Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Oktoba 2026 › 10 Oktoba

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 10 Oktoba 2026

Jumamosi · Juma la 27 la Mwaka

Sikukuu na watakatifu

Jumamosi ya Juma la 27 la Mwaka

Kumbukumbu ya hiari · Rangi ya liturujia: kijani

Kumbukumbu ya Bikira Maria siku ya Jumamosi · Kumbukumbu ya hiari

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Gal 3:22–29

22Lakini badala yake, andiko limefunga mambo yote chini ya dhambi. Mungu alifanya hivi ili kwamba ahadi yake ya kutuokoa sisi kwa imani katika Yesu Kristo iweze kupatikana kwa wale wanao amini. 23Lakini kabla ya imani katika Kristo haijaja, tulikuwa tumefungwa na kuwa chini ya sheria hadi uje ufunuo wa imani. 24Kwa hiyo sheria ilifanyika kiongozi wetu hadi Kristo alipokuja, ili kwamba tuhesabiwe haki kwa imani. 25Sasa kwa kuwa imani imekuja, hatuko tena chini ya mwangalizi. 26Kwa kuwa ninyi nyote ni watoto wa Mungu kupitia imani katika Kristo Yesu. 27Wote ambao mlibatizwa katika Kristo mmejivika Kristo. 28Hakuna Myahudi wala Myunani, mtumwa wala huru, mwanaume wala mwanamke, kwa kuwa ninyi nyote ni mmoja katika Kristo Yesu. 29Kama ninyi ni wa Kristo, basi ni uzao wa Ibrahimu, warithi kwa mujibu wa ahadi.

Wimbo wa katikati

Zab 105:2–7

2Mwimbieni yeye, mwimbieni sifa yeye; semeni matendo yake yote ya ajau. 3Mjivune katika utakatifu wa jina lake; moyo wao wamtafutao Yahwe ufurahi. 4Mtafuteni Yahwe na nguvu zake; utafuteni uwepo wake siku zote. 5Kumbukeni mambo ya ajabu aliyoyatenda, 6miujiza yake na amri zitokazo kinywani mwake, enyi kizazi cha Ibrahimu mtumishi wake, enyi watu wa Yakobo, wachaguliwa wake. 7Yeye ni Yahwe, Mungu wetu. Amri zake ziko juu ya nchi yote.

Injili

Lk 11:27–28

27Ilitokea kwamba alipokuwa akisema maneno hayo, mwanamke fulani alipasa sauti yake zaidi ya wote kwanye mkutano wa watu na kusema “ Limebarikiwa tumbo lililo kuzaa na matiti uliyoyanyonya” 28Lakini yeye akasema, wamebarikiwa wale wasikio neno la Mungu na kulitunza.

Watakatifu wa 10 Oktoba

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili A, mwaka wa siku za kazi II.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki