Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Desemba 2027 › 19 Desemba
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 19 Desemba 2027
Jumapili · Juma la 4 la Majilio
Sikukuu na watakatifu
Dominika ya 4 ya Majilio
Dominika · Rangi ya liturujia: zambarau
Masomo ya siku
Somo la kwanza
2Lakini wewe, Bethlehemu Efrata, hata kama uko mdogo miongoni mwa koo za Yuda, kutoka kweko mmoja atakuja kwangu kutawala Israeli, ambaye mwanzo wake ni kutoka nyakati za kale, toka milele. 3Kwa hiyo Mungu atawapa, hata mda wa yeye aliye katika uchungu kuzaa mtoto, na mabaki ya ndugu zake yatawarudia wana wa Israeli. 4Atasimama na kuchunga kundi lake kwa nguvu za Yahwe, kwa ukuu wa enzi ya jina la Yahwe Mungu wake. Watabaki, kwa kuwa atakuwa mashuhuri hata mwisho wa dunia. 5Atakuwa amani yetu. Wakati Waashuru watakapokuja kwenye nchi yetu, wakati wakitembea dhidi ya boma yetu, kisha kisha tutainuka juu yao wachungaji saba na viongozi nane juu ya watu.
Wimbo wa katikati
1Kwa kiongozi wa muziki, seti kwenye mtindo wa Shoshannim Eduth. Zaburi ya Asafu. Usikie, Mchungaji wa Israel, wewe uliye muongoza Yusufu kama kundi; wewe uketiye juu ya makerubi, utuangazie! 2Machoni pa Efraimu na Benjamini na Manase, uziinue nguvu zako; njoo na utuokoe. 14Urudi, Ee Mungu wa majeshi; kutoka mbinguni utazame chini na uuangalie na kuujali huu mzabibu. 15Huu ni mzizi ambao mkono wako wa kuume umeupanda, mashina ambayo wewe uliyafanya yakue. 17Mkono wako na uwe juu ya mtu aliye mkono wako wa kuume, kwa mwana wa mtu uliyemfanya imara kwa ajili yako mwenyewe. 18Ndipo hatuta kuacha wewe; utuhuishe, nasi tutaliita jina lako.
Somo la pili
5Wakati Kristo alipokuja duniani, alisema, “Hamkutamani matoleo au dhabihu, badala yake, mliandaa mwili kwa ajili yangu. 6Hamkuwa na thamani katika matoleo yote ya kuteketezwa au dhabihu kwa ajili ya dhambi. 7Kisha nilisema, “Ona, hapa ninayafanya mapenzi yako, Mungu, kama ilivyoandikwa kunihusu mimi katika gombo”. 8Alisema kama ilivyo semwa hapo juu: “Hamkutamani dhabihu, matoleo, au sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya dhambi, wala hukuona furaha ndani yake” dhabihu ambazo zinatolewa kulingana na sheria. 9Kisha alisema, “Ona, niko hapa kufanya mapenzi yako”. Ameweka pembeni taratibu zilizo za awali ili kuimarisha zile za pili. 10Katika taratibu za pili, tumekwisha tengwa kwa Mungu kwa mapenzi yake kupitia kujitoa kwa mwili wa Yesu Kristo mara moja kwa nyakati zote.
Injili
39Ndipo katika siku hizo Mariamu aliondoka na kwa haraka alikwenda katika nchi ya vilima, kwenye mji katika nchi ya Yudea. 40Alikwenda nyumbani mwa Zekaria na akamsalimia Elizabeti. 41Sasa, ilitokea kwamba Elizabeti aliposikia salamu ya Mariamu, mtoto tumboni mwake akaruka, na Elizabeti akajazwa na Roho Mtakatifu. 42Akapaza sauti yake na kusema kwa sauti kuu, “umebarikiwa wewe zaidi miongoni mwa wanawake, na mtoto aliyemo tumboni mwako amebarikiwa. 43Na imekuwaje kwangu kwamba, mama wa Bwana wangu ilipasa aje kwangu? 44Kwa kuwa tazama, iliposikika masikoni mwangu sauti ya kusalimia kwako, mtoto tumboni mwangu akaruka kwa furaha. 45Na amebarikiwe mwanamke yule ambaye aliamini ya kwamba ungetokea ukamilifu wa mambo yale aliyoambiwa kutoka kwa Bwana.”
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili C, mwaka wa siku za kazi II.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki