Bible Explorer Pata programu

Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Juni 2027 › 19 Juni

Kalenda ya Kikatoliki

Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 19 Juni 2027

Jumamosi · Juma la 11 la Mwaka

Sikukuu na watakatifu

Jumamosi ya Juma la 11 la Mwaka

Kumbukumbu ya hiari · Rangi ya liturujia: kijani

Mt. Romualdo, abati · Kumbukumbu ya hiari

Masomo ya siku

Somo la kwanza

2 Kor 12:1–10

1Ni lazima nijivune, lakini hakuna kinachoongezwa na hilo. Bali nitaendelea kwenye maono na mafunuo kutoka kwa Bwana. 2Namjua mtu mmoja katika Kristo ambaye miaka kumi na minne iliyopita ambaye—ikiwa katika mwili, au nje ya mwili, mimi sijui, Mungu anajua—alinyakuliwa juu katika mbingu ya tatu. 3Na ninajua kwamba mtu huyu—ikiwa katika mwili, au nje ya mwili, mimi sijui, Mungu anajua— 4alichukuliwa juu hadi paradiso na kusikia mambo matakatifu sana kwa mtu yeyote kuyasema. 5Kwa niaba ya mtu kama huyo nitajivuna. lakini kwa niaba yangu mwenyewe sitajivuna. Isipokuwa kuhusu udhaifu wangu. 6Kama nikitaka kujivuna, nisingekuwa mpumbavu, kwa kuwa ningekuwa ninazungumza ukweli. Lakini nitaacha kujivuna, ili kwamba asiwepo yeyote atakayenifikiria zaidi ya hayo kuliko kinachoonekana ndani yangu au kusikika kutoka kwangu. 7Sitajivuna pia kwa sababu ya hayo mafunuo ya aina ya ajabu. Kwa hiyo, hivyo sitajawa na kiburi, mwiba uliwekwa ndani ya mwili wangu, mjumbe wa shetani kunishambulia mimi, ili nisigeuke kuwa mwenye majivuno. 8Mara tatu nilimsihi Bwana kuhusu hili, ili yeye kuundoa kutoka kwangu. 9Naye akaniambia, “Neema yangu inatosha kwa ajili yako, kwa kuwa nguvu hufanywa kamili katika udhaifu. Hivyo, ningetamani zaidi kujivuna zaidi kuhusu udhaifu wangu, ili kwamba uwezo wa Kristo uweze kukaa juu yangu. 10Kwa hiyo ninatosheka kwa ajili ya Kristo, katika udhaifu, katika matukano, katika shida, katika mateso, katika hali ya masikitiko. Kwa kuwa wakati nikiwa dhaifu, kisha nina nguvu.

Wimbo wa katikati

Zab 34:7–12

7Malaika wa Yahwe huweka kambi wakiwazunguka wale wanao muogopa yeye na kuwaokoa. 8Onjeni muone Yahwe ni mzuri. Amebarikiwa mtu yule ambaye Yahwe ni kimbilio lake. 9Muogopeni Yahwe, ninyi watu watakatifu wake. Hakuna kupungukikwa kwa wale wanao mhofu yeye. 10Simba wadogo wakati mwingine hukosa chakula na kuteseka kwa njaa, bali wale wamtafutao Yahwe hawatapungukiwa chochote kilicho kizuri. 11Njoni, wana, mnisikilize mimi. nitawafundisha ninyi hofu ya Yahwe. 12Mtu nani aliyepo ambaye anatamani maisha na anapenda kuwa na siku nyingi, ili kwamba aweze kuona vizuri?

Injili

Mt 6:24–34

24Hakuna hata mmoja anayeweza kuwatumikia mabwana wawili, kwa kuwa atamchukia mmoja na kumpenda mwingine, au la sivyo atajitoa kwa mmoja na kumdharau mwingine. Hamuwezi kumtumikia Mungu na mali. 25Kwa hiyo nakuambia, usiwe na mashaka kuhusu maisha yako, kuwa utakula nini au utakunywa nini, au kuhusu mwili wako, utavaa nini. Je! Maisha si zaidi ya chakula na mwili zaidi ya mavazi? 26Tazama ndege walioko angani. Hawapandi na hawavuni na hawakusanyi na kutunza ghalani, lakini Baba yenu wa mbinguni huwalisha wao. Je ninyi si wa thamani zaidi kuliko wao? 27Na ni nani miongoni mwenu kwa kujihangaisha anaweza kuongeza dhiraa moja kwenye uhai wa maisha yake? 28Na kwa nini mna kuwa na wasiwasi kuhusu mavazi? Fikiria kuhusu maua kwenye mashamba, jinsi yanavyokua. Hayafanyi kazi na hayawezi kujivisha. 29Bado ninawaambia, hata Sulemani katika utukufu wake wote hakuvikwa kama mojawapo ya haya. 30Ikiwa Mungu anayavalisha majani katika mashamba, ambayo yadumu siku moja na kesho yanatupwa katika moto, je ni kwa kiasi gani atawavalisha ninyi, ninyi wenye imani ndogo? 31Kwa hiyo msiwe na wasiwasi nakusema, 'Je tutakula nini?' au “Je tutakunywa nini?” au “Je tutavaa nguo gani?” 32Kwa kuwa mataifa wanatafuta mambo haya, na Baba yenu wa mbinguni anajua kuwa mnahitaji hayo. 33Lakini kwanza tafuteni ufalme wake na haki yake na haya yote yatakabidhiwa kwako. 34Kwa hiyo, usione shaka kwa ajili ya kesho, kwa kuwa kesho itajishughulikia yenyewe. Kila siku inatosha kuwa na tatizo lake yenyewe.

Watakatifu wa siku

Watakatifu wa 19 Juni

Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.

Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki