Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Oktoba 2027 › 2 Oktoba

Kalenda ya Kiorthodoksi · 19 Septemba (kalenda ya Juliani)

Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 2 Oktoba 2027

Jumamosi · Wiki ya 15 baada ya Pentekoste · Sauti ya 5

Sikukuu na watakatifu

Jumamosi baada ya Kutukuzwa kwa Msalaba

Mfungo

Hakuna mfungo

Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.

Masomo ya siku

Waraka (Jumamosi baada ya Kutukuzwa kwa Msalaba)

1 Kor 1:26–29

26Angalia wito wa Mungu juu yenu, kaka na dada zangu. Si wengi wenu mlikuwa na hekima katika viwango vya kibinadamu. Si wengi wenu mlikuwa na nguvu. Si wengi wenu mlizaliwa katika ukuu. 27Lakini Mungu alichagua vitu vijinga vya dunia ili kuviaibisha vyenye hekima. Mungu alichagua kilicho dhaifu katika dunia kukiaibisha chenye nguvu. 28Mungu alichagua kile kilicho cha hali ya chini na kilichodharauliwa katika dunia. Alichagua hata vitu ambavyo havikuhesabiwa kuwa kitu, kwa kuvifanya si kitu vitu vilivyo na thamani. 29Alifanya hivi ili asiwepo yeyote aliye na sababu ya kujivuna mbele zake.

Waraka

1 Kor 4:17–5:5

17Hiyo ndiyo sababu nilimtuma kwenu Timotheo, mpendwa wangu na mtoto mwaminifu katika Bwana. Atawakumbusheni njia zangu katika Kristo, kama ninavyofundisha kila mahali na kila kanisa. 18Sasa baadhi yenu wanajisifu, wakitenda kana kwamba sitakuja kwenu. 19Lakini nitakuja kwenu kitambo, kama Bwana akipenda. Ndipo nitajua si maneno yao tu wanaojisifu, lakini nitaona nguvu zao. 20Kwa kuwa ufalme wa Mungu hauwi katika maneno bali katika nguvu. 21Mnataka nini? Nije kwenu na fimbo au kwa upendo na katika roho ya upole? 5:1Tumesikia taarifa kuwa kuna zinaa miongoni mwenu, aina ya zinaa ambayo haipo hata katikati ya watu wa Mataifa. Tuna taarifa kwamba mmoja wenu analala na mke wa baba yake. 2Nanyi mwajisifu! Badala ya kuhuzunika? Yule aliyefanya hivyo anapaswa kuondolewa miongoni mwenu. 3Ingawa sipo pamoja nanyi kimwili lakini nipo nanyi kiroho, nimekwisha mhukumu yeye aliyefanya hivi, kama vile nilikuwepo. 4Mnapokutanika pamoja katika jina la Bwana wetu Yesu, na roho yangu ipo pale kama kwa nguvu za Bwana wetu Yesu, nimekwisha mhukumu mtu huyu. 5Nimekwisha kumkabidhi mtu huyu kwa Shetani ili kwamba mwili wake uharibiwe, ili roho yake iweze kuokolewa katika siku ya Bwana.

Injili (Jumamosi baada ya Kutukuzwa kwa Msalaba)

Yn 8:21–30

21Basi akawaambia tena, “Ninaenda zangu; mtanitafuta na mtakufa katika dhambi zenu. Kule niendako, hamuwezi kuja.” 22Wayahudi wakasema, “Atajiua mwenyewe, yeye ambaye alisema, 'kule niendako hamuwezi kuja'?” 23Yesu akawaambia, “Mnatoka chini; mimi natoka juu. Ninyi ni wa Ulimwengu huu; mimi si wa ulimwengu huu. 24Kwa hiyo, naliwaambieni kuwa mtakufa katika dhambi zenu. Vinginevyo muamini kuwa MIMI NDIYE, mtakufa katika dhambi zenu”. 25Kwa hiyo wakamwambia, “Wewe ni nani?” Yesu akawaambia, Yale niliyowaambia tangu mwanzo. 26Ninayo mambo mengi ya kuzungumza na kuhukumu juu yenu. Hata hivyo, yeye aliyenituma ni wa kweli; na mambo niliyoyasikia kutoka kwake, mambo haya nayasema kwa Ulimwengu.” 27Hawakumuelewa kwamba alikuwa akiongea nao kuhusu Baba. 28Yesu akasema, “Mtakapomwinua juu Mwana wa Mtu, ndipo mtakapojua kuwa MIMI NDIYE, na kwamba sifanyi lolote kwa nafsi yangu. Kama Baba alivyonifundisha, ninazungumza mambo haya. 29Yeye aliyenituma yuko pamoja nami, na yeye hajaniacha peke yangu, kwani kila mara nafanya yale yanayompendeza.” 30Wakati Yesu akisema mambo haya, wengi walimwamini.

Injili

Mt 24:1–13

1Yesu alitoka hekaluni na kwenda zake. Wanafunzi wake walimwendea na kumuonesha majengo ya hekalu. 2Laikni aliwajibu na kuwaambia, “Je, hamuyaoni mambo haya yote? Kweli nawaambia, hakuna jiwe litalobaki juu ya lingine bila kubomolewa.” 3Na alipokaa katika Mlima wa Mizeituni, wanafunzi wake walimwendea kwa faragha na kusema, “Tuambie, mambo haya yatatokea lini? Kitu gani kitakuwa dalili ya kuja kwako na mwisho wa ulimwengu?” 4Yesu aliwajibu na kuwaambia, “Iweni makini kwamba asije mtu akawapotosha. 5Kwa kuwa wengi watakuja kwa jina langu. Watasema, 'Mimi ndiye Kristo', na watawapotosha wengi. 6Mtasikia vita na taarifa za vita. Angalieni msije mkawa na wasiwasi, kwa kuwa mambo haya hayabudi kutokea; lakini ule mwisho utakuwa bado. 7Kwa kuwa taifa litainuka dhidi ya taifa jingine, na ufalme dhidi ya ufalme. Kutakuwa na njaa na matetemeko ya ardhi katika sehemu mbalimbali. 8Lakini mambo haya yote ni mwanzo tu wa uchungu wa kujifungua. 9Ndipo watawatoa kwa ajili ya mateso na kuwaua. Mtachukiwa na mataifa yote kwa sababu ya jina langu. 10Ndipo wengi watajikwaa na kusalitiana na watachukiana wenyewe kwa wenyewe. 11Manabii wengi wa uongo watatokea na kuwadanganya wengi. 12Kwa sababu uovu utaongezeka, upendo wa wengi utapoa. 13Lakini atakaye vumilia mpaka mwisho, ataokolewa.

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 2 Oktoba

Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 19 Septemba katika kalenda ya kanisa ni 2 Oktoba katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki