Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Januari 2027 › 27 Januari
Kalenda ya Kiorthodoksi · 14 Januari (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 27 Januari 2027
Jumatano · Wiki ya 35 baada ya Pentekoste · Sauti ya 1
Sikukuu na watakatifu
Kufungwa kwa Sikukuu ya Epifania
Siku ya mfungo
Samaki wanaruhusiwa
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Waraka
1Kwa vile sheria ni kivuli cha mambo mema yajayo, si yale yaliyo halisi. Sheria kamwe haiwezi kuwakamilisha wale ambao wanaomkaribia Mungu kwa njia ya dhabihu zilezile ambazo makuhani waliendelea kutoa mwaka baada ya mwaka. 2Au vinginevyo dhabihu hizo zisingeweza kukoma kutolewa? Kwa kigezo hicho waabuduo, wakiwa wamesafishwa mara moja, wasingelikuwa na utambuzi zaidi wa dhambi. 3Bali katika dhabihu hizo kuna ukumbusho wa dhambi zilizotendwa mwaka baada ya mwaka. 4Kwa kuwa haiwezekani kwa damu ya mafahari na mbuzi kuziondoa dhambi. 5Wakati Kristo alipokuja duniani, alisema, “Hamkutamani matoleo au dhabihu, badala yake, mliandaa mwili kwa ajili yangu. 6Hamkuwa na thamani katika matoleo yote ya kuteketezwa au dhabihu kwa ajili ya dhambi. 7Kisha nilisema, “Ona, hapa ninayafanya mapenzi yako, Mungu, kama ilivyoandikwa kunihusu mimi katika gombo”. 8Alisema kama ilivyo semwa hapo juu: “Hamkutamani dhabihu, matoleo, au sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya dhambi, wala hukuona furaha ndani yake” dhabihu ambazo zinatolewa kulingana na sheria. 9Kisha alisema, “Ona, niko hapa kufanya mapenzi yako”. Ameweka pembeni taratibu zilizo za awali ili kuimarisha zile za pili. 10Katika taratibu za pili, tumekwisha tengwa kwa Mungu kwa mapenzi yake kupitia kujitoa kwa mwili wa Yesu Kristo mara moja kwa nyakati zote. 11Ni kweli, kila kuhani husimama kwa huduma siku kwa siku, akitoa dhabihu ile ile, ambayo, kwa vyovyote, kamwe isingeweza kuziondoa dhambi. 12Lakini baada ya Kristo kutoa dhabihu mara moja kwa dhambi milele yote, aliketi mkono wa kuume wa Mungu, 13akisubiri mpaka maadui zake watiwe chini na kufanywa kiti kwa ajili ya miguu yake. 14Kwa kuwa kwa njia ya toleo moja amewakamilisha milele wale ambao wametengwa kwa Mungu. 15Na Roho Mtakatifu pia ashuhudia kwetu. Kwa kuwa kwanza alisema, 16“Hili ni agano nitakalofanya pamoja nao baada ya siku hizo; asema Bwana: nitaweka sheria zangu ndani ya mioyo yao, na nitaziandika katika akili zao”. 17Kisha alisema, “Hawatazikumbuka tena dhambi na matendo yao mafu”. 18Sasa mahali palipo na msamaha kwa hawa, hakuna tena dhabihu yoyote kwa ajili ya dhambi.
Injili
30Yesu akawaonya wasimwabie mtu yeyote kumuhusu Yeye. 31Na akaanza kuwafundisha ya kuwa Mwana wa Adamu lazima ateseke kwa mambo mengi, na atakataliwa na viongozi na makuhani wakuu, na waandishi, na atauawa, na baada ya siku tatu atafufuka. 32Alisema haya kwa uwazi. Ndipo Petro akamchukua pembeni na akaanza kumkemea. 33Lakini Yesu aligeuka na kuwatazama wanafunzi wake na akamkemea Petro na kusema, “Pita nyuma yangu Shetani! Hujali mambo ya Mungu, isipokuwa mambo ya watu.” 34Kisha akauita umati na wanafunzi wake pamoja, na kuwaambia, “Kama kuna mtu anataka kunifuata, ajikane mwenyewe, achukue msalaba wake, na anifuate.
Watakatifu wa siku
- Watakatifu Watawa Mababa waliouawa Sinai na Raithu: Isaya, Sava, Musa na mwanafunzi wake Musa, Yeremia, Paulo, Adamu, Sergio, Domno, Proklo, Hipatio, Isaka, Makario, Marko, Benyamini, Eusebio, Eliya na wengine pamoja nao (karne ya 4-5) [ibada yao huimbwa tarehe 13]
- Nina Sawa na Mitume, mwangazaji wa Georgia (335)
- Mtakatifu Mtawa Yusufu Analitino wa Raithu (karne ya 4)
- Mtakatifu Mtawa Theodulo wa Sinai (karne ya 5)
- Mtakatifu Mtawa Stefano, mwanzilishi wa monasteri ya Khenolakko (karne ya 8)
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 14 Januari katika kalenda ya kanisa ni 27 Januari katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki