Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Novemba 2026 › 23 Novemba
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 23 Novemba 2026
Jumatatu · Juma la 34 la Mwaka
Sikukuu na watakatifu
Jumatatu ya Juma la 34 la Mwaka
Kumbukumbu ya hiari · Rangi ya liturujia: kijani
Mt. Klementi I, papa na shahidi · Kumbukumbu ya hiari
Mt. Kolumbani, abati · Kumbukumbu ya hiari
Masomo ya siku
Somo la kwanza
1Nilitazama na nikaona Mwana Kondoo amesimama mbele yangu juu ya Mlima Sayuni. Pamoja naye walikuwa 144,000 wenye jina lake na jina la Baba yake limeandikwa katika vipaji vya nyuso zao. 2Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisikika kama ngurumo za maji mengi na sauti kubwa ya radi. Sauti niliyoisikia ni kama wapiga vinubi wapigao vinubi vyao. 3Wakiimba wimbo mpya mbele za kiti cha enzi na mbele za wenye uhai wanne na wazee. Hakuna hata mwenye uwezo wa kujifunza huo wimbo isipokuwa kwa 144,000 ambao wamekombolewa kutoka duniani. 4Hawa ni wale ambao hawakujichafua wenyewe kwa wanawake, maana walijitunza wenyewe dhidi ya matendo ya zinaa. Ni hawa ambao walimfuata Mwana Kondoo popote alipoenda. Hawa walikombolewa kutoka kwa wanadamu wakiwa matunda ya kwanza kwa Mungu na kwa Mwana Kondoo. 5Hakuna uongo uliopatikana katika vinywa vyao; hawalaumiwi.
Wimbo wa katikati
1Zaburi ya Daudi. Nchi ni ya Yahwe, na vyote viijazavyo, dunia, na wote wakaao ndani yake. 2Kwa kuwa yeye aliianzisha juu ya bahari na kuiimarisha juu ya mito. 3Ni nani atakaye panda mlima wa Yahwe? Ni nani atakaye simama patakatifu pake? 4Yeye ambaye ana mikono misafi na moyo safi; ambaye hajauinua uongo, na haja apa kiapo ili kudanganya. 5Yeye atapokea baraka kutoka kwa Yahwe na haki kutoka kwa Mungu wa wokovu wake. 6Kizazi cha wale wamtafutao Mungu ni kama hiki, wale ambao wanautafuta uso wa Mungu wa Yakobo.
Injili
1Yesu alitazama akawaona wanaume matajiri waliokuwa wanaweka zawadi zao kwenye hazina. 2Akamuona mjane mmoja masikini akiweka senti zake mbili. 3Hivyo akasema, “Kweli nawaambieni, huyu Mjane maskini ameweka nyingi kuliko wengine wote. 4Hawa wote wametoa hizi zawadi kutoka katika vingi walivyonavyo. Lakini huyu mjane, katika umaskini wake, ametoa fedha zote alizokuwa nazo kwa ajili ya kuishi kwake.”
Watakatifu wa siku
- Mt. Klementi I, papa na shahidi
- Mt. Kolumbani, abati
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili A, mwaka wa siku za kazi II.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki