Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Oktoba 2027 › 2 Oktoba
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 2 Oktoba 2027
Jumamosi · Juma la 26 la Mwaka
Sikukuu na watakatifu
Jumamosi ya Juma la 26 la Mwaka
Kumbukumbu · Rangi ya liturujia: nyeupe
Malaika Walinzi Watakatifu · Kumbukumbu
Masomo ya siku
Somo la kwanza
Haimo katika tafsiri hii
Wimbo wa katikati
32Wanyenyekevu wameona na kufurahi; ninyi mnao matafuta Mungu, mioyo yenu itiwe nguvu. 33Maana Yahwe husikia wenye uhitaji naye hawadharau wafungwa wake. 34Mbingu na nchi zimsifu yeye, bahari na vyote vitembeavyo majini. 35Kwa maana Mungu ataiokoa Sayuni na ataujenga tena mji wa Yuda; watu wataishi huko na kupata umiliki wao. 36Ukoo wa watumishi wake watairithi; nao walipendao jina lake wataishi humo.
Injili
1Muda huo huo wanafunzi wakaja kwa Yesu na kumwambia, “Ni nani aliye mkubwa katika ufalme wa mbinguni?” 2Yesu akamwita mtoto mdogo, akamweka katikati yao, 3na kusema, “Kweli nawaambieni, msipotubu na kuwa kama watoto wadogo hamtaweza kuingia katika ufalme wa Mungu. 4Hivyo yeyote ajishushaye kama mtoto mdogo, mtu kama huyo ni mkuu katika ufalme wa mbinguni. 5Na yeyote ampokeaye mtoto mdogo kwa jina langu anipokea mimi. 10Tazameni kwamba msije mkamdharau mmoja wa wadogo hawa. Kwa maana nawambieni kuwa mbinguni kuna malaika wao siku zote wakiutazama uso wa Baba yangu aliye mbinguni.
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki