Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Novemba 2027 › 16 Novemba
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 16 Novemba 2027
Jumanne · Juma la 33 la Mwaka
Sikukuu na watakatifu
Jumanne ya Juma la 33 la Mwaka
Kumbukumbu ya hiari · Rangi ya liturujia: kijani
Mt. Gertrudi Mkuu, bikira · Kumbukumbu ya hiari
Mt. Margareta wa Scotland · Kumbukumbu ya hiari
Masomo ya siku
Somo la kwanza
Haimo katika tafsiri hii
Wimbo wa katikati
1Zaburi ya Daudi, wakati alipo mkimbia mtoto wake Absalom. Yahewh, maadui zangu wako wangapi! Ni wengi wamekuja kinyume na mimi. 2Ni wengi wanaonisema, “Hakuna msaada wowote kutoka kwa Mungu kwa ajili yake.” Selah 3Bali wewe, Yahweh, u ngao yangu pande zote, utukufu wangu, na uniinuaye kichwa changu. 4Nampazia Yahweh sauti yangu, na yeye ananijibu kutoka katika mlima wake mtakatifu. 5Nilijilaza chini na kusinzia; na niliamka, kwa kuwa Yahweh alinilinda. 6Sitaogopa kusanyiko la watu ambao wamejipanga kinyume na mimi pande zote. 7Inuka, Yahweh! Uniokoe, Mungu wangu! Kwa kuwa utawapiga maadui zangu wote kwenye taya zao; utayavunja meno ya waovu.
Injili
1Yesu aliingia na kupita katikati ya Yeriko. 2Na hapo palikuwa na mtu mmoja aitwaye Zakayo. Ambaye alikuwa mkuu wa watoza ushuru tena mtu tajiri. 3Alikuwa anajaribu kumwona Yesu ni mtu wa namna gani, lakini hakuweza kuona kwa sababu ya umati wa watu, kwa kuwa alikuwa mfupi wa kimo. 4Hivyo, alitangulia mbio mbele za watu, akapanda juu ya mkuyu ili aweze kumwona, kwa sababu Yesu alikaribia kupita njia hiyo. 5Wakati Yesu alipofika mahali pale, aliangalia juu akamwambia, 'Zakayo, shuka upesi, maana leo ni lazima nishinde nyumbani mwako.' 6Akafanya haraka, akashuka na kumkaribisha kwa furaha. 7Watu wote walipoona hayo, wakalalamika, wakisema, 'Amekwenda kumtembelea mtu mwenye dhambi.' 8Zakayo akasimama akamwambia Bwana, Tazama Bwana nusu ya mali yangu nawapa maskini, na ikiwa nimemnyang'anya mtu yeyote kitu, nitamrudishia mara nne. ' 9Yesu akamwambia, 'Leo wokovu umefika katika nyumba hii, kwa sababu yeye pia ni mwana wa Ibrahimu. 10Kwa maana Mwana wa Mtu amekuja kutafuta na kuokoa watu waliopotea. '
Watakatifu wa siku
- Mt. Gertrudi Mkuu, bikira
- Mt. Margareta wa Scotland
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki