Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Agosti 2027 › 16 Agosti
Kalenda ya Kiorthodoksi · 3 Agosti (kalenda ya Juliani)
Masomo ya Kiorthodoksi ya siku — 16 Agosti 2027
Jumatatu · Wiki ya 9 baada ya Pentekoste · Sauti ya 7
Sikukuu na watakatifu
Watakatifu Watawa Isaka, Dalmato na Fausto (karne ya 4-5)
Mfungo wa Kulala kwa Mama wa Mungu
Mfungo mkali (chakula kikavu: mkate, mboga, matunda)
Hivi ndivyo kwa kanuni ya kimonaki. Parokiani, kipimo cha mfungo huamuliwa pamoja na baba wa kiroho, kulingana na afya, umri na hali.
Masomo ya siku
Waraka
31Lakini tukijichunguza wenyewe hatutahukumiwa. 32Ila tunapohukumiwa na Bwana, twarudiwa, ili tusije tukahukumiwa pamoja na dunia. 33Kwa hiyo, kaka na dada zangu, mkutanikapo mpate kula, ngojeaneni. 34Mtu akiwa na njaa, na ale nyumbani kwake, ili kwamba mkutanikapo pamoja isiwe kwa hukumu. Na kuhusu mambo mengine mliyoandika, nitawaelekeza nitakapokuja. 12:1Kuhusu karama za rohoni, kaka na dada zangu sitaki mkose kufahamu. 2Mwajua ya kuwa mlipokuwa wapagani mliongozwa kufuata sanamu zisizoongea, kwa njia zozote mliongozwa nazo. 3Kwa hiyo, nataka mfahamu kwamba hakuna yeyote anenaye kwa Roho wa Mungu akisema, “Yesu amelaaniwa.” Hakuna yeyote atakayesema, “Yesu ni Bwana,” isipokuwa katika Roho Mtakatifu. 4Basi kuna karama tofauti tofauti, bali Roho ni yeye yule. 5Na kuna huduma tofauti tofauti, bali Bwana ni yeye yule. 6Na kuna aina mbalimbali za kazi, lakini Mungu ni yeye yule azitendaye kazi zote katika wote.
Injili
1Muda huo huo wanafunzi wakaja kwa Yesu na kumwambia, “Ni nani aliye mkubwa katika ufalme wa mbinguni?” 2Yesu akamwita mtoto mdogo, akamweka katikati yao, 3na kusema, “Kweli nawaambieni, msipotubu na kuwa kama watoto wadogo hamtaweza kuingia katika ufalme wa Mungu. 4Hivyo yeyote ajishushaye kama mtoto mdogo, mtu kama huyo ni mkuu katika ufalme wa mbinguni. 5Na yeyote ampokeaye mtoto mdogo kwa jina langu anipokea mimi. 6Lakini yeyote asababishaye mmoja kati ya wadogo hawa wanaoniamini kuasi, itakuwa vizuri kwa mtu huyo jiwe kuu la kusagia likafungwa shingoni mwake, na kuzamishwa kilindini mwa bahari. 7Ole kwa dunia kwa sababu ya wakati wa kukwazwa! kwa kuwa haina budi kwa nyakati hizo kuja, lakini ole kwake kwa mtu yule nyakati hizo zitakuja kwa ajili yake! 8kama mkono wako au mguu wako ukikusababishia kukwazika, ukate na uutupe mbali na wewe. Ni vizuri zaidi kwako wewe kuingia kwenye uzima ukiwa bila mkono au kilema, kuliko kutupwa kwenye moto wa milele ukiwa na mikono yote au miguu yote. 9Kama jicho lako likikukwaza, uling'oe na ulitupe mbali na wewe. Ni vizuri zaidi kwako wewe uingie kwenye uzima na jicho moja, kuliko kutupwa kwenye moto wa milele ukiwa na macho yote. 10Tazameni kwamba msije mkamdharau mmoja wa wadogo hawa. Kwa maana nawambieni kuwa mbinguni kuna malaika wao siku zote wakiutazama uso wa Baba yangu aliye mbinguni.
Watakatifu wa siku
- Mtakatifu Mtawa Antoni Mroma, mtenda miujiza wa Novgorod († 1147)
- Mfiadini wa Kikasisi Vyacheslav, shemasi (1918)
- Mfiadini wa Kikasisi Nikolao, padri (1938)
- Mfiadini Razhden Mwajemi (457)
- Mtakatifu Mtawa Kosma, mkaa jangwani (karne ya 6)
Tarehe zinafuata kalenda ya Juliasi ya Kanisa la Urusi (kama Makanisa ya Serbia na Georgia na Mlima Athos): 3 Agosti katika kalenda ya kanisa ni 16 Agosti katika kalenda ya kiraia. Makanisa ya kalenda mpya (Ugiriki, Romania, Bulgaria, Ukraine…) huadhimisha sikukuu zisizohamishika na watakatifu katika tarehe ya kiraia yenyewe, siku 13 mapema, na baadhi ya masomo yao ni tofauti; Pasaka na siku zinazoitegemea ni zilezile.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki