Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Septemba 2027 › 19 Septemba
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 19 Septemba 2027
Jumapili · Juma la 25 la Mwaka
Sikukuu na watakatifu
Dominika ya 25 ya Mwaka
Dominika · Rangi ya liturujia: kijani
Masomo ya siku
Somo la kwanza
Haimo katika tafsiri hii
Wimbo wa katikati
1Kwa kiongozi wa muziki; kwenye vyombo vya nyuzi. Maschil ya Daudi; wakati Ziphites alipokuja na kumwambia Sauli, “Hivi Daudi hakujificha pamoja nasi?” Uniokoe, Mungu, kwa jina lako, na kwa nguvu zako unihukumu. 2Usikie maombi yangu, Mungu; uyategee sikio maneno ya mdomo wangu. 3Kwa maana wageni wameinuka dhidi yangu, na watu wasio na huruma wanaitafuta roho yangu; nao hawakumuweka Mungu mbele yao. Selah 4Tazama, Mungu ni msaidizi wangu; Bwana ndiye anisaidiaye. 6Nitakutolea dhabihu kwa moyo mkunjufu; nitalishukuru jina lako, Yahwe, kwa maana ni jema.
Somo la pili
16Kwa kuwa palipo na wivu na ubinafsi upo, kuna vurugu na kila matendo maovu 17Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi, kisha kupenda amani, upole na ukarimu, yenye kujaa rehema na matunda mema, bila kupendelea watu fulani, na kweli. 18Na tunda la haki hupandwa katika amani kwa wale ambao wanatenda mambo ya amani. 4:1Ugonvi na migogoro miongoni mwenu vyatoka wapi? Haviinuki kutoka katika tamaa zenu mbaya zinazoleta vita ndani ya washirika wenu? 2Mnatamani kile msichokuwa nacho. Mnauwa na mnafukuzia kile msichoweza kuwa nacho. Mnapigana na kugombana, na bado hampati kwa sababu hamumwombi Mungu. 3Mnaomba na hampokei kwa sababu mnaomba kwa ajili ya mambo mabaya, ili kwamba muweze kuvitumia kwa tamaa zenu mbaya.
Injili
30Walitoka pale na kupitia Galilaya. Hakutaka mtu yeyote ajue walipo, 31kwa kuwa alikuwa anafundisha wanafunzi wake. Aliwaambia, “Mwana wa Adamu atafikishwa mikononi mwa watu, na watamuua. Atakapokuwa amekufa, baada ya siku tatu atafufuka tena.” 32Lakini hawakuelewa maelezo haya, na waliogopa kumwuliza. 33Ndipo walifika Karperinaumu. Wakati akiwa ndani ya nyumba aliwauliza, ''Mlikuwa mnajadili nini njiani”? 34Lakini walikuwa kimya. Kwani walikuwa wanabishana njiani kwamba nani alikuwa mkubwa zaidi. 35Alikaa chini akawaita kumi na wawili pamoja, na alisema nao, “Kama yeyote anataka kuwa wa kwanza, ni lazima awe wa mwisho na mtumishi wa wote.” 36Alimchukua mtoto mdogo akamweka katikati yao. Akamchukua katika mikono yake, akasema, 37“Yeyote ampokeaye mtoto kama huyu kwa jina langu, pia amenipokea mimi, na ikiwa mtu amenipokea, hanipokei mimi tu, lakini pia aliyenituma.”
Watakatifu wa siku
- Mt. Januari, askofu na shahidi
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki