Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Januari 2027 › 22 Januari
Kalenda ya Kiorthodoksi · 9 Januari (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 22 Januari 2027
Ijumaa · Wiki ya 34 baada ya Pentekoste · Sauti ya 8
Sikukuu na watakatifu
Baada ya Sikukuu ya Epifania
Siku ya mfungo
Samaki wanaruhusiwa
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Waraka
18Kwa kuwa amri iliyotangulia iliwekwa pembeni kwa sababu ilikuwa dhaifu na haifai. 19Hivyo sheria haikufanya chochote kikamilifu. Isipokuwa, kulikuwa na ujasiri mzuri kwa hayo tunamsogelea Mungu. 20Na Ujasiri huu mzuri haukutokea pasipo kuzungumzia kiapo, kwa hili makuhani wengine hawakuchukua kiapo chochote. 21Lakini Mungu alichukua kiapo wakati aliposema kuhusu Yesu, “Bwana ameapa na hatabadilisha mawazo yake.' wewe ni kuhani milele.” 22Kwa hili Yesu pia amekuja kuwa dhamana ya agano bora. 23Kwa hakika, kifo huzuia makuhani kuhudumu milele. Hii ni kwa sababu walikuwapo makuhani wengi, mmoja baada ya mwingine. 24Lakini kwa sababu Yesu anaishi milele, ukuhani wake haubadiliki. 25Kwa hiyo yeye pia anaweza kwa ukamilifu kukamilisha kuwaokoa wanaomkaribia Mungu kupitia kwake, kwa kuwa yeye anaishi daima kwa kuomba kwa ajili yao.
Injili
37Hivyo wakati wa mchana alikuwa akifundisha hekaluni na usiku alitoka nje, na kwenda kukesha katika mlima unaoitwa wa Mzeituni. 38Watu wote walimjia asubuhi na mapemaili kumsikiliza ndani ya hekalu. 22:1Basi Sikukuu ya Mkate Usiyotiwa Chachu ilikuwa imekaribia, ambayo inaitwa Pasaka. 2Makuhani wakuu na waandishi wakajadiliana namna ya kumuua Yesu, kwa sababu waliwaogopa watu. 3Shetani akaingia ndani ya Yuda Iskariote, mmoja wa wale wanafunzi Kumi na mbili. 4Yuda akaenda kujadiliana na wakuu wa makuhani na wakuu namna ambavyo atamkabidhi Yesu kwao. 5Walifurahi, na kukubaliana kumpa fedha. 6Yeye aliridhia, na alitafuta fursa ya kumkabidhi Yesu kwao mbali na kundi la watu. 7Siku ya mikate isiyotiwa chachu ikafika, ambapo kondoo wa Pasaka lazima atolewe. 8Yesu akawatuma Petro na Yohana, akasema, “Nendeni mkatuandalie chakula cha Pasaka ili tuje tukile.”
Watakatifu wa siku
- Mfiadini Polieukto (259)
- Askofu Mtakatifu Filipo, Mitropoliti wa Moscow na Urusi yote, mtenda miujiza (1569)
- Mfiadini wa Kikasisi Paulo, padri
- Nabii Shemaya (karne ya 10 K.K.)
- Askofu Mtakatifu Petro, Askofu wa Sebastia ya Armenia, ndugu wa Askofu Mtakatifu Basili Mkuu (karne ya 4)
- Mtakatifu Mtawa Eustratio, mtenda miujiza (karne ya 9)
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 9 Januari katika kalenda ya kanisa ni 22 Januari katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki