Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Januari 2027 › 23 Januari
Kalenda ya Kiorthodoksi · 10 Januari (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 23 Januari 2027
Jumamosi · Wiki ya 34 baada ya Pentekoste · Sauti ya 8
Sikukuu na watakatifu
Jumamosi baada ya Theofania
Mfungo
Hakuna mfungo
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Waraka (Jumamosi baada ya Theofania)
10Hatimaye, iweni na nguvu katika Bwana na katika uwezo wa nguvu zake. 11Vaeni silaha zote za Mungu, ili kwamba mpate kusimama kinyume na hila za shetani. 12kwa kuwa vita yetu si ya damu na nyama, bali ni dhidi ya falme na mamlaka ya roho na watawala wa ulimwengu wa uovu na giza, dhidi ya pepo katika sehemu za mbingu. 13Kwa hiyo, vaeni silaha zote za Mungu, ili mpate kusimama imara dhidi ya uovu katika kipindi hiki kiovu. Baada ya kumaliza kila kitu, mtasimama imara. 14Hatimaye simameni imara. Fanyeni hivi baada ya kuwa mmefunga mkanda katika kweli na haki kifuani. 15Fanyini hivi mkiwa mmevaa utayari miguuni mwenu wa kutangaza injili ya amani. 16Katika kila hali mkichukua ngao ya imani, ambayo itakuwezesha kuizima mishale ya yule mwovu. 17Vaeni kofia ya wokovu na upanga wa Roho, ambayo ni neno la Mungu.
Waraka
11Kwa hiyo kumbukeni kwamba hapo zamani mlikuwa watu wa Mataifa kwa jinsi ya mwili. Mnaitwa “msio na tohara” kwa kile kinachoitwa tohara ya mwili inayofanywa kwa mikono ya binadamu. 12Kwa wakati huo mlikuwa mmetengwa na Kristo. Mlikuwa wageni kwa watu wa Israel. Mlikuwa wageni kwa agano la ahadi. Hamkuwa na uhakika wa wakati ujao. Mlikuwa bila Mungu katika ulimwengiu. 13Lakini sasa katika Kristo Yesu ninyi ambao hapo mwanzo mlikuwa mbali na Mungu mmeletwa karibu na Mungu kwa damu ya Kristo.
Injili (Jumamosi baada ya Theofania)
1Kisha Yesu aliongozwa na Roho mpaka jangwani ili ajaribiwe na ibilisi. 2Alipokuwa amefunga kwa siku arobaini mchana na usiku alipata njaa. 3Mjarabu akaja na akamwambia, “Kama wewe ni Mwana wa Mungu, amuru mawe haya yawe mkate.” 4Lakini Yesu alimjibu na kumwambia, “Imeandikwa, 'Mtu hataishi kwa mkate peke yake, bali kwa kila neno litokalo kinywani mwa Mungu.''' 5Kisha ibilisi akampeleka katika mji mtakatifu na kumweka mahali pa juu sana pa jengo la hekalu, 6na kumwambia,'' kama wewe ni Mwana wa Mungu, jirushe chini, kwa maana imeandikwa, 'Ataamuru malaika wake waje wakudake,' na, 'watakuinua kwa mikono yao, ili usijikwae mguu wako katika jiwe.” 7Yesu akamwambia, ''Tena imeandikwa, 'Usimjaribu Bwana Mungu wako.''' 8Kisha, ibilisi akamchukua na kumpeleka sehemu ya juu zaidi akamwonyesha falme zote za ulimwengu na fahari ya hizo zote. 9Akamwambia, “Nitakupa vitu vyote hivi ukunisujudia na kuniabudu.” 10Kisha Yesu akamwambia, “Nenda zako utoke hapa, Shetani! Kwa maana imeandikwa, 'Yakupasa kumwabudu Bwana Mungu wako, na umtumikie yeye peke yake.'” 11Kisha ibilisi akamwacha, na tazama, malaika wakaja wakamtumikia.
Injili
18Yesu akasema, “Ufalme wa Mungu unafanana na nini, na naweza kuulinganisha na nini? 19Ni kama mbegu ya haradari aliyoitwaa mtu mmoja na kuipanda shambani mwake, na ikamea ikawa mti mkubwa, na ndege wa mbinguni wakajenga viota vyao katika matawi yake. 20Tena akasema, “Niufananishe na nini ufalme wa Mungu? 21Ni kama chachu ambayo mwanamke aliichukua na kuchanganyakwenye vipimo vitatu vya unga hata ukaumuka.” 22Yesu alitembelea kila mji na kijiji njiani akielekea Yerusalemu na kuwafundisha. 23Mtu mmoja akauliza, “Bwana, ni watu wachache tu watakaookolewa?” Hivyo akawaambia, 24“Jitahidi kuingia kwa kupitia mlango mwembamba, kwa sababu wengi watajaribu na hawataweza kuingia. 25Mara baada ya mmiliki wa nyumba kusimama na kufunga mlango, basi mtasimama nje na kupiga hodi mlangoni na kusema, Bwana, Bwana, tufungulie yeye atajibu na kuwaambia, siwajui ninyi wala mtokako.' 26Ndipo mtasema, Tulikula na kunywa mbele yako na wewe ulifundisha katika mitaa yetu.” 27Lakini yeye atawajibu, 'nawaambia, siwajui mtokako, ondokeni kwangu, ninyi watenda maovu!' 28Kutakuwa na kilio na kusaga meno wakati mtakapowaona Abrahamu, Isaka, Yakobo na manabii wote katika ufalme wa Mungu, lakini ninyi wenyewe mumetupwa nje. 29Watafika kutoka Mashariki, Magharibi, Kaskazini na Kusini, na kupumzika katika meza ya chakula cha jioni katika ufalme wa Mungu.
Watakatifu wa siku
- Baada ya Sikukuu ya Epifania
- Askofu Mtakatifu Gregori, Askofu wa Nisa (395)
- Mtakatifu Mtawa Dometiani, Askofu wa Melitene (601)
- Mtakatifu Mtawa Markiano, padri (karne ya 5)
- Mtakatifu Mtawa Paulo wa Komel (wa Obnora) (1429)
- Askofu Mtakatifu Theofani, mtawa wa faragha wa Vysha (1894)
- Mtakatifu Mtawa Antipa wa Varlaam (wa Athos) (1882)
- Mfiadini wa Kikasisi Zinovi, padri (1920)
- Mfiadini wa Kikasisi Petro, padri (1930)
- Mfiadini wa Kikasisi Anatoli, Mitropoliti wa Odesa (1938)
- Mtawa Mfiadini Arsenia, abesi (1939)
- Mbarikiwa Theosebia, shemasi mwanamke, dada wa Askofu Mtakatifu Gregori wa Nisa (385)
- Mtakatifu Mtawa Makario wa Pisma (karne ya 14)
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 10 Januari katika kalenda ya kanisa ni 23 Januari katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki