Gundua › Wafalme na Mambo ya Nyakati kando kwa kando › Anguko la Yerusalemu
Wafalme na Mambo ya Nyakati kando kwa kando · Anguko la Yerusalemu
Yehoyakini afunguliwa
2 Fal 25:27–30 · Yer 52:31–34
2 Fal 25:27–3027Ilitokea baadaye katika mwaka wa thelathini na saba wa utumwa wa Yekonia mfalme wa Yuda, katika mwezi wa kumi na mbili, siku ya ishirini na saba ya mwezi, Evil-merodaki mfalme wa Babeli akamtoa Yekonia mfalme wa Yuda kutoka gerezani. Hii ilitokea katika mwaka ambao Evil-Merodaki alipoanza kutawala.
28Akaongea naye kwa ukarimu na kumpatia kiti kizuri zaidi kuliko kile cha wafalme wengine ambao walikuwa pamoja naye Babeli.
29Evil-Merodaki akamvua Yekonia nguo za gerezani,
30na Yekinia akala siku zote kwenye meza ya mfalme katika maisha yake yote yaliyokuwa yamebakia.
Yer 52:31–3431Ikawa baadaye katika mwaka wa thelathini na saba wa kufungwa kwake Yohoyakini, mfalme wa Yuda, katika mwezi wa kumi na mbili, siku ya ishirini na tano ya mwezi, Evili Merodaki, mfalme wa Babeli akamfungua Yehoyakini mfalme wa Yuda kutoka kifungoni. Ilikuwa mwaka ambao Evili Merodaki alianza kutawala.
32Akaongea naye kwa upole na akampa kiti cha heshima kuliko cha wafalme wengine aliokuwa pamoja nao huko Babeli.
33Evili Merodaki akaondoa mavazi ya gerezani ya Yehoyakini, na Yehoyakini akala chakula cha daima katika meza ya mfalme siku zote zilizosalia za maisha yake.
34Na alipewa posho ya chakula cha kila siku kwa maisha yake yote yaliyosalia mpaka siku ya kufa kwake.
Yamewekwa alama: maneno yaliyo katika masimulizi yote, katika tafsiri unayosoma. Maneno ya kawaida zaidi (“na”, “yeye”) hayawekwi alama; neno katika umbo jingine huenda lisiwekwe.
Swahili Unlocked Literal Bible · Sambamba zimechaguliwa kwa mkono kutoka maandiko na kulinganishwa na marejeo ya OpenBible.info (CC BY). Kando kwa kando huwekwa tukio au neno lilelile tu. OpenBible.info · CC BY