Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Septemba 2027 › 29 Septemba
Kalenda ya Kiorthodoksi · 16 Septemba (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 29 Septemba 2027
Jumatano · Wiki ya 15 baada ya Pentekoste · Sauti ya 5
Sikukuu na watakatifu
Baada ya Sikukuu ya Kutukuzwa kwa Msalaba wa Bwana
Siku ya mfungo
Mfungo: pamoja na mafuta
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Waraka
15Ndugu, ninazungumza kwa namna ya kibinadamu. Hata wakati ambapo agano la kibinadamu limekwisha kuwekwa imara, hakuna awezaye kupuuza au kuongezea. 16Sasa ahadi zilisemwa kwa Ibrahim na kwa kizazi chake. Haisemi, “kwa vizazi,” kumaanisha wengi, bali badala yake kwa mmoja pekee, “kwa kizazi chako,” ambaye ni Kristo. 17Sasa nasema hivi, sheria ambayo ilikuja miaka 430 baadaye, haiondoi agano la nyuma lililowekwa na Mungu. 18Kwa kuwa kama urithi ungelikuja kwa njia ya sheria, usingekuwa tena umekuja kwa njia ya ahadi. Lakini Mungu aliutoa bure kwa Ibrahimu kwa njia ya ahadi. 19Kwa nini sasa sheria ilitolewa? Iliongezwa kwa sababu ya makosa, mpaka mzao wa Ibrahimu aje kwa wale ambao kwao alikuwa ameahidiwa. Sheria iliwekwa katika shinikizo kupitia malaika kwa mkono wa mpatanishi. 20Sasa mpatanishi humaanisha zaidi ya mtu mmoja, bali Mungu ni mmoja peke yake. 21Kwa hiyo je sheria iko kinyume na ahadi za Mungu? La hasha! Kwa kuwa kama sheria iliyokuwa imetolewa ilikuwa na uwezo wa kuleta uzima, haki ingepatikana kwa sheria. 22Lakini badala yake, andiko limefunga mambo yote chini ya dhambi. Mungu alifanya hivi ili kwamba ahadi yake ya kutuokoa sisi kwa imani katika Yesu Kristo iweze kupatikana kwa wale wanao amini.
Waraka (Mt. Eufemia)
1Na kwa hiyo, kufanya kazi pamoja, tunawasihi ninyi msiipokee neema ya Mungu pasipo matokeo. 2Kwa kuwa anasema, “Wakati uliokubalika nilikuwa makini kwenu, na katika siku ya wokovu niliwasaidia.” Tazama, sasa ni wakati uliokubalika. Tazama, sasa ni siku ya wokovu. 3Hatuweki jiwe la kizuizi mbele ya mtu yeyote, kwa kuwa hatuitakii huduma yetu iletwe katika sifa mbaya. 4Badala yake, tunajihakiki wenyewe kwa matendo yetu yote, kwamba tu watumishi wa Mungu. Tu watumishi wake katika wingi wa ustahimilivu, mateso, dhiki, ugumu wa maisha, 5kupigwa, vifungo, ghasia, katika kufanya kazi kwa bidii, katika kukosa usingizi usiku, katika njaa, 6katika usafi, maarifa, uvumilivu, wema, katika Roho Mtakatifu, katika upendo halisi. 7Tu watumishi wake katika neno la kweli, katika nguvu ya Mungu. Tuna silaha ya haki kwa ajili ya mkono wa kuuume na wa kushoto. 8Tunafanya kazi katika heshima na kudharauliwa, katika kashfa na sifa. Tunatuhumiwa kuwa wadanganyifu na wakati tu wakweli. 9Tunafanya kazi kana kwamba hatujulikani na bado tunajulikana vizuri. Tunafanya kazi kama wanaokufa na -Tazama! - bado tunaishi. Tunafanya kazi kama tunaoadhibiwa kwa ajili ya matendo yetu lakini sio kama waliohukumiwa hata kufa. 10Tunafanya kazi kama wenye masikitiko, lakini siku zote tuna furaha. Tunafanya kazi kama maskini, lakini tunatajirisha wengi. Tunafanya kazi kana kwamba hatupati kitu bali kama tunaomiliki kila kitu.
Injili
7Aliwaita wale wanafunzi kumi na wawili akaanza kuwatuma wawili wawili. Aliwapa mamlaka juu ya pepo wachafu, 8na kuwaamuru wasichukue chochote wanapokwenda isipokuwa fimbo tu. Wasichukue mkate, wala mkoba, wala fedha kibindoni; 9lakini wavae viatu, na siyo kanzu mbili. 10Na akawaambia, “Nyumba yoyote mtakayoingia, kaeni hapo mpaka mtakapoondoka. 11Na mji wowote usipowapokea wala kuwasikiliza, ondokeni kwao, kung'uteni mavumbi ya miguu yenu, iwe ushuhuda kwao.” 12Nao wakaenda wakitangaza watu watubu na kuacha dhambi zao. 13Waliwafukuza pepo wengi, na waliwapaka mafuta wagonjwa na wakaponywa.
Injili (Mt. Eufemia)
36Mmoja wa mafarisayo alimwomba Yesu aende kula pamoja naye. Baada ya Yesu kuingia kwenye nyumba ya farisayo, aliegemea kwenye meza ili ale. 37Tazama kulikuwa na mwanamke mmoja katika jiji hilo aliyekuwa na dhambi. Akagundua kuwa alikuwa amekaa kwa Farisayo, akaleta chupa ya manukato. 38Alisimama nyuma yake karibu na miguu yake huku akilia. Tena alianza kulowanisha miguu yake kwa machozi, na kuifuta kwa nywele za kichwa chake, akiibusu miguu yake na kuipaka manukato. 39Na yule farisayo aliyekuwa amemwalika Yesu alipoona hivyo, akawaza mwenyewe akisema, “Kama huyu mtu angekuwa nabii, angejua huyu ni nani na ni aina gani ya mwanamke anayemgusa, ya kuwa ni mwenye dhambi. 40Yesu akajibu na kumwambia, “Simoni nina kitu cha kukuambia. “Akasema” “Kiseme tu mwalimu!” 41Yesu akasema “Kulikuwa na wadaiwa wawili kwa mkopeshaji mmoja. Mmoja alikuwa anadaiwa dinari mia tano na wa pili alidaiwa dinari hamsini. 42Na walipokuwa hawana pesa ya kumlipa aliwasamehe wote. Sasa ni nani atampenda zaidi? 43Simoni akamjibu na kusema, “Nadhani aliyesamehewa zaidi.”Yesu akamwambia, “Umehukumu kwa usahihi.” 44Yesu akamgeukia mwanamke na kusema kwa Simoni, “Unamwona huyu mwanamke. Nimeingia kwenye Nyumba yako. Hukunipa maji kwa ajili ya miguu yangu, lakini huyu, kwa machozi yake, alilowanisha miguu yangu na kuifuta kwa nywele zake. 45Hukunibusu, lakini yeye, tangu alipoingia humu hakuacha kunibusu miguu yangu. 46Hukuipaka miguu yangu kwa mafuta, lakini ameipaka miguu yangu kwa manukato. 47Kwa jambo hili, nakwambia kwamba alikuwa na dhambi nyingi na amesamehewa zaidi, na pia alipenda zaidi. Lakini aliyesamehewa kidogo, hupenda kidogo tu.” 48Baadaye akamwambia mwanamke, “Dhambi zako zimesamehewa” 49Wale waliokaa mezani pamoja naye wakaanza kusemezana wao kwa wao, “Huyu ni nani mpaka anasamehe dhambi?” 50Na Yesu akamwambia mwanamke, “Imani yako imekuokoa. Enenda kwa amani”
Watakatifu wa siku
- Mfiadini Mkuu Eufemia, wa kusifiwa sana (304)
- Mfiadini wa Kikasisi Gregori, padri (1937)
- Mfiadini wa Kikasisi Sergio, padri (1942)
- Kuhamishwa kwa masalia ya Mwenye Haki Aleksi wa Moscow (2001)
- Mfiadini Sebastiana (karibu 86-96)
- Mfiadini Melitina (karibu 138-161)
- Wafiadini Vikta na Sosthene (karibu 304)
- Mtakatifu Mtawa Dorotheo, mkaa jangwani wa Misri (karne ya 4)
- Wafiadini ndugu Yusufu na Isaka wa Georgia (808)
- Mfiadini Lyudmila, binti wa mfalme wa Ucheki (927)
- Askofu Mtakatifu Kiprian, Mitropoliti wa Moscow, mtenda miujiza wa Urusi yote (1406)
- Mtakatifu Mtawa Kuksha wa Odesa, Mwungamaji (1964)
- Ikoni ya Mama wa Mungu iitwayo “Tazama Unyenyekevu” (1420)
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 16 Septemba katika kalenda ya kanisa ni 29 Septemba katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki