Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Agosti 2027 › 25 Agosti
Kalenda ya Kiorthodoksi · 12 Agosti (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 25 Agosti 2027
Jumatano · Wiki ya 10 baada ya Pentekoste · Sauti ya 8
Sikukuu na watakatifu
Baada ya Sikukuu ya Kugeuka Sura kwa Bwana
Mfungo wa Kulala kwa Mama wa Mungu
Mfungo mkali (chakula kikavu: mkate, mboga, matunda)
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Waraka
4Na kama ni sahihi kwa mimi kwenda pia, watakwenda pamoja nami. 5Lakini nitakuja kwenu, wakati ninapitia Makedonia. Kwa kuwa nitapitia Makedonia. 6Labda naweza kukaa nanyi au hata kumaliza majira ya baridi, ili kwamba muweze kunisaidia katika safari yangu, popote niendako. 7Kwa kuwa sitarajii kuwaona sasa kwa muda mfupi. Kwani ninatumaini kukaa nanyi kwa muda fulani, kama Bwana ataniruhusu. 8Lakini nitakaa Efeso mpaka Pentekoste, 9kwa kuwa mlango mpana umefunguliwa kwa ajili yangu, na kuna maadui wengi wanipingao. 10Sasa wakati Timotheo akija, muoneni kwamba yuko na ninyi pasipo kuogopa, anafanya kazi ya Bwana, kama ninavyofanya. 11Mtu yeyote asimdharau. Mumsaidie katika njia yake kwa amani, ili kwamba aweze kuja kwangu. Kwa kuwa ninamtarajia aje pamoja na ndugu. 12Sasa kuhusiana na ndugu yetu Apolo. Nilimtia moyo sana kuwatembelea ninyi pamoja na ndugu. Lakini aliamua kutokuja kwa sasa. Hata hivyo, atakuja wakati ana nafasi.
Injili
28Lakini mnafikiri nini? Mtu mwenye wana wawili. Akaenda kwa moja na kumwambia, 'Mwanangu, nenda ukafanye kazi katika shamba la mizabibu 29leo. 'Mwana akajibu na kusema, 'sitakwenda, ' Lakini baadaye akabadilisha mawazo yake na akaenda. 30Na Mtu yule akaenda kwa mwana wa pili na kusema kitu kilekile. Mwana huyu akajibu na kusema, 'nitakwenda, bwana', lakini hakwenda. 31Yupi kati ya wana wawili aliyefanya matakwa ya baba yake? Wakasema, “Mwana wa kwanza.” Yesu akawaambia, “Kweli nawaambieni, wakusanya ushuru na makahaba wataingia kwenye ufalme wa Mungu kabla yenu kuingia. 32Kwa maana Yohana alikuja kwenu kwa njia iliyo nyoofu, lakini hamkumwamini, wakati wakusanya ushuru na makahaba walimwamini. Na ninyi, mlipoona hilo likitendeka, hamkuweza kutubu ili baadaye mumwamini.
Watakatifu wa siku
- Wafiadini Fotio na Aniketa na wengi pamoja nao (305-306)
- Watawa Wafiadini wa Belogorsk: Barlaamu, Sergio, Eliya, Vyacheslav, Yoasafu, Yohana, Antoni, Mika, Bessarioni, Mathayo, Euthimio, Barnaba, Demetrio, Sava, Hermogeni, Arkadio, Euthimio, Markelo, Yohana, Yakobo, Petro, Yakobo, Aleksanda, Theodoro, Petro, Sergio na Aleksi (1918)
- Mfiadini wa Kikasisi Basili, padri
- Wafiadini wa Kikasisi Leonida, Yohana na Nikolao, mapadri (1937)
- Mfiadini wa Kikasisi Aleksanda, Askofu wa Komana (karne ya 3)
- Wafiadini Pamfilo na Kapitoni
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 12 Agosti katika kalenda ya kanisa ni 25 Agosti katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki