Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Desemba 2027 › 19 Desemba

Kalenda ya Kiorthodoksi · 6 Desemba (kalenda ya Juliani)

Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 19 Desemba 2027

Jumapili · Sauti ya 1

Sikukuu na watakatifu

Jumapili ya 26 baada ya Pentekoste

Mfungo wa Kuzaliwa kwa Bwana

Samaki wanaruhusiwa

Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.

Masomo ya siku

Sala ya Jioni: somo

Mit 10; Mit 3; Mit 8 (mistari iliyochaguliwa)

Sala ya Jioni: somo

Mit 10:31–11:12

31Katika kinywa cha wale watendao haki hutoka tunda la hekima, bali ulimi wa kupotosha utakatwa. 32Midomo ya wale watendao mema huyajua yanayokubalika, bali kinywa cha waovu, huyajua yanayopotosha. 11:1Yehova huchukia vipimo ambavyo havipo sahihi, bali hufurahia uzani dhahiri. 2Kinapokuja kiburi, ndipo aibu huja, bali unyenyekevu huleta hekima. 3Uadilifu wa wenye haki huwaongoza, bali udanganyifu wa njia za wajanja utawaangamiza. 4Utajiri hauna thamani siku ya ghadhabu, bali kwa kutenda haki hujilinda na mauti. 5Mwenendo wa mtu mwema huinyosha njia yake, bali waovu wataanguka kwa sababu ya uovu wao. 6Mwenendo mwema wa wale wampendezao Mungu utawalinda salama, bali wadanganyifu hunaswa katika shauku zao. 7Mtu mwovu anapokufa, tumaini lake hupotea na tumaini lililokuwa katika nguvu zake linakuwa si kitu. 8Yule atendaye haki hulindwa katika taabu na badala yake taabu humjia mwovu. 9Kwa kinywa chake asiyeamini Mungu humwangamiza jirani yake, bali kwa maarifa wale watendao haki hulindwa salama. 10Wanapofanikiwa watendao haki, mji hufurahi, waovu wanapoangamia, kunakuwa na kelele za furaha. 11Kwa zawadi nzuri za wale wanaompendeza Mungu, mji unakuwa mkubwa; kwa kinywa cha waovu mji huvurugwa. 12Mtu mwenye dharau kwa rafiki yake hana akili, bali mtu mwenye ufahamu hunyamaza.

Sala ya Jioni: somo

Haimo katika tafsiri hii

Injili ya 4 ya Sala ya Alfajiri

Lk 24:1–12

1Mapema sana siku ya kwanza ya juma, walikuja kaburini, wakileta manukato ambayo walikuwa wameyaandaa. 2Wakakuta jiwe limevingirishwa mbali na kaburi. 3Wakaingia ndani, lakini hawakuukuta mwili wa Bwana Yesu. 4Ilitokea kwamba, wakati wamechanganyikiwa kuhusu hili, ghafla, watu wawili walisimama katikati yao wamevaa mavazi ya kung'aa. 5Wanawake wakiwa wamejaa hofu na wakiinamisha nyuso zao chini, wakawaambia wanawake, “Kwanini mnamtafuta aliye hai miongoni mwa wafu? 6Hayupo hapa, ila amefufuka! Kumbukeni alivyosema nanyi alipokuwa angali Galilaya, 7akisema kwamba Mwana wa Adamu lazima atolewe kwenye mikono ya watu wenye dhambi na asulubishwe, na siku ya tatu, afufuke tena.” 8Wale wanawake wakakumbuka maneno yake, 9na wakarudi kutoka kaburini na wakawaambia mambo haya yote wale kumi na moja na wengine wote. 10Basi Maria Magdalena, Joana, Maria mama wa Yakobo, na wanawake wengine pamoja nao wakatoa taarifa hizi kwa mitume. 11Lakini ujumbe huu ukaonekana kama mzaha tu kwa mitume, na hawakuwaamini wale wanawake. 12Hata hivyo Petro aliamka, na akakimbia kuelekea kaburini, na akichungulia na kuangalia ndani, aliona sanda peke yake. Petro kisha akaondoka akaenda nyumbani kwake, akistaajabu nini ambacho kimetokea.

Waraka

Efe 5:8–19

8Kwa kuwa ninyi mwanzo mlikuwa giza, lakini sasa mmekuwa nuru katika Bwana. Hivyo tembeeni kama watoto wa nuru. 9Kwa kuwa matunda ya nuru yanajumuisha uzuri wote, haki na ukweli. 10Tafuta kile kinacho furahisha kwa Bwana. 11Usiwepo ushiriki katika kazi za giza zisizo na matunda, badala yake ziweke wazi. 12Kwa sababu mambo yanayofanywa na wao sirini ni aibu sana hata kuyaelezea. 13Mambo yote, yanapofichuliwa na nuru, huwa wazi, 14kwa kuwa Kila kitu kilichofichuliwa kinakuwa nuruni. Hivyo husema hivi, “Amka, wewe uliyelala, na inuka kutoka wafu na Kristo atang'aa juu yako.” 15Hivyo iweni makini jinsi mtembeavyo, siyo kama watu wasio werevu bali kama werevu. 16Ukomboeni muda kwa kuwa siku ni za uovu. 17Msiwe wajinga, badala yake, fahamuni nini mapenzi ya Bwana. 18Msilewe kwa mvinyo, huongoza kwenye uharibifu, badala yake mjazwe na Roho Mtakatifu. 19Zungumzeni na kila mmoja wenu kwa zaburi, na sifa, na nyimbo za rohoni. Imbeni na sifuni kwa moyo kwa Bwana.

Waraka (Mt. Nikolao)

Ebr 13:17–21

17Tiini na kujishusha kwa viongozi wenu, kwani wanaendelea kuwalinda kwa ajili ya nafsi zenu, kama wale watakaotoa hesabu. Tiini ili kwamba viongozi wenu waweze kuwatunza kwa furaha, na sio kwa huzuni, ambayo haitawasaidia. 18Tuombeni, kwani tuna uhakikwa kwamba tuna dhamira njema, tunatamani kuishi maisha ya heshima katika mambo yote. 19Na nyote ninawatia moyo zaidi mfanye hivi, ili kwamba niweze kurudi kwenu hivi karibuni. 20Sasa Mungu wa amani, ambaye aliwaleta tena kutoka kwa wafu mchungaji mkuu wa kondoo, Bwana wetu Yesu, kwa damu ya agano la milele, 21Atawapa uwezo kwa kila jambo zuri kufanya mapenzi yake, akifanya kazi ndani yetu iliyo njema ya kupendeza machoni pake, kupitia Yesu Kristo, kwake uwe utukufu milele na milele. Amina.

Injili

Lk 17:12–19

12Alipokua akiingia kwenye kijiji kimoja, huko alikutana na watu kumi waliokuwa na ukoma. Wakasimama mbali 13wakapaza sauti wakasema “Yesu, Bwana tuhurumie.” 14Alipowaona akawaambia, “Nendeni mkajionyeshe kwa makuhani.” nao walipokua wakienda wakatakasika. 15Mmoja wao alipoona kwamba amepona, akarudi kwa sauti kuu akimsifu Mungu. 16Akapiga magoti miguuni mwa Yesu akamshukuru. Yeye alikua msamaria. 17Yesu akajibu, akasema, “Je hawakutakasika wote kumi? Wako wapi wale wengine tisa? 18Hakuna hata mmoja aliyeonekana kurudi ili kumtukuza Mungu, isipokuwa huyu mgeni?” 19Akamwambia, “Inuka na uende zako imani yako imekuponya.”

Injili (Mt. Nikolao)

Lk 6:17–23

17Kisha Yesu alitelemka pamoja nao toka mlimani na kusimama mahali tambarare. Idadi kubwa ya wanafunzi wake walikuwa huko, pamoja na idadi kubwa ya watu kutoka Uyahudi na Yerusalemu, na kutoka pwani ya Tiro na Sidoni. 18Walikuja kumsikiliza na kuponywa magonjwa yao. Watu waliokuwa wakisumbuliwa na pepo wachafu waliponywa pia. 19Kila mmoja kwenye hilo kusanyiko alijaribu kumgusa kwa sababu nguvu za uponyaji zilikuwa zikitokea ndani yake, na aliwaponya wote. 20Kisha akawaangalia wanafunzi wake, na kusema, “Mmebarikiwa ninyi mlio maskini, kwa maana ufalme wa Mungu ni wenu. 21Mmebarikiwa ninyi mlio na njaa sasa, kwa maana mtashibishwa. Mmebarikiwa ninyi mliao sasa, kwa maana mtacheka. 22Mmebarikiwa ninyi ambao watu watakapowachukia na kuwatenga na kuwashutumu ninyi kwamba ni waovu, kwa ajili ya Mwana Adamu. 23Furahini katika siku hiyo na kurukaruka kwa furaha, kwa sababu hakika mtakuwa na thawabu kubwa mbinguni, kwa maana baba zao waliwatendea vivyohivyo manabii.

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 19 Desemba

Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 6 Desemba katika kalenda ya kanisa ni 19 Desemba katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki