Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Agosti 2027 › 16 Agosti
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 16 Agosti 2027
Jumatatu · Juma la 20 la Mwaka
Sikukuu na watakatifu
Jumatatu ya Juma la 20 la Mwaka
Kumbukumbu ya hiari · Rangi ya liturujia: kijani
Mt. Stefano wa Hungaria · Kumbukumbu ya hiari
Masomo ya siku
Somo la kwanza
11Watu wa Israeli walifanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana, nao wakawatumikia Mabaali. 12Wakaondoka kwa Bwana, Mungu wa baba zao, aliyewatoa kutoka Misri. Wakaifuata miungu mingine, miungu ya watu waliokuwa karibu nao, nao wakaisujudia. Wakamkasirisha BWANA kwa sababu 13waliondoka kwa Bwana na kumwabudu Baal na Maashtoreti. 14Hasira ya Bwana ikawaka juu ya Israeli, naye akawapa washambuliaji walioiba mali zao kutoka kwao. Aliwauza kama watumwa waliofanyika kwa nguvu za maadui zao waliowazunguka, hivyo hawakuweza kujikinga dhidi ya adui zao. 15Israeli walipokwenda kupigana, mkono wa Bwana ulikuwa dhidi yao kuwashinda, kama alivyowaapia. Na walikuwa katika shida kali. 16Ndipo Bwana akawainua waamuzi, waliowaokoa katika mikono ya wale waliokuwa wakiba mali zao. 17Hata hivyo hawakuwasikiliza waamuzi wao. Hawakuwa waaminifu kwa Bwana na wakajitoa wenyewe kama makahaba kwa miungu mingine na kuabudu. Waligeuka upesi na kuiacha njia waliyoishi baba zao-wale waliotii amri za Bwana-lakini wao wenyewe hawakufanya hivyo. 18Bwana aliinua waamuzi kwa ajili yao, Bwana akawasaidia waamuzi na kuwakomboa kutoka kwa mikono ya adui zao siku zote muamuzi aliishi. Bwana aliwahurumia walipougua kwa sababu ya wale waliowadhulumu na kuwasumbua. 19Lakini mwamuzi alipokufa, waligeuka na kufanya mambo ambayo yalikuwa mabaya zaidi kuliko baba zao walivyofanya. Wakaenda kuifuata miungu mingine kuitumikia na kuiabudu. Walikataa kuacha matendo yao yote mabaya au njia zao za ukaidi.
Wimbo wa katikati
34Hawakuyaharibu mataifa kama Yahwe alivyowaamuru, 35bali walichangamana na mataifa na walijifunza njia zao 36nao waliabudu sanamu, nazo zikawa mtego kwao. 37Waliwatoa wana wao na binti zao kwa mapepo. 39Walinajisiwa kwa matendo yao; katika matendo yao walikuwa kama malaya. 40Hivyo Yahwe aliwakasilikia watu wake, akawadharau watu wake mwenyewe. 43Mara nyingi alienda kuwasaidia, lakini waliendelea kuasi nao walishushwa chini kwa dhambi zao wenyewe. 44Hata hivyo, aliiangalia dhiki yao aliposikia kilio chao kwa ajili ya msaada.
Injili
16Tazama mtu mmoja akaja kwa Yesu na kusema, “Mwalimu, ni kitu gani kizuri ninachotakiwa kufanya ili nipate kuwa na uzima wa milele?” 17Yesu akamwambia, “Kwa nini unaniuliza ni kitu gani kizuri? Kuna mmoja tu aliye mwema, lakini kama ukitaka kupata uzima, shika sheria za Mungu.” 18Yule mtu akamwuliza, “Ni sheria zipi?” Yesu akasema, “Usiue, usizini, usiibe, usishuhudie uongo, 19waheshimu baba yako na mama yako, na mpende jirani yako kama nafsi yako.” 20Mtu yule akamwambia, “Mambo yote hayo nimeyatii. Bado ninahitaji nini? 21“Yesu akamwambia, “Kama ukitaka kuwa mkamilifu, nenda, ukauze ulivyo navyo, na uwape maskini, na utakuwa na hazina mbinguni. Kisha njoo unifuate.” 22Lakini kijana yule aliposikia yale Yesu aliyomwambia, akaondoka kwa huzuni, kwa sababu alikuwa na amemiliki mali nyingi.
Watakatifu wa siku
- Mt. Stefano wa Hungaria
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki