Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Agosti 2027 › 25 Agosti
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 25 Agosti 2027
Jumatano · Juma la 21 la Mwaka
Sikukuu na watakatifu
Jumatano ya Juma la 21 la Mwaka
Kumbukumbu ya hiari · Rangi ya liturujia: kijani
Mt. Yosefu wa Kalasanzi, padre · Kumbukumbu ya hiari
Mt. Ludoviko · Kumbukumbu ya hiari
Masomo ya siku
Somo la kwanza
9Kwa kuwa ndugu, mnakumbuka kazi na taabu yetu. Usiku na mchana tulikuwa tukifanya kazi kusudi tusije tukamlemea yeyote. Wakati huo, tuliwahubiria injili ya Mungu. 10Ninyi ni mashahidi, na Mungu pia, ni kwa utakatifu wa namna gani, haki, na bila lawama tulivyoenenda wenyewe mbele yenu mnaoamini. 11Vivyo hivyo, mnajua ni kwa namna gani kwa kila mmoja wenu, kama baba alivyo kwa wanawe tulivyowahimiza na kuwatia moyo. Tulishuhudia 12kwamba mlipaswa kuenenda kama ulivyo mwito wenu kwa Mungu, aliyewaita kwenye ufalme na utukufu wake. 13Kwa sababu hiyo twamshukuru Mungu pia kila wakati. Kwa kuwa wakati mlipo pokea kutoka kwetu ujumbe wa Mungu mliosikia, mlipokea si kama neno la wanadamu. Badala yake, mlipokea kama kweli ilivyo, neno la Mungu. Ni neno hili ambalo linalofanya kazi kati yenu mnaoamini.
Wimbo wa katikati
7Niende wapi mbali na roho yako? Niende wapi niukimbie uwepo wako? 8Kama nikipaa mbinguni, uko huko; kama nikifanya kitanda changu Kuzimuni, tazama, uko huko. 9Kama nikipaa kwa mbawa za asubuhi na kwenda kuishi pande za mwisho wa bahari, 10hata huko mkono wako utaniongoza, mkono wako wa kuume utanishika. 11Kama nikisema, “Hakika giza litanifunika, na nuru inizungukayo itakuwa usiku,” 12Hata giza lisingweza kuwa giza kwako. Usiku ungeng'aa kama mchana, maana giza na nuru kwako vinafanana.
Injili
27Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnafanana na makaburi yaliyopakwa chokaa, ambayo kwa nje huonekana mazuri, lakini kwa ndani yamejaa mifupa ya wafu na kila kitu kilicho kichafu. 28Vivyo hivyo, nanyi kwa nje mwaonekana wenye haki mbele ya watu, lakini kwa ndani mmejaa unafiki na udhalimu. 29Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mwajenga makaburi ya manabii na kuyapamba makaburi ya wenye haki. 30Ninyi mwasema, kama tungeishi siku za baba zetu, tusingekuwa tumeshiriki pamoja nao kumwaga damu za manabii. 31Kwa hiyo mwajishuhudia wenyewe kwamba ninyi ni watoto wa hao waliowaua manabii. 32Pia ninyi mnakamilisha kujaza sehemu inayostahili dhambi ya baba zenu.
Watakatifu wa siku
- Mt. Yosefu wa Kalasanzi, padre
- Mt. Ludoviko
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki