Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Oktoba 2026 › 17 Oktoba
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 17 Oktoba 2026
Jumamosi · Juma la 28 la Mwaka
Sikukuu na watakatifu
Jumamosi ya Juma la 28 la Mwaka
Kumbukumbu · Rangi ya liturujia: nyekundu
Mt. Ignasi wa Antiokia, askofu na shahidi · Kumbukumbu
Masomo ya siku
Somo la kwanza
15Kwa sababu hii, tangu wakati niliposikia kuhusu imani yenu ndani ya Bwana Yesu na kuhusu pendo lenu kwa wale wote ambao wametengwa kwa ajili yake. 16Sijaacha kumshukuru Mungu kwa ajili yenu na kuwataja katika maombi yangu. 17Ninaomba kwamba Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, baba wa utukufu, atawapeni roho ya hekima, mafunuo ya ufahamu wake. 18Ninaomba kwamba macho yenu ya moyoni yatiwe nuru kwa ninyi kujua ni upi ujasiri wa kuitwa kwenu. Naomba kwamba mjue utajiri wa utukufu wa urithi wake miongoni mwa wale waliotengwa kwa ajili yake. 19Naomba kwamba ujue ukuu uzidio wa nguvu yake ndani yetu ambao tunaamini. Huu ukuu ni kutokana na kufanya kazi katika nguvu zake. 20Hii ni nguvu iliyofanya kazi ndani ya Kristo wakati Mungu alipomfufua kutoka kwa wafu na kumketisha katika mkono wake wa kuume katika mahali pa mbingu. 21Alimketisha Kristo juu mbali na utawala, mamlaka, nguvu, enzi, na kila jina litajwalo. Alimketisha Yesu si tu kwa wakati huu lakini kwa wakati ujao pia. 22Mungu amevitiisha vitu vyote chini ya miguu ya Kristo. Amemfanya yeye kichwa juu ya vitu vyote katika kanisa. 23Ni kanisa kwamba ndilo mwili wake, ukamilifu wake ambaye hujaza vitu vyote katika njia zote.
Wimbo wa katikati
1Kwa kiongozi wa muziki; weka kwenye mtindo wa gittith. Zaburi ya Daudi. Yahweh Bwana wetu, ni jinsi gani jina lako ni tukufu katika dunia yote, wewe ufunuaye utukufu wako juu mbinguni. 2Kutoka katika midomo ya watoto na vichanga umeumba sifa kwa sababu ya utukufu wako, ili kuwanyamazisha maadui wote na walipa kisasi wote. 3Ninapozitazama mbingu, ambazo vidole vyako vimeumba, mwezi na nyota, ambazo umeziweka kila mmoja katika nafasi yake, 4Binadamu ni nani hata umtazame, na watu hata uwajali wao? 5Umewaumba chini kidogo kuliko viumbe vya mbinguni na umewazunguka na utukufu na heshima. 6Umemfanya binadamu kutawala kazi ya mikono yako; umeviweka vitu vyote chini ya miguu yake:
Injili
8Ninawaambia, yeyote atakayenikiri Mimi mbele za watu, Mwana wa Adamu atamkiri mbele za malaika wa Mungu. 9Lakini yeyeyote atakayenikana mbele za watu naye atakanwa mbele ya Malaika wa Mungu. 10Yeyote atakayesema neno baya juu ya Mwana wa Adamu, atasamehewa, lakini yeyote atakayemkufuru Roho Mtakatifu, hatasamehewa. 11Watakapowapeleka mbele za wakuu wa masinagogi, watawala, na wanye mamlaka, msiogope juu na namna ya kuongea katika kujitetea au nini mtakachosema, 12kwa kuwa Roho Mtakatifu atawafundisha namna mtakavyosema kwa wakati huo.”
Watakatifu wa siku
- Mt. Ignasi wa Antiokia, askofu na shahidi
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili A, mwaka wa siku za kazi II.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki