Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Oktoba 2027 › 1 Oktoba
Kalenda ya Kiorthodoksi · 18 Septemba (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 1 Oktoba 2027
Ijumaa · Wiki ya 15 baada ya Pentekoste · Sauti ya 5
Sikukuu na watakatifu
Baada ya Sikukuu ya Kutukuzwa kwa Msalaba wa Bwana
Siku ya mfungo
Mfungo: pamoja na mafuta
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Waraka
8Hata kabla, wakati hamkumjua Mungu, mlikuwa watumwa kwa wale ambao kwa asili si miungu kabisa. 9Lakini sasa kwamba mnamjua Mungu, au kwamba mnajulikana na Mungu, kwa nini mnarudi tena kwenye kanuni dhaifu za kwanza na zisizo za thamani? Je mnataka kuwa watumwa tena? 10Mnashika kwa uangalifu siku maalumu, miandamo ya miezi, majira, na miaka. Ninaogopa kwa ajili yenu. 11Ninaogopa kwamba kwa namna fulani nimejitaabisha bure. 12Ninawasihi, ndugu, muwe kama nilivyo, kwa kuwa pia nimekuwa kama mlivyo. Hamkunikosea. 13Bali mnajua kwamba ilikuwa ni kwa sababu ya ugonjwa wa mwili kwamba nilihubiri injili kwenu kwa mara ya kwanza. 14Ingawa hali yangu ya mwili iliwaweka katika jaribu, hamkunidharau au kunikataa. Badala yake mlinipokea kama malaika wa Mungu, kana kwamba nilikuwa Kristo Yesu mwenyewe. 15Kwa hiyo, iko wapi sasa furaha yenu? kwa kuwa ninashuhudia kwenu kwamba, ikiwezekana, mungelin'goa macho yenu na kunipa mimi. 16Hivyo sasa, je nimekuwa adui yenu kwa sababu ninawaambia ukweli? 17Wanawatafuta kwa shauku, bali si kwa mema. Wanataka kuwatenganisha ninyi na mimi ili muwafuate. 18Ni vyema daima kuwa na shauku kwa sababu zilizo njema, na si tu wakati ninapokuwa pamoja nanyi. 19Wanangu wadogo, ninaumwa uchungu kwa ajili yenu tena mpaka Kristo aumbike ndani yenu. 20Ningependa kuwepo pale pamoja nanyi sasa na kugeuza sauti yangu, kwa sababu ninamashaka juu yenu. 21Niambieni, ninyi ambao mnatamani kuwa chini ya sheria, hamsikii sheria isemavyo?
Injili
45Mara akawaambia wapande kwenye mashua waende sehemu nyingine, hadi Bethsaida, wakati Yeye akiwaaga makutano. 46Walipokuwa wamekwisha kuondoka, akaenda mlimani kuomba. 47Kulipokuwa jioni, na mashua yao wakati huo ikiwa katikati ya bahari, naye alikuwa peke yake nchi kavu. 48Na aliwaona wakitaabika kupiga makasia kwa sababu upepo uliwazuia. Ilipokaribia asubuhi akawaendea, akitembea juu ya maji, na alitaka kuwapita. 49Lakini walipomwona anatembea juu ya maji, wakaingiwa na wasiwasi wakidhani ni mzimu hata wakapiga kelele. 50kwa sababu walimwona wakajawa na hofu. Mara akasema nao akawaambia, “Muwe wajasiri! ni mimi! Msiwe na hofu.” 51Akaingia ndani ya mashua, na upepo ukaacha kuvuma, nao wakamshangaa kabisa. 52Hivyo hawakuwa wameelewa maana ya ile mikate. Maana akili zao zilikuwa na uelewa mdogo. 53Nao walipovuka ng'ambo, walifika nchi ya Genesareti mashua ikatia nanga.
Watakatifu wa siku
- Mtakatifu Mtawa Eumeni, Askofu wa Gortina (karne ya 7)
- Kutangazwa mtakatifu kwa Mtakatifu Mtawa Eufrosini wa Suzdal, aliyeitwa Theodulia duniani (1698)
- Mtakatifu Mtawa Hilarioni wa Optina (1873)
- Wafiadini wa Kikasisi Aleksi na Petro, mapadri (1918)
- Wafiadini wa Kikasisi Amfilokio, Askofu wa Krasnoyarsk, Yohana, Boris, Mikaeli, Vladimir, Benyamini, Konstantino, mapadri, na Mfiadini Sergio (1937)
- Mfiadini Ariadna (karne ya 2)
- Wafiadini Sofia na Irina (karne ya 3)
- Wafiadini Bidzina, Shalva na Elizbar, wakuu wa Ksani (1660)
- Mfiadini Kastori
- Ikoni za Mama wa Mungu: ya Molchensk (1405), ile iitwayo “Mponyaji” (karne ya 18), na ya Staraya Russa (1888)
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 18 Septemba katika kalenda ya kanisa ni 1 Oktoba katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki