Mwanzo › Mistari maarufu ya Biblia › 2 Wakorintho 5:17
Mstari wa Biblia · ULB
2 Wakorintho 5:17
Kwa hiyo, ikiwa mtu yeyote yuko ndani ya Kristo, yeye ni kiumbe kipya. Mambo ya kale yamepita. Tazama, yamekuwa mapya.
Soma sura nzima: 2 Wakorintho 5
Katika muktadha
14Kwa kuwa upendo wa Kristo watushurutisha, kwa sababu tuna uhakika na hili: kuwa mtu mmoja alikufa kwa ajili ya wote, na kwa hiyo wote wamekufa.
15Na Kristo alikufa kwa ajili ya wote, ili kwamba wale wanaoishi wasiishi tena kwa ajili yao wenyewe. Badala yake, lazima waishi kwa ajili yake yeye ambaye alikufa na alifufuliwa.
16Kwa sababu hii, kuanzia sasa na kuendelea hatumuhukumu mtu kulingana na viwango vya wanadamu, ingawa hapo kwanza tulimtazama Kristo katika namna hii. Lakini sasa hatumuhukumu yeyote kwa namna hii tena.
17Kwa hiyo, ikiwa mtu yeyote yuko ndani ya Kristo, yeye ni kiumbe kipya. Mambo ya kale yamepita. Tazama, yamekuwa mapya.
18Vitu vyote hivi vyatoka kwa Mungu. Alitupatanisha sisi kwake mwenyewe kupitia Kristo, na ametupatia huduma ya upatanisho.
19Hiyo ni kusema, katika Kristo, Mungu anaupatanisha ulimwengu kwake mwenyewe, sio kuhesabu makosa yao dhidi yao. Anawekeza kwetu ujumbe wa upatanisho.
20Kwa hiyo tunateuliwa kama wawakilishi wa Kristo, kana kwamba Mungu alikuwa anafanya rufaa yake kupitia sisi. Tunawasihi ninyi kwa ajili ya Kristo: “Mpatanishwe kwa Mungu!”
Kwa Kiingereza
Therefore if anyone is in Christ, he is a new creation. The old has passed away. Behold, the new has come!Marejeo mtambuka
Vifungu ambavyo wasomaji huviunganisha na hiki mara nyingi zaidi.
Nitawapatia moyo mpya na roho mpya sehemu zenu za ndani, na nitautoa moyo wa jiwe kutoka kwenye nyama zenu. Kwa kuwa nitawapatia moyo wa nyama.Lazima mvue mambo yote yanayoendana na mwenendo wenu wa zamani, utu wa zamani. Ni utu wa zamani unaooza kwa sababu ya tamaa za udanganyifu. Vueni utu wenu wa zamani ili kwamba mfanywe upya katika roho ya akili zenu. Fanyeni hivi ili muweze kuvaa utu mpya, unaoendana na Mungu. Umeumbwa katika haki na utakatifu wa kweli.Msifikirie hayo mambo yaliyopita, wala kuyafikiria mambo ya zamani. Tazama ninakaribia kufanya mambo mapya; sasa yanakaribia kutokea; Je humyajui haya? Nitafanya njia jangani na na mikondo ya maji katika jangwaYesu akamjibu, “Amini, amini, mtu hawezi kuingia katika ufalme wa Mungu asipozaliwa mara ya pili.”Uniumbie moyo safi, Mungu, na uifanye upya roho ya haki ndani yangu.Nitawapatia moyo mmoja, na nitaweka roho mpya kati yao. Nitaondoa moyo wa jiwe kutoka kwenye miili wao na kuwapatia moyo wa nyama,Kwa hiyo basi hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu.Kwa kuwa haijalishi kutahiriwa au kutokutahiriwa kuwa ni kitu. Badala yake uzao mpya ni muhimu.Vyanzo: OpenBible.info, CC BY 4.0 · Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki