Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Januari 2027 › 23 Januari

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 23 Januari 2027

Jumamosi · Juma la 2 la Mwaka

Sikukuu na watakatifu

Jumamosi ya Juma la 2 la Mwaka

Kumbukumbu ya hiari · Rangi ya liturujia: kijani

Kumbukumbu ya Bikira Maria siku ya Jumamosi · Kumbukumbu ya hiari

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Ebr 9:2–3, 11–14

2Kwani katika hema kulikuwa na chumba kimeandaliwa, chumba cha nje, paliitwa mahali patakatifu. Katika eneo hili palikuwa na kinara cha taa, meza na mikate ya wonyesho. 3Na nyuma ya pazia la pili kulikuwa na chumba kingine, paliitwa mahali patakatifu zaidi. 11Kristo alikuja kama kuhani mkuu wa mambo mazuri ambayo yamekuja. kupitia ukuu na ukamilifu wa hema kuu ambayo haikufanywa na mikono ya watu, ambayo si wa ulimwengu huu ulioumbwa. 12Ilikuwa si kwa damu ya mbuzi na ndama, bali kwa damu yake mwenyewe kwamba Kristo aliingia mahali patakatifu zaidi mara moja kwa kila mmoja na kutuhakikishia ukombozi wetu wa milele. 13Kama kwa damu ya mbuzi na mafahari na kunyunyiziwa kwa majivu ya ndama katika hao wasiosafi walitengwa kwa Mungu na kufanya miili yao safi, 14Je si zaidi sana damu ya Kristo ambaye kupitia Roho wa milele alijitoa mwenyewe bila mawaa kwa Mungu, kuosha dhamiri zetu kutoka matendo mafu kumtumikia Mungu aliye hai?

Wimbo wa katikati

Zab 47:1–2, 5–8

1Kwa kiongozi wa muziki. Zaburi ya wana wa Korah. Pigeni makofi, enyi watu wote; mpigieni Mungu kelele za ushindi. 2Kwa maana Yahwe Aliye Juu anatisha; ni Mfalme mkuu dunia yote. 5Mungu ameinuliwa juu kwa shangwe, Kwa mbiu ya shangwe Yahwe yu juu. 6Mwimbieni Mungu sifa, imbeni sifa; mwimbieni sifa Mfalme wetu, imbeni sifa. 7Kwa maana Mungu ni Mfalme duniani kote; mwimbieni mkiwa na uelewa. 8Mungu anatawala mataifa yote; Mungu hukaa kwenye kiti cha enzi.

Injili

Mk 3:20–21

20Kisha alienda nyumbani, na umati wa watu wakaja pamoja tena, hata wasiweze kula hata mkate. 21Familia yake waliposikia habari hiyo, walienda kumkamata, kwani walisema, “ Amerukwa na akili”.

Watakatifu wa 23 Januari

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki