Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Septemba 2027 › 30 Septemba
Kalenda ya Kiorthodoksi · 17 Septemba (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 30 Septemba 2027
Alhamisi · Wiki ya 15 baada ya Pentekoste · Sauti ya 5
Sikukuu na watakatifu
Baada ya Sikukuu ya Kutukuzwa kwa Msalaba wa Bwana
Mfungo
Hakuna mfungo
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Waraka
23Lakini kabla ya imani katika Kristo haijaja, tulikuwa tumefungwa na kuwa chini ya sheria hadi uje ufunuo wa imani. 24Kwa hiyo sheria ilifanyika kiongozi wetu hadi Kristo alipokuja, ili kwamba tuhesabiwe haki kwa imani. 25Sasa kwa kuwa imani imekuja, hatuko tena chini ya mwangalizi. 26Kwa kuwa ninyi nyote ni watoto wa Mungu kupitia imani katika Kristo Yesu. 27Wote ambao mlibatizwa katika Kristo mmejivika Kristo. 28Hakuna Myahudi wala Myunani, mtumwa wala huru, mwanaume wala mwanamke, kwa kuwa ninyi nyote ni mmoja katika Kristo Yesu. 29Kama ninyi ni wa Kristo, basi ni uzao wa Ibrahimu, warithi kwa mujibu wa ahadi. 4:1Ninasema kwamba maadamu mrithi ni mtoto, hana tofauti na mtumwa, hata ingawa ni mmiliki wa mali yote. 2Badala yake, yuko chini ya waangalizi na wadhamini mpaka wakati uliowekwa na baba yake. 3Kadhalika pia na sisi, tulipokuwa watoto, tulishikiliwa katika utumwa wa kanuni za kwanza za ulimwengu. 4Lakini wakati sahihi ulipofika, Mungu alimtuma mwanawe, mzaliwa wa mwanamke, mzaliwa chini ya sheria. 5Alifanya hivi ili kuwakomboa wale waliokuwa chini ya sheria, ili kwamba tupokee hali ya kuwa kama wana.
Injili
30Na mitume, walikusanyika pamoja mbele ya Yesu, wakamweleza yote waliyofanya na waliyoyafundisha. 31Naye akawaambia, “Njooni wenyewe mahali pa faragha na tupumzike kwa muda.” Watu wengi walikuwa wanakuja na kuondoka, hata hawakupata nafasi ya kula. 32Hivyo wakapanda mashua wakaenda mahali pa faragha peke yao. 33Lakini waliwaona wakiondoka na wengi wakawatambua, kwa pamoja walikimbia kwa miguu kutoka miji yote, nao wakafika kabla yao. 34Walipofika pwani, aliona umati mkubwa na akawahurumia, kwa sababu walikuwa kama kondoo wasiokuwa na mchungaji. Na akaanza kuwafundisha mambo mengi. 35Muda ulipoendelea sana, wanafunzi wakamjia wakamwambia,”Hapa ni mahali pa faragha na muda umeendelea. 36Uwaage waende miji ya jirani na vijiji ili wakajinunulie chakula.” 37Lakini akawajibu akisema, “Wapeni ninyi chakula.” Wakamwambia, “Tunaweza kwenda na kununua mikate yenye thamani ya dinari mia mbili na kuwapa wale?” 38Akawambia,” Mna mikate mingapi? Nendeni mkaangalie.” walipopata wakamwambia, “Mikate mitano na samaki wawili.” 39Akawaamuru watu waketi katika makundi juu ya majani mabichi. 40Wakawaketisha katika makundi; makundi ya mamia kwa hamsini. 41Kisha akachukua mikate mitano na samaki wawili, na kutazama mbinguni, akaibariki kisha akawapa wanafunzi waweke mbele ya umati. Na kisha aligawa samaki wawili kwa watu wote. 42Walikula wote hadi wakatosheka. 43Walikusanya vipande vya mikate iliyobaki, Vikajaa vikapu kumi na viwili, na pia vipande vya samaki. 44Na walikuwa wanaume elfu tano waliokula mikate. 45Mara akawaambia wapande kwenye mashua waende sehemu nyingine, hadi Bethsaida, wakati Yeye akiwaaga makutano.
Watakatifu wa siku
- Wafiadini Vera, Nadezhda, Lyubov (Imani, Tumaini, Upendo) na mama yao Sofia (karibu 137)
- Watawa Wafiadini Paulo, Theodosio, Nikodemo na Serafim (1918)
- Mtawa Mfiadini Irina (1931)
- Mfiadini Yohana (1941)
- Mtawa Mfiadini Aleksandra (1943)
- Wafiadini Theodotia (karibu 230) na Agathoklia
- Wafiadini Peleo na Nilo, Maaskofu wa Misri, Zenoni, padri, Patermuthio, Eliya na wengine 151 (karibu 310)
- Askofu Mtakatifu Yoakimu, Patriarki wa Aleksandria
- Ikoni za Mama wa Mungu za Konstantinopoli (1071) na za Makariev (1442)
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 17 Septemba katika kalenda ya kanisa ni 30 Septemba katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki