Bible Explorer

Gundua › Wafalme na Mambo ya Nyakati kando kwa kando › Sauli na Daudi

Wafalme na Mambo ya Nyakati kando kwa kando · Sauli na Daudi

Mashujaa wa Daudi

2 Sam 23:8–39 · 1 Nya 11:10–47

2 Samweli

2 Sam 23:8–39

8Haya ni majina ya askari wa Daudi: Yashobeamu Mhakmoni alikuwa kiongozi wa mashujaa. Aliua watu mia nne wakati mmoja.

9Baada yake alikuwa Elieza mwana wa Dodo, mwana wa mwahohi, mmoja wa mashujaa watatu wa Daudi. Alikuwepo walipowashinda Wafilisti waliokuwa wamekusanyika kwa vita, na wakati watu wa Israeli walipokuwa wamekimbia.

10Elieza akasimama na kuwapiga Wafilisti mpaka mkono wake ukachoka, mpaka mkono wake ukang'ang'ania mpini wa upanga wake. Siku hiyo Yahwe akatoa ushindi mkuu. Jeshi likarejea kwa ajili ya kuteka tu nyara za waliouawa na Elieza.

11Baada yake alikuwa Shama mwana wa Agee, Mharari. Wafilisti wakajikusanya pamoja palipokuwa na shamba la dengu, na jeshi likawakimbia.

12Lakini Shama akasimama katikati ya shamba na kulitetea. Aliwauwa Wafilisti, na Yahwe akaleta ushindi mkuu.

13Watatu kati ya askari thelathini walishuka kwa Daudi nyakati za mavuno, katika pango la Adulamu. Jeshi la Wafilisti lilikuwa limepiga kambi katika bonde la Mrefai.

14Wakati huo Daudi alikuwa katika ngome yake, pangoni, wakati Wafilisti walikuwa wanaimilk Bethlehemu.

15Daudi alitamani maji na akasema, “Kama ingekuwa mtu mmoja angenipa maji ya kunywa kutoka kisima kilichopo Bethlehemu, kisima kilichopo langoni!”

16Hivyo mashujaa hawa watatu wakapita kati ya jeshi la Wafilisti na kuchota maji katika kisima cha Bethlehemu, kilichopo langoni. Wakachukua maji na kuyaleta kwa Daudi, lakini yeye akakataa kuyanywa. Badala yake akayamwaga mbele za Yahwe.

17Kisha akasema, “Iwe mbali nami, Yahwe, kwamba niyanywe haya. Je ninywe damu ya watu waliohatarisha maisha yao?” Hivyo akakataa kuyanywa. Haya ni mambo yaliyofanywa na mashujaa watatu.

18Abishai, nduguye Yoabu na mwana wa Seruya, alikuwa akida wa watatu. Alipigana kwa mkuki wake na watu mia tatu na akawauwa wote mara. Mara kwa mara alitajwa kati ya mashujaa watatu.

19Hakuwa maarufu kuliko wale watatu? Alifanywa akida wao. Lakini, umaarufu wake haukulingana na umaarufu wa wale mashujaa watatu.

20Benaya kutoka Kabseeli mwana wa Yehoyada; alikuwa mtu hodari aliyefanya matendo makuu. Aliwauwa wana wawili wa Arieli wa Moabu. Pia alishuka shimoni na kuuwa simba wakati wa theruji.

21Na alimwua Mmisri aliyekuwa mtu mnene sana. Mmisri alikuwa na mkuki mkononi, lakini Benaya alipigana naye kwa fimbo tu. Aliuchukua mkuki mkononi mwa Mmisri na kisha kumwua nao.

22Benaya mwana wa Yehoyada alifanya matendo haya, naye alitajwa kati ya mashujaa watatu.

23Alikuwa na heshima kuliko mashujaa thelathini kwa ujumla wao, lakini hakuwa na heshima kama wale mashujaa watatu. Hata hivyo Daudi alimweka kuwa mlinzi wake.

24Wafuatao ni wale watu thelathini: Asaheli nduguye Yoabu, Elhanani mwana wa Dodo kutoka Bethlehemu,

25Shama Mharodi, Elika Mharodi,

26Helesi Mpeloni, Ira mwana wa Ikeshi Mtekoi,

27Abi Ezeri Mwanathothi, Mebunai Mhushathi,

28Salmoni Mhahoi, Maharai Mnetofathi;

29Helebu mwana wa Baana, Mnetofathi, Itai mwana wa Rabai kutoka Gibea ya Wabenjamini,

30Benaya Mpirathoni, Hidai wa mabonde ya Gaashi.

31Abieliboni Mwarbathi, Azmawethi Mbarhumi,

32Eliaba Mshalboni, wana wa Yasheni, Yonathani mwana wa Shama Mharari;

33Ahiamu mwana wa Sharari Mharari,

34Elifeleti mwana wa Ahasbai Mmaakathi, Eliamu mwana wa Ahithofeli Mgiloni,

35Hezro Mkarmeli, Parai Mwarbi,

36Igali mwana wa Nathani kutoka Soba, Bani kutoka kabila la Gadi,

37Zeleki Mwamoni, Naharai Mbeerothi, mbeba silaha wa Yoabu mwana wa Seruya,

38Ira Mwithri, Garebu Mwithri,

39Uria Mhiti - jumla yao thelathini na wanane.

1 Mambo ya Nyakati

1 Nya 11:10–47

10Hawa walikuwa viongozi Daudi aliyo kuwa nao, waliyo jionyesha imara katika ufalme wake, pamoja na Israeli, kumfanya mfalme, kutii neno la Yahweh kuhusu Israeli.

11Hii ni orodha ya wanajeshi shupavu wa Daudi. Yashobeami, mwana wa Mhakimoni, alikuwa mkuu wa kikosi cha thelathini. Aliwaua wanaume mia tatu na mkuki wake katika sehemu moja.

12Baada ya yeye alikuwa Eleazari mwana wa Dodo, Mahohi, aliyekuwa mmoja wa wanaume watatu hodari.

13Alikuwa na Daudi huko Pasidamimu, na pale Wafilisti wakakusanyika pamoja kwa mapambano, ambapo palikuwa na uwanja wa ngano na jeshi liliwakimbia Wafilisti.

14Walisimama katikati ya uwanja. Wakautetea na kuwakata Wafilisti na Yahweh akawaokoa na ushindi mkubwa.

15Kisha watatu wa viongozi thelathini wakashuka chini kwenye mwamba wa Daudi, katika pango la Adulamu. Jeshi la Wafilisti walieka kambi katika bonde la Refaim.

16Kwa wakati huo Daudi alikuwa katika ngome yake, pangoni, Wafilisti walikita kambi yao Bethilehemu.

17Daudi alikuwa na kiu ya maji na akasema, “Laiti mtu akanipatia maji ya kunywa kutoka kisima kilicho Bethilehemu, kisima kilicho pembeni mwa lango!”

18Hawa wanaume hodari watatu wakatoboa kupita jeshi la Wafilisti na kuchota maji kwenye kisima cha Bethilehemu, kisima pembeni mwa lango. Wakachukuwa maji na kumletea Daudi, lakini alikataa kunywa. Badala yake, akamwaga chini kwa Yahweh.

19Kisha akasema, “Yahweh, iwe mbali na mimi, kwamba ni yanywe haya maji. Je ninywe damu ya wanaume walio hatarisha maisha yao?” Kwa sababu wameeka maisha ya hatarini, akakataa kunywa. Haya ni mambo wanaume hodari watatu walio fanya.

20Abishai kaka wa Yoabu, alikuwa kiongozi wa watatu. Alitumia mkuki wake dhidi ya watu mia tatu na kuwaua. Ametajwa pamoja na wale watatu.

21Kati ya wale watatu, yeye alipewa heshima mara mbili na akawa kiongozi wao. Japo hakuwa mmoja wa miongoni mwao.

22Benaia mwana wa Yehoiada alikuwa mwanaume mwenye nguvu aliye fanya mambo makuu. Aliua wana wawili wa Arieli wa Moabu. Pia alishuka chini ya shimo na kumuua simba wakati theluji ikianguka.

23Alimua hadi Mmisri, mwanaume mwenye mita mbili na theluthi moja. Mmisri alikuwa na mkuki kama gongo la mshonaji, lakini alimfuata chini na fimbo tu. Akakamata mkuki katika mkono wa Mmisri na kumuua na mkuki wake.

24Benaia mwana wa Yehoiada alifanya haya matukio, na akatajwa miongoni mwa wale wanaume hodari watatu.

25Alisifika zaidi ya wale wanajeshi thelathini kwa ujumla, lakini hakuwa pewa hadhi ya wale wanajeshi watatu hodari. Daudi alimueka kiongozi wa walinzi wake.

26Wanaume hodari walikuwa Asaheli kaka wa Yoabu, Elhanani mwana wa Dodo wa Bethilehemu,

27Shamothi Mherori, Helezi Mpeloni,

28Ira mwana wa Ikeshi Mtekoi, Abi Eza Manathothi,

29Sibekai Mhushathite, Ilai Mahohite,

30Maharai Mnetofathi, Heledi mwana wa Baana Mnetofathite,

31Itai mwana wa Ribai wa Gibea uzao wa Benjamini, Benaia Mpirathoni,

32Hurai wa mabonde ya Gaashi, Abieli Marbathi,

33Azmavethi Mbaharumi, Eliaba Mshaalboni,

34Mwana wa Hashemu Mgizoni, Yonathani mwana wa Shagee Mhararite,

35Ahiamu mwana wa Sacari Mhararite, Elifali mwana wa Uri,

36Hefa Mmekarathi, Ahija Mpeloni,

37Hezro Mcarmeli, Maarai mwana wa Ezibai,

38Yoeli kaka wa Nathani, Mibhari mwana wa Hagiri,

39Zeleki Mamoni, Naharai Mberothi (mbeba ngao ya Yoabu mwana wa Zeruia),

40Ira Mithire, Garebu Mithire,

41Uria Mhiti, Zabadi mwana wa Ahlai,

42Adina mwana wa Shiza Mreubeni (kiongozi wa Wareubeni) na thelathini pamoja nae,

43Hanani mwana wa Maaka, na Yoshafati Mmithini,

44Uzia Mashiterathi, Shama na Yeieli wana wa Hothamu Waaroeri,

45Jediaeli mwana wa Shimri, Joha (kaka yake Mtize),

46Elieli Mmahavi, Yeribai na Yoshavia mwana wa Elnaamu, Ithima Mmoabi,

47Elieli, Obedi, na Yaasieli Wamezobai.

Yamewekwa alama: maneno yaliyo katika masimulizi yote, katika tafsiri unayosoma. Maneno ya kawaida zaidi (“na”, “yeye”) hayawekwi alama; neno katika umbo jingine huenda lisiwekwe.

Swahili Unlocked Literal Bible · Sambamba zimechaguliwa kwa mkono kutoka maandiko na kulinganishwa na marejeo ya OpenBible.info (CC BY). Kando kwa kando huwekwa tukio au neno lilelile tu. OpenBible.info · CC BY