Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Novemba 2026 › 21 Novemba

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 21 Novemba 2026

Jumamosi · Juma la 33 la Mwaka

Sikukuu na watakatifu

Jumamosi ya Juma la 33 la Mwaka

Kumbukumbu · Rangi ya liturujia: nyeupe

Kutolewa kwa Bikira Maria Hekaluni · Kumbukumbu

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Ufu 11:4–12

4Hawa mashahidi ni miti miwili ya mizeituni na vinara viwili ambavyo vimesimama mbele ya Bwana wa dunia. 5Kama mtu yeyote ataamua kuwadhuru, moto hutoka vinywani mwao na kuwadhuru adui zao. Yeyote anayetaka kuwadhuru lazima auawe kwa njia hii. 6Hawa mashahidi wana uwezo wa kufunga anga ili kwamba mvua isinyeshe wakati wanatabiri. Wana nguvu ya kubadili maji kuwa damu na kuipiga nchi kwa kila aina ya pigo wakati wowote wakitaka. 7Wakati watakapokuwa wamemaliza ushuhuda wao, yule mnyama anayetoka kwenye shimo lisilo na mwisho atafanya vita dhidi yao. Atawashinda na kuwaua. 8Miili yao italala katika mtaa wa mji mkuu (ambao kimfano unaitwa Sodoma na Misri) ambapo Bwana wao alisulubiwa. 9Kwa siku tatu na nusu baadhi kutoka katika jamaa za watu, kabila, lugha na kila taifa watatazama miili yao na hawatatoa kibali kuwekwa katika kaburi. 10Wale wanaoishi katika nchi watafurahi kwa ajili yao na kushangilia, hata kutumiana zawadi kwa sababu hao manabii wawili waliwatesa wale walioishi katika nchi. 11Lakini baada ya siku tatu na nusu pumzi ya uhai kutoka kwa Mungu itawaingia nao watasimama kwa miguu yao. Hofu kuu itawaangukia wale wanaowaona. 12Kisha watasikia sauti kuu kutoka mbinguni ikiwaambia, “Njoni huku!” Nao watakwenda juu mbinguni katika wingu, wakati adui zao wakitazama.

Wimbo wa katikati

Zab 144:1–2, 9–10

1Zaburi ya Daudi. Atukuzwe Yahwe, mwamba wangu, anifundishaye mikono yangu vita na vidole vyangu kupigana. 2Wewe ni uaminifu wa agano langu na ngome yangu, mnara wangu mrefu na uniokoaye, ngao yangu na yule ambaye katika yeye napata kimbilio, uyatiishaye mataifa chini yangu. 9Nitakuimbia wimbo mpya, Mungu; kwa kinanda cha nyuzi kumi nitakuimbia sifa wewe, 10uwapaye wafalme wokovu, uliye muokoa Daudi mtumishi wako dhidi ya upanga wa uovu.

Injili

Lk 20:27–40

27Baadhi ya Masadukayo wakamwendea, wale ambao wanasema kwamba hakuna ufufuo, 28wakamwuliza, wakisema, “Mwalimu, Musa alituandikia kwamba kama mtu akifiwa na ndugu mwenye mke ambaye hana mtoto basi anapaswa kumchukuna mke wa ndugu yake na kuzaa nae kwa ajili ya kaka yake. 29Kulikuwa na ndugu saba Wa kwanza alioa, akafa bila kuacha mtoto, 30na wa pili pia. 31Wa tatu akamchukua vilevile, vivyo hivyo wa saba hakuacha watoto na akafa. 32Baadaye yule mwanamke pia akafa. 33Katika ufufuo atakuwa mke wa nani? Maana wote saba walikuwa wamemwoa. ' 34Yesu akawaambia, “Wana wa ulimwengu huu huoa na kuolewa. 35Lakini wale wanastaohili kupokea ufufuo wa wafu na kuingia uzima wa milele hawaoi wala hawaolewi. 36Wala hawawezi kufa tena, kwa sababu huwa sawasawa na malaika na ni watoto wa Mungu, wana wa ufufuo. 37Lakini hiyo wafu wanafufuliwa, hata Musa alionyesha mahali katika habari za kichaka, pale alimwita Bwana kama Mungu wa Ibrahimu na Mungu wa Isaka na Mungu wa Yakobo. 38Sasa, yeye si Mungu wa wafu, bali wa walio hai, kwa sababu wote huishi kwake. “ 39Baadhi ya walimu wa Sheria wakamjibu, 'Mwalimu, umejibu vema. ' 40Hawakuthubutu kumwuliza maswali mengine zaidi.

Watakatifu wa 21 Novemba

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili A, mwaka wa siku za kazi II.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki