Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Januari 2027 › 26 Januari

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 26 Januari 2027

Jumanne · Juma la 3 la Mwaka

Sikukuu na watakatifu

Jumanne ya Juma la 3 la Mwaka

Kumbukumbu · Rangi ya liturujia: nyeupe

Watakatifu Timotheo na Tito, maaskofu · Kumbukumbu

Masomo ya siku

Somo la kwanza

2 Tim 1:1–8

au: Tit 1:1–5

1Paulo mtume wa Yesu Kristo kwa mapenzi ya Mungu, sawasawa na ahadi ya uzima ulio ndani ya Kristo Yesu, 2kwa Timotheo mwana mpendwa: Neema, rehema na amani toka kwa Mungu Baba na Kristo Yesu Bwana wetu. 3Ninamshukuru Mungu, ambaye ninamtumikia kwa nia njema kama walivyofanya baba zangu, ninapokumbuka daima katika maombi yangu. Usiku na 4mchana ninatamani kukuona, ili kwamba nijawe na furaha. Ninayakumbuka machozi yako. 5Nimekuwa nikikumbushwa kuhusu imani yako halisi, ambayo hapo kwanza ilikaa kwa bibi yako Loisi na mama yako Yunisi. Na nina hakika ya kwamba imani hiyo inakaa ndani yako pia. 6Hii ndiyo sababu nakukumbusha kuchochea karama ya Mungu iliyomo ndani yako kwa njia ya kuwekewa mikono yangu. 7Kwa kuwa Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na upendo na nidhamu. 8Kwa hiyo usiuonee haya ushuhuda kuhusu Bwana wetu, wala wangu mimi Paulo mfungwa wake. Bali ushiriki mateso kwa ajili ya injili sawasawa na uweza wa Mungu.

Wimbo wa katikati

Zab 40:1, 3, 6–7, 9–10

1Kwa kiongozi wa muziki. Zaburi ya Daudi. Nalimungoja Yahwe kwa uvumilivu; alinisikia na kusika kilio changu. 3Yeye ameweka wimbo mpya mdomoni mwangu, sifa kwa Mungu. Wengi watauona na kumheshimu yeye na kumwamini Yahwe. 6Wewe haufurahishwi katika sadaka au matoleo, bali wewe umeyafungua masikio yangu; wala haukuhitaji sadaka ya kuteketeza au sadaka ya dhambi. 7Ndipo nilisema mimi, “Tazama, nimekuja; imeandikwa kuhusu mimi katika kitabu cha hati. 9Katika kusanyiko kubwa nimetangaza habari njema ya haki yako; Yahwe, wewe unajua sikuizuia midomo yangu. 10Sikuficha haki yako moyoni mwangu; nimetangaza uaminifu wako na wokovu wako; sijaficha uaminifu wa agano lako au uaminifu wako kwenye kusanyiko kubwa.

Injili

Mk 3:31–35

31Kisha mama yake na ndugu zake walikuja na kusimama nje. Wakamtuma mtu, kumwita. 32Na umati wa watu uliokuwa umekaa karibu naye wakamwambia, “mama yako na ndugu zako wako nje, na wanakutafuta wewe”. 33Aliwajibu, “Ni nani mama yangu na ndugu zangu?” 34Aliwaangalia waliokuwa wamekaa wamemzunguka, na akasema, “Tazama, hawa ni mama zangu na ndugu zangu! 35Yeyote afanyaye mapenzi ya Mungu, mtu huyo ni ndugu yangu, na dada yangu, na mama yangu”.

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 26 Januari

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki