Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Agosti 2027 › 24 Agosti
Kalenda ya Kiorthodoksi · 11 Agosti (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 24 Agosti 2027
Jumanne · Wiki ya 10 baada ya Pentekoste · Sauti ya 8
Sikukuu na watakatifu
Baada ya Sikukuu ya Kugeuka Sura kwa Bwana
Mfungo wa Kulala kwa Mama wa Mungu
Mfungo: chakula kilichopikwa bila mafuta
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Waraka
29Au pia watafanya nini wale waliobatizwa kwa ajili ya wafu? Kama wafu hawafufuliwi kabisa, kwa nini tena wanabatizwa kwa ajili yao? 30Na kwa nini tuko katika hatari kila saa? 31Kaka na dada zangu, kupitia kujisifu kwangu katika ninyi, ambayo ninayo katika Kristo Yesu Bwana wetu, natangaza hivi: nakufa kila siku. 32Inanifaidia nini, katika mtazamo wa wanadamu, kama nilipigana na wanyama wakali huko Efeso, kama wafu hawafufuliwi? “Acha basi tule na kunywa, kwa kuwa kesho tunakufa.” 33Msidanganywe: “Makundi mabaya huharibu tabia njema. 34“Muwe na kiasi! muishi katika haki! msiendelee kutenda dhambi. Kwa kuwa baadhi yenu hamna maarifa ya Mungu. Nasema hivi kwa aibu yenu. 35Lakini mtu mwingine atasema, “Jinsi gani wafu wanafufuliwa? Nao watakuja na aina gani ya mwili?” 36Wewe ni mjinga sana! Kile ulichopanda hakiwezi kuanza kukua isipokuwa kimekufa. 37Na kile unachopanda sio mwili ambao utakuwa, bali ni mbegu iliyochipua. Inaweza kuwa ngano au kitu kingine. 38Lakini Mungu ataipa mwili kama apendavyo, na katika kila mbengu mwili wake mwenyewe.
Injili
23Yesu alipofika hekaluni, wakuu wa makuhani na wazee wa watu wakamjia wakati alipokuwa akifundisha na kumwuliza, “Ni kwa mamlaka gani unafanya mambo haya? Na ni nani aliyekupa mamlaka haya?” 24Yesu akajibu na kuwaambia, “Nami tena nitawauliza swali moja. kama mkiniambia, nami vilevile nitawaambia ni kwa mamlaka gani ninafanya mambo haya. 25Ubatizo wa Yohana- ulitoka wapi, mbinguni au kwa wanadamu?” Wakahojiana wenyewe, wakisema, tukisema, ulitoka mbinguni, 'atatuambia, kwa nini hamkumwamini? ' 26Lakini tukisema, 'ulitoka kwa wanadamu, 'tunawaogopa makutano, kwa sababu wote wanamwona Yohana kama nabii.” 27Kisha wakamjibu Yesu na kusema, “Hatujui” Akawaambia pia, “Wala mimi sitawaambia ni kwa mamlaka gani nafanya mambo haya.
Watakatifu wa siku
- Mfiadini Euplo, shemasi mkuu (304)
- Mfiadini Susana, bikira, na pamoja naye Gayo, Papa wa Roma, Gavinio, padri, Klaudio, Maksimo, Prepedigna, Aleksanda na Kufio (295-296)
- Watawa Wafiadini Theodoro na Basili wa Mapango ya Kyiv (1098)
- Mtakatifu Mtawa Theodoro, mwana wa mfalme wa Ostroh, wa Mapango ya Kyiv (karibu 1438)
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 11 Agosti katika kalenda ya kanisa ni 24 Agosti katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki