Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Novemba 2026 › 22 Novemba
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 22 Novemba 2026
Jumapili · Juma la 34 la Mwaka
Sikukuu na watakatifu
Bwana Wetu Yesu Kristo, Mfalme wa Ulimwengu
Sherehe · Rangi ya liturujia: nyeupe
Masomo ya siku
Somo la kwanza
11Kwa kuwa Bwana Yahwe asema hivi: Tazama! mimi mwenyewe nitawatafuta kondoo wangu na kuwaulizia, 12kama mchungaji atafutaye kundi lake juu ya siku hiyo yupo ndani ya kundi lake lililotawanyika. Hivyo nitalitafuta kundi langu, na nitalichunga kutoka sehemu lilipokuwa limetawanyika siku ya mawingu na giza. 15Mimi mwenyewe nitachunga kondoo wangu, na mimi mwenyewe nitawalaza chini-hivi ndivyo Bwana Yahwe 16asemavyo-Nitawatafuta waliopotea nitawarudisha waliofukuzwa. Nitawafunga waliovunjika na kuwaponya kondoo waliougua lakini wanene na wenye nguvu nitawaharibu. Nitawalisha kwa haki. 17Hivyo sasa ninyi, kundi langu-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-tazama, nitakuwa hakimu kati ya kondoo na kondoo na kati ya kondoo dume na mbuzi dume.
Wimbo wa katikati
1Zaburi ya Daudi. Yahwe ni mchungaji wangu; sita pungukiwa na kitu. 2Yeye hunilaza katika majani mabichi; huniongoza kando ya maji matulivu. 3Yeye huurejesha uhai wangu; huniongoza katika njia iliyo sahihi kwa ajili ya jina lake. 5Wewe waandaa meza mbele yangu katika uwepo wa maadui zangu; umenipaka mafuta kichwa changu na kikombe changu kinafurika. 6Hakika wema na uaminifu wa agano vitaniandama siku zote za maisha yangu; nami nitaishi katika nyumba ya Yahwe milele!
Somo la pili
20Lakini sasa Kristo amefufuka kutoka kwa wafu, matunda ya kwanza ya wale waliokufa. 21Kwa kuwa kifo kilikuja kupitia mwanadamu, pia kupitia mwanadamu ufufuo wa wafu. 22Kwa kuwa kama katika Adam wote wanakufa, hivyo pia katika Kristo wote watafanywa hai. 23Lakini kila moja katika mpango wake: Kristo, matunda ya kwanza, na kisha wale walio wa Kristo watafanywa hai wakati wa kuja kwake. 24Ndipo utakuwa mwisho, pale Kristo atakapo kabidhi ufalme kwa Mungu Baba. Hii ni pale atakapo komesha utawala wote na mamlaka yote na nguvu. 25Kwa kuwa lazima atawale mpaka atakapoweka maadui zake wote chini ya nyayo zake. 26Adui wa mwisho kuharibiwa ni kifo. 28Wakati vitu vyote vimewekwa chini yake, kisha Mwana mwenyewe atawekwa chini kwake Yeye ambaye aliviweka vitu vyote chini yake. Hii itatokea ili kwamba Mungu Baba awe yote katika vyote.
Injili
31Wakati Mwana wa Adamu atakapokuja katika utukufu wake, na malaika wote pamoja naye, ndipo atakapokaa juu ya kiti chake cha utukufu. 32Mataifa yote yatakusanyika mbele zake, naye atawatenganisha watu, kama vile mchungaji anavyowatenganisha kondoo na mbuzi. 33Atawaweka kondoo mkono wake wa kuume, bali mbuzi atawaweka mkono wa kushoto. 34Kisha mfalme atawaambia wale walio mkono wake wa kulia, 'Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme ulioandaliwa kwa ajili yenu tangu kuwekwa msingi wa ulimwengu. 35Kwa kuwa nilikuwa na njaa na mlinipa chakula; Nilikuwa mgeni na mlinikaribisha; 36Nilikuwa uchi, na mlinivika nguo; Nilikuwa mgonjwa na mkanitunza; Nilikuwa kifungoni na mkaniijia.' 37Ndipo wenye haki watamjibu na kumwambia, 'Bwana, lini tulikuona ukiwa na njaa, na kukulisha? Au una kiu na tukakupa maji? 38Na lini tulikuona ukiwa mgeni, na tukakukaribisha? Au ukiwa uchi na tukakuvisha nguo? 39Na lini tulikuona ukiwa mgonjwa, au katika kifungo, na tukakujia? 40Na mfalme atawajibu na kuwaambia, 'Kweli nawaambia, mlichotenda hapa kwa mmoja wa ndugu zangu wadogo, mlinitendea mimi.' 41Ndipo atawaambia hao walio mkono wake wa kushoto, 'Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, nendeni katika moto wa milele ulioandaliwa kwa ajili ya shetani na malaika zake, 42kwa sababu nilikuwa na njaa lakini hamkunipa chakula; Nilikuwa na kiu lakini hamkunipa maji; 43Nilikuwa mgeni lakini hamkunikaribisha; nikiwa uchi lakini hamkunipa mavazi; nikiwa mgonjwa na nikiwa kifungoni, lakini hamkunitunza.' 44Ndipo wao pia watamjibu na kusema, 'Bwana, lini tulikuona ukiwa na njaa, au una kiu, au u mgeni, au ukiwa uchi, au ukiwa mgonjwa, au ukiwa mfungwa, na hatukukuhudumia? 45Kisha atawajibu na kusema, 'Kweli nawaambia, kile ambacho hamkutenda kwa mmoja wa hawa wadogo, hamkunitendea mimi.' 46Hawa watakwenda katika adhabu ya milele bali wenye haki katika uzima wa milele.”
Watakatifu wa siku
- Mt. Sesilia, bikira na shahidi
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili A, mwaka wa siku za kazi II.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki