Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Oktoba 2026 › 18 Oktoba
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 18 Oktoba 2026
Jumapili · Juma la 29 la Mwaka
Sikukuu na watakatifu
Dominika ya 29 ya Mwaka
Dominika · Rangi ya liturujia: kijani
Masomo ya siku
Somo la kwanza
1Yahwe asema hivi kwa mapakwa mafuta, kwa Koreshi, niliyemshika kwa mkono wa kuume, illi niweze kuangamiza mataifa mbele yake, kuwalinda wafalme, kufunguo milango mbele yao, ili lango liwe wazi: 4Kwa niaba ya Jakobo mtumishi wangu, na Israeli chaguo langu, Nimekuita wewe kwa jina lako: nimekupa heshima iliyotukuka, jabo hakunijua mimi. 5Mimi ni Yahwe na hapana mwingine; hakuna Mungu ila mimi. Nitakuimarisha katika vita, japo hamkunifamu mimi; 6kwamba watu wajue kutoka mapambazuko ya jua, na kutoka magharibi, kwamba hakuna mungu mwngine ila mimi: Mimi ni Yahwe, na hakuna mwingine.
Wimbo wa katikati
1Oh, mwimbieni Yahwe wimbo mpya; mwimbieni Yahwe, nchi yote. 3Tangazeni utukufu wake kati ya mataifa, matendo yake ya ajabu kati ya mataifa. 4Maana Yahwe ni mkuu na wakusifiwa sana. Ni wakuhofiwa kuliko miungu mingine. 5Maana miungu yote ya mataifa ni sanamu, bali ni Yahwe aliye zifanya mbingu. 7Mpeni Yahwe sifa, enyi ukoo wa watu, mpeni sifa Yahwe kwa ajili ya utukufu wake na nguvu. 8Mpeni Yahwe utukufu ambao unastahili jina lake. Leteni matoleo na muingie nyuani mwake. 9Mpigieni magoti Yahwe mkiwa mmevaa mavazi ambayo yanaheshimu utakatifu wake. Nchi yote tetemekeni mbele zake. 10Semeni kati ya mataifa, Yahwe anatawala.” Ulimwengu pia umeimarishwa; hauwezi kutikiswa. Yeye huwahukumu watu kwa haki.
Somo la pili
1Paulo, Silwano na Timotheo kwa kanisa la Wathesalonike katika Mungu Baba na Bwana Yesu Kristo. Neema na amani iwe nanyi. 2Tunatoa shukrani kwa Mungu kila mara kwa ajili yenu nyote, wakati tunapowataja katika maombi yetu. 3Tunaikumbuka bila kukoma mbele ya Mungu na baba yetu kazi yenu ya imani, juhudi ya upendo, na uvumilivu wenye ujasiri kwa ajili ya baadaye katika Bwana Yesu Kristo. 4Ndugu Mnaopendwa na Mungu, tunajua wito wenu. 5Na jinsi injili yetu ilivyokuja kwenu si kwa neno tu, bali pia katika nguvu, katika Roho Mtakatifu, na katika uhakika. Kwa namna hiyo, mnajua pia sisi tulikuwa watu wa namna gani miongoni mwenu kwa ajili yenu.
Injili
15Ndipo Mafarisayo waliondoka na kupanga jinsi ya kumkamata Yesu katika maneno yake mwenyewe. 16Ndipo walipowatuma wanafunzi wao pamoja na Maherode. Na walimwambia Yesu, “Mwalimu, tunajua kuwa wewe ni mtu wa kweli, na kwamba unafundisha matakwa ya Mungu katika ukweli. Haujali maoni ya mtu mwingine na hauoneshi upendeleo kwa watu. 17Kwa hiyo tuambie, unafikiri nini? Je, ni sahihi kisheria kulipa kodi kwa Kaisari au hapana?” 18Yesu alifahamu uovu wao na akasema, “Kwa nini mnanijaribu, enyi wanafiki? 19Nionesheni pesa itumikayo kulipia kodi.” Ndipo wakamletea dinari. 20Yesu akawauliza, “Sura na jina hili ni vya nani?” 21Wakamjibu, “Vya Kaisari.” Ndipo Yesu akawaambia, “Mpeni Kaisari vitu vilivyo vyake na vya Mungu mpeni Mungu.”
Watakatifu wa siku
- Mt. Luka, mwinjili
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili A, mwaka wa siku za kazi II.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki