Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Oktoba 2026 › 9 Oktoba

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 9 Oktoba 2026

Ijumaa · Juma la 27 la Mwaka

Sikukuu na watakatifu

Ijumaa ya Juma la 27 la Mwaka

Kumbukumbu ya hiari · Rangi ya liturujia: kijani

Mt. Dionisi, askofu, na wenzake, mashahidi · Kumbukumbu ya hiari

Mt. Yohane Leonardi, padre · Kumbukumbu ya hiari

Mt. Yohane Henry Newman, padre na mwalimu wa Kanisa · Kumbukumbu ya hiari

Kufunga na toba

Siku ya toba

Kila Ijumaa ni siku ya toba; kila baraza la maaskofu huamua jinsi inavyoadhimishwa: kujinyima nyama au tendo lingine la toba. Kufunga kunawahusu wenye miaka 18 hadi 59, kujinyima nyama kuanzia miaka 14.

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Gal 3:7–17

7Kwa namna ile ile eleweni kwamba, wale ambao wanaamini ni watoto wa Abrahamu. 8Andiko lilitabiri kwamba Mungu angewahesabia haki watu wa mataifa kwa njia ya imani. Injili ilihubiriwa kwanza kwa Abrahamu: “katika wewe mataifa yote yatabarikiwa”. 9Ili baadaye wale ambao wana imani wabarikiwe pamoja na Abrahamu, ambaye alikuwa na imani. 10Wale ambao wanategemea matendo ya sheria wako chini ya laana. Kwa kuwa imeandikwa, “Amelaaniwa kila mtu ambaye hashikamani na mambo yote yaliyoandikwa katika kitabu cha sheria, kuyatenda yote.” 11Sasa ni wazi kwamba Mungu hamhesabii haki hata mmoja kwa sheria, kwa kuwa “Mwenye haki ataishi kwa imani”. 12Sheria haitokani na imani, lakini badala yake “Ambaye hufanya mambo haya katika sheria, ataishi kwa sheria.” 13Kristo alitukomboa sisi kutoka katika laana ya sheria wakati alipofanyika laana kwa ajili yetu. Kwa kuwa imeandikwa, “Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti.” 14Lengo lilikuwa kwamba, baraka ambazo zilikuwa kwa Ibrahimu zingekuja kwa watu wa mataifa katika Kristo Yesu, ili kwamba tuweze kupokea ahadi ya Roho kupitia imani. 15Ndugu, ninazungumza kwa namna ya kibinadamu. Hata wakati ambapo agano la kibinadamu limekwisha kuwekwa imara, hakuna awezaye kupuuza au kuongezea. 16Sasa ahadi zilisemwa kwa Ibrahim na kwa kizazi chake. Haisemi, “kwa vizazi,” kumaanisha wengi, bali badala yake kwa mmoja pekee, “kwa kizazi chako,” ambaye ni Kristo. 17Sasa nasema hivi, sheria ambayo ilikuja miaka 430 baadaye, haiondoi agano la nyuma lililowekwa na Mungu.

Wimbo wa katikati

Zab 111:1–6

1Msifuni Yahwe. Nitamshukuru Yahwe kwa moyo wangu wote katikati ya kusanyiko la wanye haki, na katika mkutano. 2Kazi za Yahwe ni kuu, zikisubiriwa na wale wazitamanio. 3Kazi yake ni adhama na utukufu, na haki yake yadumu milele. 4Hufanya mambo makuu ambayo yatakumbukwa; Yahwe ni mwenye huruma na neema. 5Huwapa chakula wafuasi wake waaminifu. Siku zote atalikumbuka agano lake. 6Alionesha uweza wa kazi zake kwa watu wake kwa kuwapa urithi wa mataifa.

Injili

Lk 11:15–26

15Lakii watu wengine wakasema, huyu anaondo mapepo kwa Beelzebul, mkuu wa mapepo 16Wengine walimjaribu na kumtaka awaonyeshe ishara kutoka mbinguni. 17Lakini Yesu aliyatambua mawazo yao na kuwaambia, “Kila ufalme utakaogawanyika itakuwa ukiwa, na nyumba iliyo gawanyika itaanguka. 18Kama Shetani atakuwa amegawanyika, ufalme wake utasimamaje? Kwa sababu mwasema natoa mapepo kwa Belzebuli 19Kama mimi natoa mapepo kwa Belzebuli, je wenzenu wanatoa mapepo kwa njia gani? Kwa sababu hii, wao watawahukumu ninyi. 20Lakini, kama natoa mapepo kwa kidole cha Mungu, basi uflame wa Mungu umewajia. 21Mtu mwenye nguvu aliye na silaha akilinda nyumba yake, vitu vyake vitakaa salama. 22Lakini akivamiwa na mtu mwenye nguvu zaidi, Yule mtu mwenye nguvu atamnyang'anya silaha zake, na kuzichukua mali zake zote. 23Yeye asiye pamoja nami yuko kinyume nami, na yeye asiyekusanya pamoja nami hutapanya. 24Pepo mchafu amtokapo mtu, huenda na kutafuta mahali pasipo na maji ili ajipumzishe. Atakapokuwa amekosa, husema, 'nitarudi nilipotoka. 25Akirudi na kukuta nyumba imefagiliwa na imekaa vizuri. 26Hivyo huenda na kutafuta mapepo saba walio waovu kuliko yeye mwenyewe na kuwaleta waje wakae mahali pale. Na hali ya mtu huyo huwa mbaya kuliko ilivyokuwa mara ya kwanza.”

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 9 Oktoba

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili A, mwaka wa siku za kazi II.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki