Mwanzo › Masomo ya Biblia ya kila siku › Juni 2027 › 13 Juni
Kalenda ya Kikatoliki
Masomo ya Misa (Kikatoliki) — 13 Juni 2027
Jumapili · Juma la 11 la Mwaka
Sikukuu na watakatifu
Dominika ya 11 ya Mwaka
Dominika · Rangi ya liturujia: kijani
Masomo ya siku
Somo la kwanza
22Bwana Yahwe asema hivi, 'Basi mimi mwenyewe nitaichukua sehemu ya juu ya mti wa mkangazi, na nitaupanda mbali na matawi yake laini. Nitaukata, na mimi mwenyewe nitaupanda juu ya mlima mrefu. 23Nitaupanda juu ya milima ya Israeli hivyo utazaa matawi na kuzaa matunda, na utakuwa mkangazi wa fahari ili kwamba kila ndege arukaye ataishi chini ya huo. Watajenga viota chini ya kivuli cha matawi yake. 24Kisha miti yote ya shambani itajua kwamba mimi ni Yahwe. Nimeishusha miti mirefu na nimeiinua juu miti mifupi. Naunyausha mti mbichi na kuufanya mti mkavu kuchanua. Mimi Yahwe, nimesema hivyo hii itatokea; nami nimelifanya hili.'”
Wimbo wa katikati
1Zaburi, wimbo kwa ajili ya siku ya Sabato. Ni jambo jema kumshukuru Yahwe na kuliimbia sifa jina lako, Uliye Juu, 2kutangaza uaminifu wa agano lako wakati wa asubuhi na uaminifu wako kila usiku, 12Wenye haki watastawi kama mtende; watakua kama mwerezi wa Lebanoni. 13Wamepandwa katika nyumba ya Yahwe; wakistawi katika nyua za Mungu wetu. 14Wao huzaa matunda hata uzeeni; hukaa safi na wenye afya, 15kutangaza kuwa Yahwe ni wa haki. Yeye ni mwamba wangu, na hakuna udhalimu ndani yake.
Somo la pili
6Kwa hiyo muwe na ujasiri siku zote. Muwe macho kwamba wakati tuko nyumbani katika mwili, tuko mbali na Bwana. 7Kwa kuwa tunatembea kwa imani, sio kwa kuona. Kwa hiyo tunaujasiri. 8Ni bora tuwe mbali kutoka kwenye mwili na nyumbani pamoja na Bwana. 9Kwa hiyo tunaifanya kuwa lengo letu, kama tukiwa nyumbani au mbali, tumpendeze yeye. 10Kwa kuwa lazima wote tuonekane mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, ili kwamba kila mmoja aweze kupokea kile kinachostahili kwa mambo yaliyofanyika katika mwili, ikiwa ni kwa uzuri au kwa ubaya.
Injili
26Na akasema, “Ufalme wa Mungu umefananishwa na mtu aliyepanda mbegu katika udongo. 27Alipolala usiku na kuamka asubuhi, na mbegu zikachipuka na kukua, ingawa hajui ilivyotokea. 28Dunia hutoa mbegu yenyewe; kwanza majani, halafu maua, halafu mbegu zilizo komaa. 29Na wakati mbegu itakapokua imeiva mara hupeleka mundu, kwa sababu mavuno yamewadia.” 30Na akasema, “tuufananishe ufalme wa Mungu na kitu gani, au tutumie mfano gani kuuelezea?. 31Ni kama mbegu ya haradali, ambapo ilipopandwa ni ndogo sana kuliko mbegu zote duniani. 32Hata, wakati imepandwa, inakuana kuwa kubwa zaidi ya mimea yote ya bustani, na inafanya matawi makubwa, hata ndege wa mbinguni huweza kufanya viota vyao kwenye kivuli chake.” 33Kwa mifano mingi alifundisha na alisema neno kwao, kwa kadiri walivyoweza kuelewa, 34na hakusema nao bila mifano. Lakini wakati alipokuwa peke yake, akawaelezea kila kitu wanafunzi wake.
Watakatifu wa siku
- Mt. Antoni wa Padua, padre na mwalimu wa Kanisa
Kalenda ya Jumla ya Kirumi; baraza la maaskofu linaweza kuhamisha baadhi ya maadhimisho (Epifania, Kupaa Bwana, Ekaristi Takatifu) hadi Jumapili au kuongeza yake. Kitabu cha masomo: mzunguko wa Jumapili B, mwaka wa siku za kazi I.
Vyanzo: Swahili Unlocked Literal Bible · © Door43 World Missions Community, CC BY-SA 4.0 · Vyanzo na haki