Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Januari 2027 › 28 Januari
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 28 Januari 2027
Alhamisi · Juma la 3 la Mwaka
Sikukuu na watakatifu
Alhamisi ya Juma la 3 la Mwaka
Kumbukumbu · Rangi ya liturujia: nyeupe
Mt. Thoma wa Akwino, padre na mwalimu wa Kanisa · Kumbukumbu
Masomo ya siku
Somo la kwanza
19Kwa hiyo, ndugu, tunao ujasiri wa kuingia mahali patakatifu zaidi kwa damu ya Yesu. 20Hiyo ni njia ambayo ameifungua kwa ajili yetu kwa njia ya mwili wake, mpya na hai inayopitia kwenye pazia. 21Na kwa sababu tunaye kuhani mkuu juu ya nyumba ya Mungu, 22na tumkaribie na moyo wa kweli katika utimilifu wa uhakika wa imani tukiwa na mioyo iliyonyunyiziwa safi kutoka uovu wa dhamiri na kuwa na miili yetu iliyooshwa kwa maji safi. 23Basi na tushikilie kwa uthabiti katika ungamo la ujasiri wa tumaini letu, bila ya kugeuka, kwa sababu Mungu aliyeahidi ni mwaminifu. 24Na tuzidi kutafakari namna ya kumtia moyo kila mmoja kupenda na matendo mema. 25Na tusiache kukusanyika pamoja, kama wafanyavyo wengine. Badala yake, kutiana moyo kila mmoja zaidi na zaidi, kama muonavyo siku inakaribia.
Wimbo wa katikati
1Zaburi ya Daudi. Nchi ni ya Yahwe, na vyote viijazavyo, dunia, na wote wakaao ndani yake. 2Kwa kuwa yeye aliianzisha juu ya bahari na kuiimarisha juu ya mito. 3Ni nani atakaye panda mlima wa Yahwe? Ni nani atakaye simama patakatifu pake? 4Yeye ambaye ana mikono misafi na moyo safi; ambaye hajauinua uongo, na haja apa kiapo ili kudanganya. 5Yeye atapokea baraka kutoka kwa Yahwe na haki kutoka kwa Mungu wa wokovu wake. 6Kizazi cha wale wamtafutao Mungu ni kama hiki, wale ambao wanautafuta uso wa Mungu wa Yakobo.
Injili
21Yesu akawaambia, “ Je huwa unaleta taa ndani ya nyumba na kuiweka chini ya kikapu, au chini ya kitanda? Huileta ndani na kuiweka juu ya kiango. 22Kwa kuwa hakuna chochote kilichojificha ambacho hakitajulikana, na hakuna siri ambayo haitawekwa wazi. 23Akiwapo mwenye masikio ya kusikia, na asikie!” 24Akawaambia, “ Iweni makini kwa kile mnachokisikia, kwa kuwa kipimo mpimacho, ndicho mtakachopimiwa, na itaongezwa kwenu. 25Kwa sababu yeye aliyenacho, atapokea zaidi, na yule asiyenacho, kutoka kwake vitachukuliwa hata vile alivyonavyo.”
Watakatifu wa siku
- Mt. Thoma wa Akwino, padre na mwalimu wa Kanisa
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki