Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Julai 2027 › 6 Julai
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 6 Julai 2027
Jumanne · Juma la 14 la Mwaka
Sikukuu na watakatifu
Jumanne ya Juma la 14 la Mwaka
Kumbukumbu ya hiari · Rangi ya liturujia: kijani
Mt. Maria Goretti, bikira na shahidi · Kumbukumbu ya hiari
Masomo ya siku
Somo la kwanza
22Yakobo akaamka wakati wa usiku, na akawachukua wakeze, wajakazi wake na wanaye kumi na wawili. Akawawavusha kijito cha Yaboki. 23Kwa njia hii akawapeleka kupitia chemichemi pamoja na mali yake yote. 24Yakobo akaachwa peke yake, na mtu akashindana naya mpaka alfajiri. 25Mtu yule alipoona kwamba hawezi kumshinda, akalipiga paja lake. Paja la Yakobo likatenguka alipokuwa akishindana naye. 26Yule mtu akasema, “Niache niende, kwani kunakucha.” Yakobo akasema, sitakuacha uende mpaka uwe umenibariki.” 27Yule mtu akamwuliza, “Jina lako ni nani?” Yakobo akasema, “Yakobo.” Yule mtu akasema, 28“Jina lako halitakuwa Yakobo tena, ila Israeli. Kwa kuwa umeshindana na Mungu na wanadamu na umeshinda.” 29Yakobo akamwambia, “Tafadhari niambie jina lako.” Akasema, “Kwa nini kuniuliza jina langu?” Kisha akambariki pale. 30Yakobo akapaita mahali pale Penieli kwani alisema, “Nimemwona Mungu uso kwa uso, na maisha yangu yamesalimika.” 31Jua likatoka wakati Yakobo anaipita Penieli. Alikuwa akichechemea kwa sababu ya paja lake. 32Ndiyo maana wana wa Israeli hawali kano ya paja iliyopo katika nyonga ya paja, kwa sababu yule mtu aliziumiza hizo kano alipotegua paja la Yakobo.
Wimbo wa katikati
1Maombi ya Daudi. Sikia ombi langu kwa ajili ya haki, Yawhe; uusikilize mwito wangu wa msaada. Uyasikilize maombi yangu yatokayo katika midomo isiyo na udanganyifu. 2Uthibitisho wangu na uje kutoka uweponi mwako; macho yako na yaone kile kilicho sahihi! 3Kama utaujaribu moyo wangu, kama utakuja kwangu wakati wa usiku, wewe utanitakasa na hautapata mipango yeyote ya uovu; mdomo wangu hautavunja sheria. 6Nakuita wewe, kwa kuwa unanijibu, Mungu; geizia sikio lako kwangu na usikilize ninapo ongea. 7Onyesha uaminifu wa agano lako katika namna ya ajabu, wewe uokoaye kwa mkono wa haki yako wale wanao kukimbilia wewe kutoka kwa adui zao. 8Unilinde kama mboni ya jicho lako; unifiche katika kivuli cha mbawa zako 15Bali mimi, nitauona uso wako katika haki; Nitashuhudiwa, pale nitakapo amka, na macho yako.
Injili
32Ndipo wale wanaume wawili walipokuwa wakienda zao, Tazama, mtu mmoja bubu aliyepagawa na pepo akaletwa kwa Yesu. 33Na pepo walipomtoka, yule mtu bubu akaanza kuongea. Umati ukashangazwa na kusema “Hii haijawahi kutokea katika Israel. 34Lakini mafarisayo walikuwa wakisema “ Kwa wakuu wa pepo, anawafukuza mapepo” 35Yesu akaenda kwenye miji yote na vijiji. Naye akaendelea kufundisha katika masinagogi, akihubiri injili ya ufalme, na kuponya magonjwa ya kila aina na udhaifu wa aina zote. 36Wakati alipotazama umati, naye aliwaonea huruma, kwa sababu walisumbuka na kuvunjika moyo. Walikuwa kama kondoo wasio na mchungaji. 37Naye akawaambia wanafunzi wake. “Mavuno ni mengi, lakini wafanya kazi ni wachache. 38Hivyo basi upesi mwombeni Bwana wa mavuno, ili kwamba atume wafanya kazi katika mavuno yake.”
Watakatifu wa siku
- Mt. Maria Goretti, bikira na shahidi
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki