Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Julai 2027 › 5 Julai

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 5 Julai 2027

Jumatatu · Juma la 14 la Mwaka

Sikukuu na watakatifu

Jumatatu ya Juma la 14 la Mwaka

Kumbukumbu ya hiari · Rangi ya liturujia: kijani

Mt. Antoni Maria Zakaria, padre · Kumbukumbu ya hiari

Masomo ya siku

Somo la kwanza

Mwa 28:10–22

10Yakobo akatoka Beersheba na akaelekea Harani. 11Akaja mahali fulani na akakaa pale usiku kucha, kwa kuwa jua lilikuwa limekuchwa. Akachukua mojawapo ya mawe katika eneo hilo, akaliweka chini ya kichwa chake, na akalala usingizi katika eneo hilo. 12Akaota na kuona ngazi imewekwa juu ya nchi. Ncha yake ilifika hata mbinguni na malaika wa Mungu walikuwa wakishuka na kupanda juu yake. 13Tazama, Yahwe amesimama juu yake na kusema, “Mimi ni Yahwe, Mungu wa Ibrahimu baba yako, na Mungu wa Isaka. Nchi uliyolala juu yake, nitakupa wewe na uzao wako. 14Uzao wako utakuwa kama mavumbi ya ardhi, na utaenea mbali kuelekea magharibi, mashariki, kaskazini, na kusini. Kupitia kwako na kupitia uzao wako familia zote za dunia zitabarikiwa. 15Tazama, mimi nipo nawe, na nitakulinda kila uendako, Nitakurudisha katika nchi hii tena; kwani sitakuacha. Nitafanya kila nililokuahidi.” 16Yakobo akaamka katika usingizi, na akasema, “Hakika Yahwe yupo mahali hapa, sikujua hili.” 17Akaogopa na kusema, “Eneo hili linatisha kama nini! Hili sio kingine zaidi ya nyumba ya Mungu. Hili ni lango la mbinguni.” 18Yakobo akaamka mapema asubuhi na akachukua jiwe alilokuwa ameliweka chini ya kichwa chake. Akaliweka kama nguzo na kumimina mafuta juu yake. 19Akapaita pale Betheli, lakini jina la kawaida la mji lilikuwa Luzu. 20Yakobo akatoa nadhiri, kusema, “Ikiwa Mungu atakuwa nami na atanilinda katika njia nipitayo, na atanipa mkate wa kula, na mavazi ya kuvaa, 21hata nikarudi salama katika nyumba ya baba yangu, ndipo Yahwe atakapokuwa Mungu wangu. 22Kisha jiwe hili nililoliweka kama nguzo litakuwa jiwe takatifu. Kutoka katika kila utakachonipa, kwa hakika nitakupa tena sehemu ya kumi.”

Wimbo wa katikati

Zab 91:1–4, 14–15

1Yeye aishiye katika makazi ya Aliye Juu atakaa katika uvuli wa mwenyezi. 2Nami nitasema kuhusu Yahwe, “Yeye ni kimbilio langu na ngome yangu, Mungu wangu, ambaye niaamini katika yeye.” 3Kwa maana yeye atakuokoa dhidi ya mtego wa mwindaji na dhidi ya pigo liletalo mauti. 4Yeye atakufunika kwa mbawa zake, na chini ya mbawa zake utapata kimbilio. Uaminifu wake ni ngao na ulinzi. 14Kwa sababu amejitoa kwangu, nitamuokoa. Nitamlinda kwa sababu yeye ni mwaminifu kwangu. 15Aniitapo, nitamjibu. Katika shida nitakuwa naye; nitampatia ushindi na nitamuheshimu.

Injili

Mt 9:18–26

18Wakati Yesu alipokuwa akiwaambia mambo hayo, tazama, afisa akaja akasujudu mbele yake, Naye akasema, “ Binti yangu amefariki punde, lakini njoo na uweke mkono wako juu yake na yeye ataishi tena. 19Ndipo Yesu akasimama na kumfuata na wanafunzi wake pia. 20Tazama, mwanamke ambaye alikuwa anatokwa damu kwa muda wa miaka kumi na miwili, akaja karibu na Yesu na akagusa sehemu ya pindo la vazi lake. 21Kwa kuwa alisema, “Endapo nitagusa vazi lake, nami nitapata uponyaji.” 22Yesu akageuka na kumtazama na kumwambia. “Binti, jipe moyo, imani yako imekufanya upone,” Na muda huo huo mwanamke akapata uponyaji muda huo. 23Na Yesu alipofika kwenye nyumba ya afisa, naye aliwaona wapiga tarumbeta na umati wa watu ulikuwa ukipiga kelele. 24Naye akasema, “Tokeni hapa, kwa kuwa binti hajafa, bali amelala. Lakini wao walicheka na kumkebehi. 25Na wale watu walipotolewa nje, naye akaingia chumbani na kumshika mkono na msichana akaamka. 26Na habari hizi zikaenea katika mji mzima.

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 5 Julai

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki