Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Oktoba 2026 › 19 Oktoba
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 19 Oktoba 2026
Jumatatu · Juma la 29 la Mwaka
Sikukuu na watakatifu
Jumatatu ya Juma la 29 la Mwaka
Kumbukumbu ya hiari · Rangi ya liturujia: kijani
Mt. Paulo wa Msalaba, padre · Kumbukumbu ya hiari
Watakatifu Yohane de Brébeuf na Isaka Jogues, mapadre, na wenzao, mashahidi · Kumbukumbu ya hiari
Masomo ya siku
Somo la kwanza
1Kama vile mlivyo kuwa mmekufa katika makosa na dhambi zenu. 2Ilikuwa katika haya kwamba kwanza mlienenda kulingana na nyakati za ulimwengu huu. Mlikuwa mkienenda kwa kufuata mtawala wa mamlaka ya anga. Hii ndiyo roho yake yule afanyaye kazi katika wana wa kuasi. 3Sisi wote hapo mwanzo tulikuwa miongoni mwa hawa wasioamini. Tulikuwa tukitenda kwa namna ya tamaa mbaya za miili yetu. Tulikuwa tukifanya mapenzi ya mwili na ufahamu wetu. Tulikuwa kwa asili wana wa ghadhabu kama wengine. 4Lakini Mungu ni mwingi wa rehema kwa sababu ya pendo lake kubwa alilotupenda sisi. 5Wakati tulipokuwa wafu katika makosa yetu, alituleta pamoja katika maisha mapya ndani ya Kristo. Ni kwa neema kwamba mmeokolewa. 6Mungu alitufufua pamoja na kutufanya kukaa pamoja katika mahali pa mbingu ndani ya Kristo Yesu. 7Alifanya hivi ili katika nyakati zijazo aweze kutuonesha utajiri mkuu wa neema yake. Hutuonesha sisi hili kwa njia ya wema wake ndani ya Kristo Yesu. 8Kwa neema mmeokolewa kwa njia ya imani. Na hii haikutoka kwetu. Ni zawadi ya Mungu. 9Haitokani na matendo. Matokeo yake, asiwepo mmoja wapo wa kujisifu. 10Kwa sababu sisi tu kazi ya Mungu, tumeumbwa katika Kristo Yesu kutenda matendo mema. Ni matendo haya ambayo Mungu aliyapanga tangu zamani za kale kwa ajili yetu, ili tutembee katika hayo.
Wimbo wa katikati
1Zaburi ya shukrani. Mpigieni Yahwe kelele za furaha, enyi nchi yote. 2Mtumikieni Yahwe kwa furaha; njoni mbele zake mkiimba kwa furaha. 3Mjue kuwa Yahwe ni Mungu; alituumba, na sisi tu wake. Tu watu wake na kondoo wa malisho yake. 4Ingieni malangoni mwake kwa shukrani na nyuani mwake kwa kusifu. Mshukuruni yeye na litukuzeni jina lake. 5Maana Yahwe ni mwema; uaminifu wa agano lake wadumu milele na uaminifu wake vizazi na vizazi vyote.
Injili
13Mtu mmoja katika kusanyiko akamwambia, “Mwalimu, mwambie ndugu yangu anigawie sehemu ya uruthi wangu.” 14Yesu akamjibu, ni nani aliye niweka kuwa mwamuzi na mpatanishi kati yenu.? 15Ndipo akawaambia, Jihadharini na kila namna ya tamaa, kwa sababu uzima wa mtu hauko katika wingi wa vitu alivyo navyo.” 16Yesu akawaambia mfano, akisema, Shamba la mtu mmoja tajiri lilizaa sana, 17na akajiuliza ndani yake, akisema, nitafanyaje kwani sina mahali pa kuhifadhi mazao yangu? 18Akasema, nitafanya hivi. Nitavunja ghala zangu ndogo na kujenga iliyo kubwa, na kuyahifadhi mazao yangu yote na vitu vingine. 19Nitaiambia nafsi yangu, “Nafsi, umejiwekea akiba ya vitu vingi kwa miaka mingi. Pumzika, ule, unywe na kustarehe.” 20Lakini Mungu akamwambia, ewe mtu mpumbavu, usiku wa leo wanahitaji roho kutoka kwako, na vitu vyote ulivyoviandaa vitakuwa vya nini? 21Ndivyo itakavyokuwa kwa kila mtu anayejiwekea mali na si kujitajirisha kwa ajili ya Bwana.
Watakatifu wa siku
- Mt. Paulo wa Msalaba, padre
- Watakatifu Yohane de Brébeuf na Isaka Jogues, mapadre, na wenzao, mashahidi
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili A, mwaka wa siku za kazi II.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki