 14Kwa kuwa kwa njia ya toleo moja amewakamilisha milele wale ambao wametengwa kwa Mungu. 15Na Roho Mtakatifu pia ashuhudia kwetu. Kwa kuwa kwanza alisema, 16“Hili ni agano nitakalofanya pamoja nao baada ya siku hizo; asema Bwana: nitaweka sheria zangu ndani ya mioyo yao, na nitaziandika katika akili zao”. 17Kisha alisema, “Hawatazikumbuka tena dhambi na matendo yao mafu”. 18Sasa mahali palipo na msamaha kwa hawa, hakuna tena dhabihu yoyote kwa ajili ya dhambi.

Wimbo wa katikati

Zab 110:1–4

1Zaburi ya Daudi. Yahwe humwambia bwana wangu, “Kaa mkono wangu wa kuume mpaka nitakapowaweka adui zako chini ya miguu yako.” 2Yahwe atainyosha fimbo ya nguvu yako toka Sayuni; utawale kati ya adui zako. 3Siku ile ya uweza wako watu wako watakufuata wakiwa katika mavazi matakatifu ya hiari yao wenyewe; tokea tumbo la alfajiri ujana wako utakuwa kwako kama umande. 4Yahwe ameapa, na hatabadilika: “Wewe ni kuhani milele, baada ya namna ya Melkizedeki.”

Injili

Mk 4:1–20

1Tena alianza kufundisha kandokando ya bahari. Na umati mkubwa ulikusanyika ukamzunguka, akaingia ndani ya mtumbwi baharini, na kukaa. Umati wote walikuwa pembeni mwa bahari ufukweni. 2Na akawafundisha mambo mengi kwa mifano, na akasema kwao kwa mafundisho yake. 3Sikilizeni, mpanzi alienda kupanda. 4Alipokuwa akipanda, baadhi ya mbegu zilianguka njiani, na ndege wakaja wakazila. 5Mbegu zingine zilianguka kwenye mwamba, ambako hapakuwa na udongo mwingi. Mara zikanyauka, kwa sababu hazikuwa na udongo wakutosha. 6Lakini jua lilipochomoza, zilinyauka, na kwa sababu hazikuwa na mzizi, zilikauka. 7Mbegu ziingine zilianguka katikati ya miiba. Miiba ilikua na ikazisonga, na hazikuzaa matunda yeyote. 8Mbegu zingine zilianguka kwenye udongo mzuri na zikazaa matunda wakati zikikua na kuongezeka, zingine zilizaa mara thelathini zaidi, na zingine sitini, na zingine mia”. 9Na akasema, “Yeyote mwenye masikio ya kusikia, na asikie!” 10Yesu alipokuwa peke yake, wale waliokuwa karibu naye na wale kumi na wawili walimuuliza kuhusu mifano. 11Akasema kwao, “Kwenu mmepewa siri za ufalme wa Mungu. Lakini kwa walio nje kila kitu ni mifano, 12ili wakitazama, ndiyo hutazama, lakini hawaoni, na kwa hiyo wanaposikia ndiyo husikia, lakini hawaelewi, amasivyo wangegeuka na Mungu angeliwasamehe.” 13Na akasema kwao, “Je hamuelewi mfano huu? Mtawezaje kuelewa mifano mingine?. 14Mpanzi alipanda neno. 15Baadhi ni wale walioanguka pembeni mwa njia, mahali neno lilipopandwa. Na walipolisikia, mara Shetani akaja na kulichukua neno ambalo lilipandwa ndani yao. 16Na baadhi ni wale waliopandwa juu ya mwamba, ambao, wanapolisikia neno, kwa haraka wanalipokea kwa furaha. 17Na hawana mizizi yoyote ndani yao, lakini huvumilia kwa muda mfupi. Halafu tabu na masumbufu vinapokuja kwa sababu ya neno, mara hujikwaa. 18Na wengine ni wale waliopandwa katika miiba. Wanalisikia neno, 19lakini masumbufu ya dunia, udanganyifu wa mali, na tamaa za mambo mengine, huwaingia na kulisonga neno, na linashindwa kuzaa matunda. 20Kisha kuna wale ambao wamepandwa kwenye udongo mzuri. Wanalisikia neno na kulipokea na huzaa matunda: baadhi thelathini, na baadhi sitini, na baadhi mia moja.”

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 27 Januari

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki