Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Oktoba 2026 › 8 Oktoba

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 8 Oktoba 2026

Alhamisi · Juma la 27 la Mwaka

Sikukuu na watakatifu

Alhamisi ya Juma la 27 la Mwaka

Siku ya kawaida · Rangi ya liturujia: kijani

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Gal 3:1–5

1Wagalatia wajinga, ni jicho gani ovu lililowaharibu? Je Yesu Kristo hakuoneshwa kama msulubiwa mbele ya macho yenu? 2Mimi nataka tu kufahamu hili kutoka kwenu. Je mlimpokea Roho kwa matendo ya sheria au kwa kuamini kile mlichosikia? 3Je, ninyi ni wajinga kiasi hiki? Je mlianza katika Roho ili mmalize katika mwili? 4Je mliteseka kwa mambo mengi bure, kama kweli yalikuwa ya bure? 5Je yeye atoaye Roho kwenu na kutenda matendo ya nguvu kati yenu hufanya kwa matendo ya sheria au kwa kusikia pamoja na imani?

Wimbo wa katikati

Lk 1:69–75

69Ametuinulia pembe ya wokovu katika nyumba ya mtumishi wake Daudi, kutoka miongoi mwa mwa ukoo wa mtumishi wake Daudi, 70kama alivyosema kwa kinywa cha manabii wake waliokuweko katika nyakati za kale. 71Atatuoka kutoka kwa adui zetu na kutoka mikononi mwa wote wanaotuchukia. 72Atafanya hivi kuonesha rehema kwa baba zetu, na kukumbuka agano lake takatifu, 73kiapo alichokisema kwa Abrahamu baba yetu. 74Aliapa kuthibitha kwamba ingewezekana kumtumikia Yeye bila hofu, baada ya kuokolewa kutoka katika mikononi ya adui zetu. 75katika utakatifu na haki mbele zake siku zetu zote.

Injili

Lk 11:5–13

5Yesu akawaambia, “Ni nani kwenu atakuwa na rafiki, ambaye atamuendea usiku, na kumwambia, Rafiki niazime mikate mitatu. 6Kwa sababu rafiki yangu amenijia sasa hivi kutoka safarini, nami sina cha kumuandalia.' 7Na yule aliyeko ndani akamjibu, usinitaabishe, Mlango umekwisha kufungwa, na watoto wangu, pamoja nami tumekwisha kulala kitandani. Siwezi kuamka na kukupa wewe mikate. 8Nawaambia, japo kuwa haamki na kukupatia mikate kama rafiki yake, kwa sababu ya kuendelea kumgongea bila aibu, ataamka na kukupatia vipande vingi vya mikate kulingana na mahitaji yako. 9Nami pia nawaambieni, Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtapata, pigeni hodi nanyi mtafunguliwa. 10Kwa kuwa kila mtu aombaye atapokea, na kila mtu atafutaye atapata, na kila mtu apigaye hodi, mlango utafunguliwa kwake. 11Ni baba yupi miongoni mwenu, mwanaye akimuomba samaki atampa nyoka badala yake.? 12Au akimuomba yai atampa nge badala yake?. 13Kwa hiyo, ikiwa ninyi mlio waovu mnajuwa kuwapa watoto wenu zawadi nzuri, je si zaidi sana Baba yenu wa mbinguni kwamba atawapa Roho Mtakatifu hao wamuombao?”

Watakatifu wa 8 Oktoba

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili A, mwaka wa siku za kazi II.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki