Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Novemba 2027 › 15 Novemba

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 15 Novemba 2027

Jumatatu · Juma la 33 la Mwaka

Sikukuu na watakatifu

Jumatatu ya Juma la 33 la Mwaka

Kumbukumbu ya hiari · Rangi ya liturujia: kijani

Mt. Alberto Mkuu, askofu na mwalimu wa Kanisa · Kumbukumbu ya hiari

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Haimo katika tafsiri hii

Wimbo wa katikati

Zab 119:53, 61, 134, 150, 155, 158

53Hasira kali imenishikilia kwa sababu ya waovu wanaoikataa sheria yako. 61Kamba za waovu zimenifunga; nami sijaisahau sheria yako. 134Unikomboe dhidi ya wanadamu waonevu ili niyatii maagizo yako. 150Wale wanaonitesa wananikaribia, lakini wako mbali na sheria yako. 155Wokovu uko mbali na waovu, maana hawazipendi amri zako. 158Nimewaona wasaliti wakitia kinyaa kwa sababu hawalishiki neno lako.

Injili

Lk 18:35–43

35Ikawa Yesu ulipokaribia Yeriko, mtu mmoja kipofu alikuwa ameketi kando ya barabara akiomba msaada, 36aliposikia umati wa watu ukipita aliuliza nini kinatokea. 37Wakamwambia kwamba Yesu wa Nazareti anapita. 38Hivyo yule kipofu akalia kwa sauti, akisema, 'Yesu, Mwana wa Daudi, unirehemu.' 39wale waliokuwa wakitembea walimkemea huyo kipofu, wakamwambia anyamaze. Lakini yeye akazidi kulia kwa sauti, 'Mwana wa Daudi, unirehemu. 40Yesu akasimama akaamuru mtu yule aletwe kwake. Kisha yule kipofu alipomkaribia, Yesu akamwuliza, 41'Unataka nikufanyie nini?' Akasema, 'Bwana, nataka kuona.' 42Yesu akamwambia, 'Upate kuona. Imani yako imekuponya. ' 43Mara hiyo akapata kuona, akamfuata Yesu akimtukuza Mungu. Walipoona hili, watu wote wakamsifu Mungu.

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 15 Novemba

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki